Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

wacha uwongo huo.. mara ya mwisho alipoenda matibabu india Serikali ndiyo iliyolipa gharama zote.. Naona una goldfish memory.. kwani hiyo habari ilienea kila sehemu.. tafuta chengine cha kudanganya
 
Sasa wewe hapa umeleta kitu gani tena mbona hatukuelewi!
 
Kauli kama hizi ndio kauli za kichochezi,mambo ya zanzibar ni heri angetuachia wenyewe wazanzibari kama alivonukiliwa akisema huko nyuma kuwa mambo ya zanzibar hayamuhusu,
kauli hizi zina maana ya kuendelea kupigilia misumari mgawanyiko wa wazanzibari ili kuendelea kuitawala zanzibar "devide and rule"
raisi anasimamisha siasa za upinzani ili kujenga nchi na kauli mbiu ya "hapa kazi tu",sasa hizi siasa za vijembe na kufurahisha wanaosikiliza kwenye mikutano ya hadhara zitajenga nchi kweli
 
Tatizo ni kwamba akifanya mambo haya, ipo siku wataingia madarakani watu wasisaini naye stahiki zake wakati yeye keshastaafu.

What goes around comes around!
 
Huku tunakoenda sasa siko aisee,
Yaani mtu akikataa kukupa mkono wewe unambania stahiki zake ambazo ziko kikatiba kisa una madaraka??
Kwani huo mkono nao uko kikatiba mpaka ulipize kwa kumnyima mafao yaliyoko kiikatiba??
Anawafundisha nini walioko chini yake??

Mpaka 2020 tutakua tumeona na kusikia mengi sana aisee
 
Alikuwa anatania tu. Nakumbuka alivyotania tufyatue
 
Huyu mtu kuna wakati itafika ataamrisha mishahara na vyeo viwe vinapanishwa kwa kuzingatia itikadi za kisiasa
 
Uongozi wa visasi kamwe hauwezi kutibu majeraha ya umaskini tuliyonayo Tanzania.
 
kuongoza ni kazi ngumu sana ndiyo maana mzee jakaya alipoingia madarakani alianza kuota Mvi Mapema.
 
Huyu ana nia mbaya na kuwachonganisha Wazanzibar tu, kauli zake zote ni za ovyo kwa wazanzibar sio za kuunganisha ni za kuwagawa ili aendelee kuwatawala.
Kwako seif anania nzuri ya kuunganisha wazambari
 
ndio maana hajaenda mbeya hawakumpa mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…