- Thread starter
- #21
Well said! Ila dola gani isiyo na jeshi?Zanzibar siyo nchi (Country), bali ni dola(State) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu muungano uliwekwa kimkataba na hati idhini (Union Charter/Articles of the Union). Hivyo Zanzibar ilipunguza sehemu ya uhuru wake kujiwala (National Sovereignty) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pili, suala la ajira lina pembe mbili. Kuna pembe ya Muungano na pembe ya Zanzibari. Watanganyika wapo Zanzibari na wanafanya kazi, lakini ni katika zile sehemu za mambo yanayohusu Muungano tu. Jambo kama hili liko hata kule Hong-Kong Uchina, na maisha yanaenda kama kawaida.
Tatu, suala la bendera siyo shida, maana bendera ni utambulisho tu (Emblem of Identity). Hata wewe ukiamua kuwa na bendera yako unaweza kuitengeneza na kuisajili kupitia HAKI-MILIKI (Intellectual Property). Nchini Marekani kila jimbo lina bendera yake na maisha yanaenda vizuri tu. Tena wananda mbali kabisa na kutumia bendera (The Confederate Flag) ya madola ya kusini (Dixie-Land) ambayo yaliasi muungano.
Nne, nadhani jina Raisi ni cheyo tu, hivyo unaweza leo ukamua kumuita Raisi wa Zanzibari wa Zanzibar Waziri Mkuu wa visiwani, Gavana,Sultani au Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Lakini muhimu kujiuliza ni hili: Je, madaraka yake ya Uraisi yanaishia wapi na ukimlinganisha na Raisi mwenzake ??? Utakuja kufahamu ni kwamba Raisi wa Zanzibari hauvuki maji ya Pemba na Unguja, lakini Raisi wa Tanganyika madaraka yake yanavuka maji na kufika Pemba hadi Unguja, katika ngazi ya kitaifa hadi kichama.
Tano, mashirikisho mengi huwa na mihimili na taasisi zinazojitegemea kama mahakama, bunge na serikali zao. Wengine kama Ethiopia walienda mbali zaidi kuwa hata vikosi vyao binafsi vya ulinzi. Nchini Marekani kuna baadhi ya majimbo yana nguvu sana hadi kumuwezesha Gavana kutoa adhabu ya kifo. Hivyo hili la Zanzibar lisikutatize kabisa mkuu.
Sita, kuhusu uwakilishi wa Zanzibari kwenye siasa za kimataifa hilo ni jambo la kawaida sana maana sheria za kimataifa hazikatazi. Tokea mwaka 1945 hadi 1991 Umoja wa Kisovieti ulikuwa una viti vitatu kule Umoja wa Mataifa ambavyo ni vya Urusi, Ukraine na Belarus ilhali wote wanatoka kwenye nchi moja iitwayo The Union of Soviets Socialist Republics (USSR). Hivyo hapa napo binafsi sioni tatizo kabisa.
Saba, kuhusu taasisi kujiendesha kwa utofauti hilo linatokana na uwepo wa madara ya ndani ya kujiendesha (Internal Sovereignty). Hata nchini Uchina, Hong-Kong inajiendesha kitofauti kabisa, nchini Marekani jimbo kama California ambalo huwa linajiendesha kitofauti kabisa na sera zake za kiliberi. Ambacho wengi kinatukera ni kwamba Tanganyika kutoweza kujiamulia mambo yake binafsi. Tunalitaka taifa letu.
Nane, hili la mikopo nakubaliana na wewe kabisa. Zanzibari haitakiwi ipate fungu lolote lile kwenye masuala yasiyo ya muungano (Non-Union Matters) ambayo yanaihusu Tanganyika. Mbaya zaidi hili la kukopa kupitia mngongo wa Tanganyika, ilhali sheria za kimataifa zinaruhusu Zanzibar iweze kukopa yenyewe binafsi. Katiba ya Ujerumani inaruhusu Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi kuingia katika mikataba binafsi ya kimataifa na nchi nyingine. Hivyo Ujerumani Mashariki inaruhusiwa hadi kukopa nje, ili mradi tu itoe taarifa kwa serikali ya Muungano.
Tunataka Zanzibar nao wakope kwa jina lao, maana inaruhusiwa kabisa. Huu ujanja wa kutaka kuimiza Tanganyika, umenza kututia kinyaa watu wengi na kutukera sana. Hasahasa unapofanywa na Raisi Mzanzibari ambaye kiuhalisia hakutakuwa kabisa kugusa mambo ya Tanganyika.
Tisa, kuhusu ardhi. Wazanzibari ni watu wenye midomo sana na wanapenda kuongea siasa zao ambazo zimejaa ubaguzi wa rangi na dini. Lakini ukweli mchungu ni kwamba kuna mambo ambayo Tanganyika ikitutumua misuli, lazima wataumia sana. Mwaka 2014 ilifanyika tafiti na kufahamika kwamba kule Zanzibar (1 Square Kilometer inakaliwa na watu 200) wakati huku Tanganyika (1 Square Kilometer inaliwa na watu 20-30).
Tukisema tuanze kuwakazia, nadhani watu kama Raisi Hussein Mwinyi, Raisi Samia, Bakhresa na wapemba wengine ambao wako Dar es Salaam kisheria inabidi wamiliki ardhi kama wawekezaji kupitia kitu kiitwacho The Derivetive Right. Lakini jambo jingine kubwa utafiti wa mafuta ya Zanzibar ulifanywa kipindi cha Raisi Magufuli na kutambulika kwamba baadhi ya miamba yenye mafuta ambayo Zanzibari ingechimba imefika hadi Tanganyika, tena sehemu kubwa iko Tanganyika.
Kiukweli mimi natamani Tanganyika irudi, ikiwezekana kabisa tuvunje huu muungano.
Halafu nyie Moderators mliopo ONLINE (Boqin , Wand , BlackBold , YinYang , Active , Mhariri ) tafadhali tuheshimiane sana. Hili la mimi kuweka nukta .... ili kuwahi nafasi ya kuandika muda nitakaotaka mimi binafsi haliwahusu kabisa. Sasa kujifanya mko kichwani mwangu na kutabiri kwamba navuruga mijadala ni upigaji ramli na uchwani. Nimewavumilia sana kuna siku mkanipa BAN, leo mmefuta nilichoandika. Tafadhali sana heshimuni uhuru wangu na tusipangiane cha kuandika.
Kwenye suala la ajira, hujanishawishi mkuu.
Ajira zote za Zanzibar ni lazima uwe na kitambulisho cha mkazi.. labda nafasi nyeti za wizara/taasisi zinazihusiana na muungano mfano ofisi ya makamu wa rais.