NasDaz kinachosikitisha hakuna juhudi za wazi za makusudi kutoka kwa hao Waislamu safi kuelimisha wenzao ubaya wa haya!
Ndugu yangu MTAZAMO, unataka kuniambia hao unawaowaita Waislamu safi wanafurahishwa na hayo mambo?! Watafurahishwa vipi wakati wanawafanya wajiskie vibaya kwa kuonekana wao ni watu hatari?! Trust me, hao watu hawasukumwi na dini bali wana agenda binafsi na dini ni kama cover tu! Na kama wanafanya hivyo kwa ajili ya dini basi hawaifahamu dini....huo ndio ukweli wenyewe!!
Ngoja nikupe mfano wa yale yanayotokea Mashariki ya Kati!! Unakuta Mwislamu wa Suni anaenda kujilipua kwenye Msikiti wa Shiha...sasa huyo nae anapigania dini? Dini ipi wakati wote ni dini moja na walichotofautiana ni madhehebu?! Lakini ukifuatilia kwa makini, utakuta dhehebu moja lina-opress dhehebu lingine labda kwa vile dhehebu husika lina watu wazito serikalini au ndio wanaoshikilia na kumiliki keki ya taifa! jambo hili limetokea sana Iraq baada ya Saadam kuondolewa madarakani! sasa hiyo utaita dini? Tuje kwa Osama ambae ndo alifanya sura ya Uislamu iharibike kabisa duniani!! Je, huyu nae alikuwa anapigania dini?! Hivi ulishawahi kusikia Al-Qaeda ya Osama ikiripua Kanisa?! Hivi umeshapata kusikia Osama akiilenga Vatican au Cantebury?! Why target yake kubwa ilikuwa ni USA pamoja na UK? Why not at least Italy yaliko Makao Makuu ya RC au German iliko Lutheran?! USA na ukristo wapi na wapi? Hivi wewe unaweza kutamka kwa yakini kabisa kwamba Ukristo wa Marekani ni tishio kwa Uislamu? Kwa Ukristo upi walio nao? Hivi kuna uhusiano gani kati ya ukristo na overseas embassies ambazo Osama alikuwa anazilenga?!
Nimekupa mfano wa Osama kukuonesha ni namna gani watu wanatumia dini wakati ukiangalia kwa makini unakosa uhusiano wa matendo yao na kile wanachodai kukipigania! Osama alikuwa anapigana vita anayoifahamu mwenyewe...(Binafsi nahisi ni vita za kutetea Waarabu wenzake au ni vita dhidi ya watu wa magharibi)! Lakini kama ilivyo kawaida, njia moja wapo ya kushinda vita ni kuwa mzuri wa propaganda!! Osama alifahamu fika kwamba Waarabu hawapo kila mahala duniani, lakini Waislamu wapo kila mahala! Hivyo alifahamu kabisa akisema napigania Uislamu basi anaweza pata sapoti hata toka kwa wandengereko wa Tanzania kuliko kusema anapigania Waarabu! Na hilo akafanikiwa....!
Sasa basi, kwa haya yaliyotokea ZNZ, kwanza ni mapema mno ku-conclude ni nani amefanya mauaji hayo! Lakini vyovyote iwavyo, si sahihi kusema kwamba hao wauaji wamesukumwa na Uislamu...! Uisllamu kwa maana ipi? JIHAD au nini? JIHAD haipo hivyo....JIHAD kwa mujibu wa Uislamu ni pale inapotokea kuwapo kundi la watu kuwazuia Waislamu kwa namna yoyote ile kufanya ibada zao...mathalani, leo aje kiongozi mmoja na akatoa amri kwamba misikiti yote ifungwe na ni marufuku Waislamu kusali....hapo JIHAD ruksa! Na hapa ndipo Muislamu anapoambiwa kufa kwa ajili ya dini yake! Na hili hata Wakristo wanaweza kufanya....sizani kama nchi itakalika hii leo hii itangazwe kwamba marufuku Wakristo kwenda kanisani!
Sasa basi, kutokana na mfano mdogo wa JIHD ni nini hasa, je hao wa ZNZ wanapigana JIHAD ipi?
binafsi naona kinachotokea ZNZ ni ZNZ Politics! Ninavyozungumzia ZNZ politics hapa simaanishi siasa za CCM na CUF....bali siasa za "tuachieni ZNZ yetu"; hatutaki muungano!! Hawa wasiotaka muungano wana chuki ya wazi na watu wa Bara! Kwa bahati mbaya kabisa, makanisa yanaonekana ndio chimbuko la watu wa Bara!! Trust me, leo hii ikitokea Wakristo wote ZNZ wametoka na kurudi bara, wauaji hao sasa watawageukia Wabara wengine kwa visingizio vingine!