Eee Mungu wangu ni nini tena hii? dah! unbelievable! hatari sana hii ndugu zangu watanzania wenzangu. Tunu ya amani na mshikamano katika nchi yetu naona sasa iko mashakani more than ever katika historia ya nchi hii.
Ukijaribu ku-sum up matukio ya harakati za kidini za hivi karibuni na jinsi serikali inavyoshadidia na kusapoti upande mmoja unapata tabu sana.
Hapa hatujamaliza kupata suluhu juu ya swala la haki ya kuchinja baina ya waislamu na wakristo ambapo serikali inaonekana kuwa upande wa waisilamu kwa sababu ambazo wanazijua wao wenyewe. Mchungaji ameuwawa na bado tupo kwenye maombolezo haya mengine yanatokea.......
Juzi kati padre ambrose alikoswakoswa kuuwawa huko huko Zanzibar na hakuna mtu yeyote aliyechukuliwa hatua. kabla ya tukio la leo kulikuwa na vipeperushi vinavyodai kwamba mission iliyofeli ya kumuua padre ambrose siyo mwisho wa mapambano, na kweli hatujakaa sawa tunasikia padri Mushi kauwawa. Serikali nayo imekaa kimya tu, wahusika waliozalisha na kusambaza vipeperushi hivyo wako huru na wanaendeleza mambo yao. tusisahau kwamba Ijumaa juzi hapa waislamu pamoja na kutoruhusiwa kuandamana lakini waliandamana.
machungu ya uchomaji makanisa haujaisha bado, in fact leo jumapili tumeendelea kuchanga kwa ajili ya kujenga kanisa la Mbagala lililochomwa moto.
Tunaelekea wapi? Na ni kwa nini uongozi wa juu wa nchi hii imekuwa ikisaidia kueneza uislamu hata ikibidi kutoa uhai wa watu na kuhatarisha amani na mshikamano wetu. Kwani nchi hii zi haina dini kwa mujibu wa katiba?.Tumeona sasa udini umeingia hadi bungeni, michango ya wabunge huegemea dini yao. Aibu kubwa sasa hii.
Enyi wakristo, watu wa Mungu tuamkeni sasa, ni lazima tena ni muhimu haya mambo sasa tuyachukulie kwa uzito wake na kutafuta namna nzuri ya kukabiliana nayo.
Eeh Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, wewe uliye mwema kwa viumbe vyako, tunakuomba Amani yako itamalaki, tunakuomba Umoja na Udugu na Upendo katika nchi yetu. Shetani Baba wa uharibifu, achinjae na kuua ashindwe katika Jina la Yesu, Mwana wako na Mwokozi wetu.
Jina lako Baba Lihimidiwe Milele na Milele.
Na semeni wote Ameeeen!