Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Huyu ni mtaka Shari, fujo, vita ndiyo maana mawazo yake yote yako Rwanda, Somalia,Libya na Iraq na si nje ya hapo
 
Huyu Raisi Mimi namkubali sana!!
Hata Kama Ni Mimi nisingesaini kwakweli!
Nyie mnaopenda kubembelezwa Safari hii mjipange upya!!
 
Hi
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

Hi fedha za nani?? Ni kodi zetu hizi ndizo anapandishie ngebe!!?? No please tumetengeneza sheria na taratibu namna ya kutumia fedha zetu ZIFUATWE!!
 
Kama ni Rais tu, kwa kweli tumempata!

Mwl. Nyerere aliwahi kusema kuhusu udhaifu wa katiba yetu na namna inavyoruhusu Rais aliyepo madarakani (nakumbuka alitumia neno "kichaa") kujigeuza kuwa mtawala wa kiimla (ndio mnaita dikteta uchwara?) kwa urahisi sana.
 
Kwa kweli ni MUNGU tu ndo atakaye amua hatma ya Taifa hili .

Maana daaah yamezidi sasa [emoji17]
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

kadri siku zinavyosonga mbele naona huyu mzee anazidi kujidhalilisha kwa kauli zake mbovu....time will tell.
 
Hata Shein sidhani kama yuko sawa! Otherwise hawa jamaa hawajui kuwa wananchi wanawatazama.

Wanachokiongea majukwaani hakuna mwananchi mwenye akili timamu ataona ni sawa!

Naona kama vile wameamua kuwa KAMA NOMA NA IWE NOMA!
 
Binafsi nimejazwa hofu sana na hii hotuba ya Rais Magu, pale kibanda maiti. Anasema anayewagawa watz ni shetan, lakini anakili kuwa yeye ndiye bingwa wa kuwabagua wapinzani wake kwenye serikali yake!
 
Kwani anadhani Dr. Shein anasaini stahiki za mpinzani wake (Maalim Seif) kwa hiyari yake? Huyo baba Jesca hajui kwamba kuna taratibu za kisheria zimewekwa na zimetajwa kwenye katiba kuhusu stahiki za wastaafu level ya Maalim Seif au ndo anadhihirisha ile tabia yake ya kutofuata utawala wa sheria?
Mi nimeangalia taarifa ya habari, nikatokwa machozi. Ee Mungu tudaidie
 
Rais kasema "Kama mtu anakataa mkono wako nawe kataa mkono wake kwa mambo yake, nikuombe nawe uwe unamkatalia mkono wako kufanye mambo yake' Anamuomba Mungu kumpa walau robo ya moyo wa Shein lakini naye ambae walau robo ya mawazo yake."

Wacha kupotosha watu
Kwahiyo umesikia peke yako?
 
Back
Top Bottom