Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Hata mimi nisinge saini.

No hu sign kwakua unampenda au kumchukia, una sign kwakua ni haki yake kikatiba na kwakua hajavunja sheria basi swala la kukataa mkono nikuonyesha kutoridhika kwake, ilibidi asikilizwe na baada ya kusikiliza then ndipo uangalie kama kuna kosa au la na kama kuna kosa basi vyombo vya kusimamia haki vipo... Kuna mambo ya msingi ya kuzingatia, kusimamia haki hata kama inamhusu mtu ambaye hakupendezi wewe binafsi.
 
Watu wanafiki sana tena haswaa hawa wajiitao wapinga kila litendwalo na uongozi was serikali ya awamu ya tano,hv rais kakosea kitu gani? Je,ilikuwa ni busara kwa seif kuukataa mkono wa rais mbele za watu na alikuwa anatoa picha gani kwa kadamnasi? Alifanya udhalikishaji na hyo ni kutokana na dhana yake kuwa hataki kukubali kuwa shein ndiye rais wa znzbar,sasa Leo hii na mijidevu yake kama kiota cha mwanchoko anapeleka fomu zake zisainiwe na MTU asiyemsadiki kuwa rais wake that is totally foolish upon him,next time ajifunze kiburi sio maunguana na nyie nyumbu sio kila jambo mnalisimamia vidole ikiwa hata halina tija acheni uzwazwa

Sasa Nikuulize Swali Wewe Unaejifanya Unaakili Nyingi??

Hivi Ikitokea Mkoa mmoja Hapa Tanzania Chama Tawala Kisipate Hata Jimbo Moja, Je Wasipeleke Maendeleo Katika Mkoa Huo Kwa Sababu Hawakuchaguliwa??? Jibu lolote utakalojibu ni Kwanini??

Mkuu Mambo Mengine Hayataki Akili Kubwa! ni akili ya Kawaida tu inatosha Kuyafikiria!!

Maalim Seif Ni Makamo Wa Rais Mstaafu!! Kwahiyo Kuhudumiwa Kama Makamo Wa Rais Mstaafu Lipo Kwenye Katiba Ya Nchi,, Hafanyiwi Huduma Kwakuwa Anaonewa Huruma na Shein! Hapana! Bali Ni sheria Ndiyo inaelekeza Hivyo..
Sasa Shein Hawezi Kuvunja Katiba Kwa Makamo Mstaafu Kwa Utashi Wa Kisiasa.

Lakini Kitendo Cha Maalim Seif Kuto Kumpa Mkono Shein! Haikuandikwa Kwenye Katiba Kuwa Mkono Wa Shein Lazima Upokelewe.

Hebu Nyinyi CCM kajifunzeni Sheria Coz Mumekuwa Brainwashed Wa Kutupwa...
 
Hakuna sheria inayolazimisha viongozi kushikana mikono.

Haki za Seif zipo na zinalindwa kisheria. Kitendo cha kusema makaratasi yasisainiwe kwasababu amekataa kutoa mkono, ni jambo la hatari sana

Haki za watu zinalindwa kikatiba, kama kuna haja sheria zifutwe kwa utaratibu uliopo

Nimesikiliza hotuba za Rais ZNZ kwa mtazamo wangu naona zimeongeza ufa badala ya kuponya

Zimeacha ZNZ kwa makovu makubwa sana na hali itakuwa tatizo kubwa sana

ZNZ imegawanyika kwa kiwango kikubwa, haiwezekani kukawa na kejeli, dharau kisha watu kudhani kuna kuponya tatizo!
 
Kwa fikra za mkuu wa nchi ni dhahiri uchaguzi haujaisha.Nlitarajia ahubiri umoja na namna Bora ya kutekeleza ilani ya CCM huku akiomba uungwaji mkono.Ila hii ya kulipa visasi.Tunasafari ndefu tuendako.
Raisi anapaswa kushauriwa vyema.
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

Kama ilivyo haki yake kikatiba Seif kupata stahiki zake pia ni haki kikatiba seif kumpatia heshima rais wa nchi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Yeye aliyekataa shughuli za Siasa,na aliyekataa mkono wa kinafiki nani wa kunyooshewa kidole?
 
Hakuna sheria inayolazimisha viongozi kushikana mikono.

