Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

ukweli ni kwamba maalimu seif hakutaka unafki hata wasipo saini haki zaki itakuwa ni muendelezo wa zulma tu ila katika dini zote mbili zulma ni thambi kubwa sana fikiria we hapo ulipo aliyekuzulumu utampa hata salamu yako?
 
Yule Aliyekuwa Mpaka Leo Hajaamini Kama CCM wana Akili Ndogo (Narrow Minded) Kuliko Hata Kuku Basi Mkutano Wa Leo Unguja na Uzi Huu Unatosha Kumjuilisha Hilo!!!

Kuhusu Rais Shein Kusaini Kwa Ajili Ya Kumpatia Hela Za Kusafiri Nje Ya Nchi, Pamoja Na Matibabu
Muheshimiwa Magufuli Kalizungumza Hili Pale Alipowasoma Wale Hadhira (CCM) kuwa Akili Zao Ni Finyu Kiasi Ya Kwamba Ni Brainwashed na Ni Remote Controlled Kiasi Ya Kwamba Watashindwa Kujiuliza Anasaini Kwa Sheria/Katiba ipi??

Ni Kweli Maalim Seif Alikuwa Ni Waziri Kiongozi, Na Baadae Akawa Makamo Wa Rais!
Kipindi Hicho Cha UwaziriKiongozi/UmakamoRaisi ni Kweli Alikuwa Akisafiri Kwa Kutumia Fedha Ya Serikali Kwa Ziara Zote Za Kiserikali Kwasababu Katiba inamruhusu Kufanya Hivyo.

Lakini Baada Ya Kuachana Na Nyadhifa Zote Hizo Basi Hasafiri Kwa Ziara Za Kiserikali, Bali Anasafiri Kwa Safari Zake Binafsi au Ziara Za Kichama!
Na Safari Hizo Zote Anatumia Pesa/Nauli Yake na Wala Si Kutoka Kwa Shein!

Mheshimiwa Magufuli Usiwachezee Watu Akili Kiasi Hicho Ya Kuwa Shein Atowe Pesa Za Serikali Ampe Seif Akazitembelee Ughaibuni.

Yeye Akiwa Ni Kama Makamo Wa Rais Mstaafu Atakuwa Anazohuduma Zilizoainishwa Kwenye Sheria Ni Lazima Azipate Kutoka Serikalini! Lakini Swala La Kusafiri na Kutibiwa Nje Ya Nchi Hilo Maalim Seif Haitegemei Serikali Kifedha Bali Ni yeye Mwenyewe Anaouwezo Wa Kujifadhili.

Labda ingefanana ungelisima Wewe Muheshimiwa Magufuli na Mheshimiwa Shein Mushirikiane Na Balozi Za Nchi Mbali mbali ili Anyimwe Viza Za Kusafiria Kama itawezekana! Na hilo Ndiyo lililo kwenye uwezo wenu.
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshauri Rais wa Zanzibar kuwa kwasababu Shein ndiye anayesaini stahiki za yule aliyemkatalia kumpa mkono siku ya mazishi ya mzee Jumbe basi Shein naye asisaini tena stahiki za huyo mtu.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.



!
!
kila mtu huwa na busara kabla hajaongea chochote kile. Nilijua tu atatoa boko ila boko gani ndio nilikuwa sijui.
 
Mkuu anaamini dawa ya bishoo ni kuwa bishoo zaidi yake.

Katiba kitu gani bhana?

Baraza lote la wawakilishi ni CCM si vifungu vinabadilishwa tu analishwa jeuri yake.

Hizi ndizo siasa za Africa mwenye madaraka ndiyo Alfa na Omega hata kwenye vyama vya upinzani tumeona watu wakiabudiwa kisa Chairmen.

Hakuna jipya.

Kamuulizeni Prof Safari kama alipata stahiki zake alipofukuzwa kazi Chuo cha diplomasia.

Kikwete akiwa Waziri wa Foreign affairs aligoma kukiondolea kinga ya kibalozi ili Safari akiburuze Chuo mahakamani.(as per Mwanahalisi though I am not sure if this is a credible source)

Malcolm X aliwahi kusema kwamba kitabu anachokiamini yeye hakina kitu kama turning the other cheek so ukimgusa bega anakupeleka makaburini.
 
Rais Magufuli anajitia tu aibu ktk ziara hii ya ZNZ
Wala alikua hajui nn akawaambie wakazi wa Unguja na Pemba
Lolote linalokuja yy anaongea
 
Naanza kumkumbuka marehemu Chiluba jinsi alivyoingia madarakani na kudharau waliomtangulia kama Mzee Kaunda. Kilichotokea ni kuwa baada ya yeye kuondoka madarakani aliyoyafanya kwa mwenzie yakajirudi kwake na alikaa sana "Segerea" ya Zambia na hakuna aliyemuunga mkono tena akajihisi upweke sana na ndio uliochangia safari yake ya peponi au jehanamu mapema. Madaraka ni dhamana unayoipata miongoni mwa wengi sio ujanja wako, hebu muoneni JK jinsi alivyoishi kwa kauli za hekima kiasi kuwa hata kama kamuumiza mtu bado unamuona binadamu.
Mswahili sasa yupo huru na wakati wowote unaweza kumuona mitaa ya ilala anakunywa kahawa bila ulinzi
 
kuna sheria inasema ni lazima mpeane mikono? lakini hicho anachokisaini kiko kwenye sheria. mkiambiwa mkuu anatumia mamlaka yake kwa utashi wake na sio sheria isemavyo mnakataa. hapa ndio tabia ya mkulu inapoonyesha kwake sheeia sio kitu muhimu sana bali ni kile akipendacho yeye ndio sheria.
kuna sheria inasema ni lazima mpeane mikono? lakini hicho anachokisaini kiko kwenye sheria. mkiambiwa mkuu anatumia mamlaka yake kwa utashi wake na sio sheria isemavyo mnakataa. hapa ndio tabia ya mkulu inapoonyesha kwake sheeia sio kitu muhimu sana bali ni kile akipendacho yeye ndio sheria.
utamfanya nini rais ukiweka pending makaratasi yako?
 
Back
Top Bottom