Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Sheria inamtaka kusaini
Hujajib swali,anasaini kama nani kwa Maalim wakati Maalim hamtambui Shein na serikali yake kwa tafsir ya Maalim Znz hakuna Rais na ndio maana nasema unafiki ni mmbaya sana na mtu mnafiki ni muuaji,JPM kwa hilo namuunga mkono hakuna sababu ya Shein kusaini makaratas ya Maalim ukizingatia Maalim hamtambui!
 
Ngoma ndo kwanza linaanza tutashuhudia mengi kipindi cha miaka kumi
 
Sasa wewe kwa akili yako hiyo nusu ulojaaliwa rais anawaunganisha au anawatenganisha wazanzibari? Ndiyo maana Nabii Suleiman as alimuaomba Mwenyezi Mungu Hekma.
Sefu alivyokataa mkono alikuwa anawaunganisha wazanzibari?..
Sefu sijui amewapa nini nyie watu,hongera magufuli sasa unaongea lugha wanayoitaka cuf
 
Kweli kabisa mkuu. Huyu mtu kila akiongea ni visasi na hasira tu. Sijui ni baba wa aina gani. Sijui amelelewa katika mazingira gani? Sijui kweli kama ana imani ya dini yoyote kwasababu dini zote huhubiri upendo, amani, msamaha na mshikamano. Huyu anahubiri visasi, utengano, vitisho, na mabavu! Tulifikaje hapa?!
Hujaona visasi vya Waemba wa cuf kuwanyanyasa ccm huko Pemba !?? mpaka wanawekewa vikwazo vya uchumi ? useless wapemba cuf !
 
Hii video imenionyesha wazi huyu mtu ni wa aina gani. IQ ni ya mtu wa kawaida kabisa, definitely not presidential material.

Aliyesema maendeleo hayachagui chama leo anasema hawezi weka mtu hata moja wa chama kingine kwenye serikali yake, na anavyoitamka kibabe, duh.

Alafu hilo swala la Dr Shein kutokupewa mkono ni uamuzi wa mwenzake, ila kumtaka Dr Shein asifanye kazi yake kisa hakupewa mkono ni ujinga wa hali ya juu, kazi ni kazi tu, kua kiongozi haimaanishi watu ulio na ugomvi nao uwanyime haki zao, unalipwa ufanye kazi yako, emotions zako lazima zikae pembeni.

Huyu mtu ana moyo wa kulipiza kisasi sijawahi pata kuona, ni kosa kubwa sana, hata kura yangu nilimpa, tena nikachoma nauli kupanda ndege hadi bongo, biggest mistake of my life.

Kwa mtu mwenye fikra za namna hii hamtoenda popote, subirini miaka 5 ijayo mtashuhudia, sasa hivi mwenye direction kidogo labda waziri mkuu, na waziri wa ardhi, wengine wote fikra kama za muheshimiwa huyu. Wameconcentrate kushindana na maadui zao badala ya kuweka akili kwenye maendeleo. Nimeamini mwafrika ni mwafrika tu, tena ambaye hana exposure na nchi za nje kama huyu ndiyo kabisaaa, ondoa hope zote.
 
Hujajib swali,anasaini kama nani kwa Maalim wakati Maalim hamtambui Shein na serikali yake kwa tafsir ya Maalim Znz hakuna Rais na ndio maana nasema unafiki ni mmbaya sana na mtu mnafiki ni muuaji,JPM kwa hilo namuunga mkono hakuna sababu ya Shein kusaini makaratas ya Maalim ukizingatia Maalim hamtambui!
Mungu atusaidie sana! Hivi kwanini tumechagua kumpotosha rais wetu mpendwa? Wewe unang'ang'ania Seif hamtambui Shein kama hoja ya kutosaini, serious? Suala hili ni la kisheria na kikatiba, Seif asipomtambua Shein urais wake unakoma? Hebu tuache kujitoa akili kwenye masuala nyeti kwa mustakabali wa taifa letu tafadhali!
 
Kweli kabisa mkuu. Huyu mtu kila akiongea ni visasi na hasira tu. Sijui ni baba wa aina gani. Sijui amelelewa katika mazingira gani? Sijui kweli kama ana imani ya dini yoyote kwasababu dini zote huhubiri upendo, amani, msamaha na mshikamano. Huyu anahubiri visasi, utengano, vitisho, na mabavu! Tulifikaje hapa?!
Inasikitisha kwamba tumevuruga na kusigina katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado hatujaona imetosha tumeamua kuwafuata na wazanzibar ambao taratibu maumivu waliyoyapata uchaguzi wa mwaka jana yalikuwa yameanza kupoa, tunawachochea tena kuzidi kuhasimiana huku tukiwashauri wasigine kwa mara nyingine tena katiba yao! Mungu atusaidie sana!
 
Kuna tabia mbovu sana ya kuchimbana ambayo JPM kashindwa kuivumilia, namaanisha kwa ndugu zetu wa visiwani.
Kuishi kwa kusimangana, kunyanyasana kihisia, na Dr wa upande wa pili wa muungano, ni mpole na mvumilivu sana.
Sio wanasiasa wengi duniani wenye uwezo mkubwa wa uvumilivu. Maishani inafika kipindi mtu unakubaliana na hali halisi, kwamba sio kila ukitakacho kitafanikiwa kutokea.
Na ajikwezaye hudhalilishwa.
 
Nimeikopi mahali:

Anaandika Rashid Chilumba mwanachama mtiifu wa CCM.

Matamshi aliyoyatoa Ndugu Rais leo hapa Unguja sikuyatarajia yatoke kwenye kinywa cha mkuu wa nchi, Haya yanamwagia mafuta kwenye moto.

Suala kama la pensheni au matibabu ya mtu aliyewahi kuwa Kiongozi ni la kisheria siyo hiyari ya mtu, Yaan hata umfumanie na mkeo Sheria inakutaka usaini na apewe. Mengine mmalizane wenyewe.

Na kwa kuwa Tumesema siasa zimeisha Basi tujitahidi kuzimaliza kweli, sare za vyama, vijembe na maneno ya ngebe kwenye mikutano ya serikali inawagawa raia.

Siku zijazo wasio wana CCM wanaweza kuacha kuhudhuria mikutano ya Kiongozi mkuu wa nchi kwa sababu wanajihisi wanyonge na wakiwa.

Tuzungumze Maendeleo, kufanya kazi na kubadili maisha yetu, hawa Wakosoaji na wapinzani watakuwepo daima, kuwashambulia katika jukwaa lililolipiwa kodi na watu wote ikiwemo wao si jambo la kiungwana.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Hotuba za Ndugu Rais katika ziara yake visiwani hazijanivutia wala kusisimua. Zimeiacha Zanzibar katika mtafaruku ule ule au mkubwa zaidi.
 
hizo pesa anazosaini Shein ni zake au ni kodi zetu? Hayo mambo ya kupeana mikono yako kwenye sheria gani? mnataka kutumia ofisi za umma kwa mahaba yenu?
Hahahah kumbe una support uchocheaji wa uhasama kama alioufanya Seif sio. Amefanya vizuri sana sana. Daaaa. Basi sawa. Akisema mwingine linakuwa kosa. Utaratibu kwa kisheria hauwezi pingwa kwa sababu upo. Ila Magufuli anajaribu kuonyesha dhamira ya moyo kama binadamu, kama unadharauriwa basi ujue autimatically hata ungekuwa wewe response yako ingekuwa negative. Huo ni katika ubinadam. Anyway. Tumsamehe Seif kwa sababu asingefanya vile basi matamshi kama haya tusingeyasikia
 
Back
Top Bottom