Haki za Seif zipo na zinalindwa kisheria. Kitendo cha kusema makaratasi yasisainiwe kwasababu amekataa kutoa mkono, ni jambo la hatari sana

Haki za watu zinalindwa kikatiba, kama kuna haja sheria zifutwe kwa utaratibu uliopo

Nimesikiliza hotuba za Rais ZNZ kwa mtazamo wangu naona zimeongeza ufa badala ya kuponya

Zimeacha ZNZ kwa makovu makubwa sana na hali itakuwa tatizo kubwa sana

ZNZ imegawanyika kwa kiwango kikubwa, haiwezekani kukawa na kejeli, dharau kisha watu kudhani kuna kuponya tatizo!
Kama katika katiba inasema kila raia wa wa Tanzania analazimika kusimama bendera ya nchi inapopandishwa iweje kwa Rais kutopewa heshima yake na kudharauliwa kiasi cha seif kutokumpa mkono mbele za watu na jioni kwenda kudai pesa za matibabu
 
Watu wanafiki sana tena haswaa hawa wajiitao wapinga kila litendwalo na uongozi was serikali ya awamu ya tano,hv rais kakosea kitu gani? Je,ilikuwa ni busara kwa seif kuukataa mkono wa rais mbele za watu na alikuwa anatoa picha gani kwa kadamnasi? Alifanya udhalikishaji na hyo ni kutokana na dhana yake kuwa hataki kukubali kuwa shein ndiye rais wa znzbar,sasa Leo hii na mijidevu yake kama kiota cha mwanchoko anapeleka fomu zake zisainiwe na MTU asiyemsadiki kuwa rais wake that is totally foolish upon him,next time ajifunze kiburi sio maunguana na nyie nyumbu sio kila jambo mnalisimamia vidole ikiwa hata halina tija acheni uzwazwa
Kwahiyo kwako busara ni kurudia uchaguzi?
 
Nyie mnaochangia kushangaa kauli za magufuli ni wachanga katika kisima cha busara, huwezi kuelewa maono yenye sura ya kitaifa. Kuna vitendo na kauli zingne huelekezwa kwa fulan lakn athar zake zinawagusa maelfu ya watu ukiwemo wew. Kuna watu akili zao huishia kuona kipimo chao pekee namba ikizidi hupotea relini hukosa ajenda ndo utasikia ooh ni matakwa ya sheria! alafu sheria hiyo ikiwabana mnageuza oh! Katiba hii ni dhaifu, mkiona upenyo wa kisheria kumuonea mtu mnautumia, mkidhibitiwa utasikia oh! Inavunjwa katiba! Dikteta huyo!. Katiba sio msahafu penye udhaifu hekima ya kiongoz lazima ipazibe, kuilinda katiba ni pamoja na kutetea madhaifu yake sio kuachilia.
 
Kama katika katiba inasema kila raia wa wa Tanzania analazimika kusimama bendera ya nchi inapopandishwa iweje kwa Rais kutopewa heshima yake na kudharauliwa kiasi cha seif kutokumpa mkono mbele za watu na jioni kwenda kudai pesa za matibabu
Sawam tupe sheria hiyo inayosema ni wajibu wa Rais kupewa mkono?

Pili, kuna uhusiano gani wa mikono ya watu wawili na uendeshaji wa nchi?

Tatu, haki za Seif zipo kwa ridhaa ya mtu au zipo kisheria?
 
Ivi Magu alienda kuwaunganisha Wazanzibari kweli ?

RAIS: hakuna mpinzani atatia mguu katika serikali yangu..
(sio kauli ya kibaguzi? lakini kwani Mrema vepe ?au kamsahau ?)

RAIS: huyo aliekataa kisima chake kutumiwa na watu wa chama fulani, mngemtumbukiza kisimani..

Na je aliekataa wapinzani kuingia kwenye serikali yake ?

RAIS: huwezi kukataa mkono wangu halafu nisaini stahiki zako..

Na je waliomzomea Mbeya, ndio atawatenga ?
 
Kosa lishatendeka, twashuhudia madhara yake sasa. Kwa akili hii ya mkuu wa nchi , tutateseka sana.
 
Labda waziri wa sheria atoka na tamko kwamba raisi hakumaanisha alikua anatania
 
Hata yeye hajui kuwa sio vyote vizuri anavyovifanya vinatumiwa na wanaompenda tu?
Hata mahasimu wake wanavitumia. Hata Mungu huwanyesha Mvua na wale wa shetani wavune japo watayatumia mavuno hayo kushukuru shetani kuwa kawabariki. !!
 
Ndio ana waunganisha wa Zanzibari hivyo. Hizi hotuba zake zinanikumbusha enzi za Mzee Kenyatta wanafunzi walikuwa wanajaa Tv room kusubiri Mzee atatoka na lipi.
 
Sawam tupe sheria hiyo inayosema ni wajibu wa Rais kupewa mkono?

Pili, kuna uhusiano gani wa mikono ya watu wawili na uendeshaji wa nchi?

Tatu, haki za Seif zipo kwa ridhaa ya mtu au zipo kisheria?
Kauli zako zinaonekana zina harufu ya utovu wa maadili, hivyo judgement zako zina msukumo wa utukutu tu sio tafakar ya hekima. Kaa pemben
 
Back
Top Bottom