Wweed
JF-Expert Member
- Jan 13, 2013
- 255
- 42
Mauji ya Daudi Mwangosi, kuweka ndani kwa Sheikh Ponda,Sheikh Farid na wenzake, kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka, na hata kufungiwa na gazeti la Mwanahalisi, kunathibitisha pasi na shaka kuwa serikali ya CCM inayo uwezo, nia na ujasiri wa kutenda pale tu maslahi yao yanapoguswa.
Mauji ya Padre Evarist Mushi huko Zanzibar si kwamba yamefanywa na waislam, bali yamefanywa na wahalifu wanaotumia kivuli cha dini kutimiza azma zao. Na wahalifu hawa wamekuwa na wakati mzuri sana wa kufanya mambo yao kwa sababu serikali ya CCM ina 'interest' kubwa kwenye udini kwani ni njia muhimu ya kugawa na kutawala Watanzania.
Kama kweli serikali ya CCM ingekuwa inaguswa (kimaslahi) na misuguano ya udini wangeshachukua hatua mapema kama walivyofanya kwa Mwangosi, Dr Ulimboka, Sheikh Ponda, na Mwahalisi.
Na huko tuendekako, unless mambo yabadilike - tena kwa haraka - basi Watanzania andaeni viroba vya kubebea vifusi. Makanisa Zanzibar yatapigwa mabomu ya nguvu. Hiki ndicho kinachofuta.
Mazishi ya Padre Evarist Mushi.
Kama kumbukumbu zangu ni sahihi, Padre Evarist Mushi anatokea shirika la White Fathers. Ingekuwa vema kama uongozi wa Kanisa Katoliki wangemzika Padre Evarist Mushi kwenye Seminary yao - USA-River, Arusha. Wakimzika huyu Padre Zanzibar, haitachukuwa muda mrefu, watu 'wasiojulikana - tena, watalifukuwa kaburi lake. Ni matumaini yangu kuwa Kanisa litamrudisha huyu Padre mahali ambapo atapumzika kwa amani.
Mh hujatizama hiyo clip?,ustaath Illulakasema ''WAZI KWEUPEe'' kuwa waislam wasio lege lege wa-ue viongozi wa KI-KRISTO aither kwa kujificha o kujionesha vyovyote vile suala ni kuua mpaka waogopwe,sasa wewe hili la wahuni umelitoa wapi?,wahuni huwa wana ua kwa maslahi ya mali je hao wali iba/kujaribu kuiba baada ya mauaji?,Ukisema WAISLAM SIASA KALI NITAKUELEWA ILA WAHUNI......! mmmmmm acha wewe.haya mambo yanaratibiwa na serikali inaogopa kuwa imara kwayo.

