Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Mkulu hana kifua cha kubeba maudhi akakaa kimya..to me ishara mojawapo ya maturity ni kuweza kuhimili makwazo na ukakaa kimya
 
Yeye anamshangaa Shein kusaini makaratasi ya mtu baada ya kukataa kumpa mkono, lakini hashangai yeye aliyejitoa kafara ya kupambana na mafisadi kushiriki ufisadi wa boti bovu la bilioni nane kisha kujikausha kama siye vile, hashangai kuigwaya Lugumi hata kuiogopa kuitaja tu!!! Kweli hawakukosea waliosema ukistaajabu ya Mussa......
Ile picha ya Seif akikataa kuupokea mkono Wa Shein inabidi tuitengenezee T-shirts na kuzivaa kwa wingi ili kuendelea kumkera mkuu.
Angalau tupate na sisi kitu cha kumkera.
 
Tangu lini Magufuli akawa na kauli zenye busara..??

Huyu ana nia mbaya na kuwachonganisha Wazanzibar tu, kauli zake zote ni za ovyo kwa wazanzibar sio za kuunganisha ni za kuwagawa ili aendelee kuwatawala.
 
Sasa mna lalamika nini????????? Si mbadilishe katiba? Mnapiga kekele tuu bila maana yoyote.
 
Hiyo sheria ya Seif kulipwa posho iko kwenye bible au Qur'an?

Si inatenguliwa tu anakula jeuri yake au inasainiwa kila baada ya miezi saba.

Mi nakerwa na unafiki tu,kumpongeza Seif kwa kile alichokifanya halafu leo uje kulialia eti rais anachochea mgawanyiko ni upuuzi.
 
Hayo maneno ya magufuli hayakuwa maneno ya busara na hekima kama kiongozi wa nchi. Huyu mtu anahitaji kuthibitiwa.
 
Rais kasema "Kama mtu anakataa mkono wako nawe kataa mkono wake kwa mambo yake, nikuombe nawe uwe unamkatalia mkono wako kufanye mambo yake' Anamuomba Mungu kumpa walau robo ya moyo wa Shein lakini naye ambae walau robo ya mawazo yake."

Wacha kupotosha watu
Malipo ya viongozi wastaafu yapp kwenye katiba na hawana namna ya kuyazuia
 
Baadhi ya wanajamii forum mnashangaza et JPM kumwambia Shein asisaini posho za SEIF anajenga chuki lkn SEIF kuukataa mkono wa Shein sio kujenga chuki.
kupewa mkono ni jambo la binafsi kusaini posho ni jambo la kisheria,kutompa mkono, seif hajavunja sheria lakini kutosaini posho atakua kavunja sheria,swali anaevunja na asievunja nani anahatarisha amani
 
Huku Wachambuzi na Political scientists wanaita kwa Mara ya Kwanza " TANZANIA IMEPATWA KWA IKULU* ** Kuna kitabu kimoja kinaitwa Natafsiri " GHARAMA ZA CHUKI NI KUBWA KULIKO ZA UPENDO" Chuki hufubaza Thinking and Reasoning capacity.....Kuna Mengi ya kuandika lakini NANI WA KUMFUNGA PAKA KENGERE?
 
Hiyo sheria ya Seif kulipwa posho iko kwenye bible au Qur'an?

Si inatenguliwa tu anakula jeuri yake au inasainiwa kila baada ya miezi saba.

Mi nakerwa na unafiki tu,kumpongeza Seif kwa kile alichokifanya halafu leo uje kulialia eti rais anachochea mgawanyiko ni upuuzi.
Bwana Mdogo sheria haifanyi kazi kinyumenyume

Ikatungwa sheria Leo Haiwezi kuhukumu ya JANA.

SHULE SHULE SHULE
 
Baadhi ya wanajamii forum mnashangaza et JPM kumwambia Shein asisaini posho za SEIF anajenga chuki lkn SEIF kuukataa mkono wa Shein sio kujenga chuki.
Aisee hata mimi nimeshangaa sana[emoji15] [emoji23]
 
Back
Top Bottom