Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nafikiri hupo sahihi, laweza kuja tokea tena hapa Africa, kama si kwetu.Naanza kumkumbuka marehemu Chiluba jinsi alivyoingia madarakani na kudharau waliomtangulia kama Mzee Kaunda. Kilichotokea ni kuwa baada ya yeye kuondoka madarakani aliyoyafanya kwa mwenzie yakajirudi kwake na alikaa sana "Segerea" ya Zambia na hakuna aliyemuunga mkono tena akajihisi upweke sana na ndio uliochangia safari yake ya peponi au jehanamu mapema. Madaraka ni dhamana unayoipata miongoni mwa wengi sio ujanja wako, hebu muoneni JK jinsi alivyoishi kwa kauli za hekima kiasi kuwa hata kama kamuumiza mtu bado unamuona binadamu.
Huyu ana nia mbaya na kuwachonganisha Wazanzibar tu, kauli zake zote ni za ovyo kwa wazanzibar sio za kuunganisha ni za kuwagawa ili aendelee kuwatawala.
Akiwa Pemba aliwambia haoni haja ya wao mke na mume kununiana kisa siasa na wajiepushe na mambo ambayo yalitokea Libya leo anaongea kinyume na kuikana kauli ya jana ya kuwaasa watu wawe na umoja na mshikamano.Hakuna kitu kama hicho ni sawa na kusubiri meli ubungo!!
Huo ndio ukweli Seif ilibidi afunzwe adabu.Jamani huyu mtu akiachiwa atazidi kuivuruga nchi, ana matatizo makubwa
Maskini Magu afadhali asingekuwa Rais ameharibu kila kitu!! tumemwona katika udhaifu wote. JK welcome back awamu ya tatu yakoNimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshauri Rais wa Zanzibar kuwa kwasababu Shein ndiye anayesaini stahiki za yule aliyemkatalia kumpa mkono siku ya mazishi ya mzee Jumbe basi Shein naye asisaini tena stahiki za huyo mtu.
Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?
Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.
Tunakokwenda ujinga hautavumiliwaTunakokwwnda sijui itakuwaje??!
mnafiki tu!Akiwa Pemba aliwambia haoni haja ya wao mke na mume kununiana kisa siasa na wajiepushe na mambo ambayo yalitokea Libya leo anaongea kinyume na kuikana kauli ya jana ya kuwaasa watu wawe na umoja na mshikamano.
Ninapatwa na mashaka mengi kuwa pengine kuna wakati bob anakuwa sio yeye yaani akili yake inapata intruders. .na hili linasemwasemwaNimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshauri Rais wa Zanzibar kuwa kwasababu Shein ndiye anayesaini stahiki za yule aliyemkatalia kumpa mkono siku ya mazishi ya mzee Jumbe basi Shein naye asisaini tena stahiki za huyo mtu.
Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?
Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.