Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Maskini Magu afadhali asingekuwa Rais ameharibu kila kitu!! tumemwona katika udhaifu wote. JK welcome back awamu ya tatu yako

Nyie mna matatizo sana. Yaani Maalim Seif afanye ujinga kisha aachwe tu kwa vile ana haki ya kupokea mafao?
 
ila haimlazimishi ! ......maana hakuna adhabu ikiacha
Wewe ukiajiriwa huwezi kusema hulazimiki kufanya kazi. Kumtaka ndio lazima yenyewe kwani ndiyo kazi yake anayolipwa kwayo. Rais anafanya kazi kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu sio kwamba anafanya jinsi anavyotaka yeye. Akifanya kwa jinsi anavyotaka yeye ndio utaona matokeo kama ya sinto fahamu ya hivi karibuni ya maandamano na mikutano ya siasa.
 
Wewe utakuwa ni mwanaLUMUMBA.
Hahahaa. ungejua. Ni mpinzani ambaye nimebadilika fikra! Zenye mashiko na uzalendo kwa nchi yangu. Tunashuhudia kabisa upinzani wa kweli ni ule uliokuwepo wakati wa Dr Slaa na Prof Lipumba. Na ndio maana wanaonekana ni hatari kwa maslahi ya baadhi yao wakaamua kutafuta mbinu za kuwapiga chini. Uliobaki sasa sio upinzani ni upingaji tu. Wengi wao ni wasaka tonge tu. Eti mtu bila tafakuri yoyote unaamua kubadilishia gia angani na kupiga chini ajenda ya ufisadi hivihivi. Kisa eti tumemsafisha. Yuleyule ambaye tulikuwa tukimwita fisadi kwa zaidi ya miaka nane wajameni. Hatutasahau kamwe tendo hili katika historia ya nchi yetu. Na tutawarithisha vizazi vijavyo matendo haya makuu ya ukosefu wa maadili yaliyotokea
 
Anonymous x
I can guess. Huyo jamaa aliyechoma nauli ya ndege kuja kumpigia kura mkubwa lakini sasa anajuta. Ila amefunguka vizuri tu kwa uwazi kwakuwa hata mkubwa mwenyewe si huwa anasema nasema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu
 
Wazo zuri sana hili.

Ile picha ya Seif akikataa kuupokea mkono Wa Shein inabidi tuitengenezee T-shirts na kuzivaa kwa wingi ili kuendelea kumkera mkuu.
Angalau tupate na sisi kitu cha kumkera.
 
Hajui kuchuja maneno...hana maono wala dira..kwake linalomwijia kichwan anaropoka..hili ni tatizo kubwa na kwa mtindo huu wa kauli za kibabe wala hawezi kulisogeza taifa mbele..leo ukweli unaanza kujidhihili...uchumi wa nchi uko hovyo sana..lakin yy bado ni majigambo ..

Hotuba zake huwezi kuzifanyia marejeo zimejaa ubinafsi..mimi ndio rais..mimi ndio rais..huku akitafuta umaarufu kwa watanzania wajinga wanaomshukuru kwa kuliwezesha tukio la kupatwa kwa jua kutokea nchini...

Si kila msitu ni kwa ajili ya kila nyani..hata nafasi ya urais si kwa kila mtu wa aina yake..ajifunze kuliunganisha taifa na sio kuligawa..asifikir yeye ana akili sana kuliko watanzania wengine..zile pushups na kupita juu ya roof ya gari vinasadifu aina ya mtu tulie nae..

Kwa bahati mbaya hata waziri mkuu nae kawa kimya na kwa hali ilivyo inaonekana ni mtu wa kuburuzwa asiyeweza mshauri rais ipasavyo..yupo yupo tu anahangaika..
Ziara yake zanzibar imetia chumvi kwenye kidonda...mambo ya ajabu sana..
Very sad bro..
Fuatilia taarifa ya kamati ya bunge ..ilivofanya ziara jana bandari ya daslaam....utagundua tu hata mapato tunayoaambiwa ni hewa kila mwezi huwenda ni hewa
 
I can guess. Huyo jamaa aliyechoma nauli ya ndege kuja kumpigia kura mkubwa lakini sasa anajuta. Ila amefunguka vizuri tu kwa uwazi kwakuwa hata mkubwa mwenyewe si huwa anasema nasema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu
Hahahahahah,yaani mtu ukichoka bwn unaweza fanya lolote eti
 
Tatizo Rais anaongeaga mambo bila kutafakari,hiyo sio hiyari yake!Ni takwa la kikatiba!Hutasaini ataenda mahakamani na mahakama itaamuru apewe stahiki zake,au utaigomea na mahakama pia?Huu ukurupukaji na matamko ya mwendokasi kufurahisha halaiki hayana msingi na yanamtia aibu Rais!Rais anaongea watu tunaoelewa tunainamisha vichwa chini kwa aibu!
vipi hua haulambi lambi na lips? kukata kata vi jani je? wanaume wengine bwana!!
 
Hivi huwa anapata muda wa kutafakari matamko yake? Au bora liende!!

Sidhani. Mimi Binafsi niliposikia ile kauli ya Malaika nao wanatakiwa waishi kama wale walioandikwa kwenye kitabu cha Salman Rushdie!!!!, mpaka muda ule nilikuwa bado napiga Ngoma nikichanganya na Manyanga ya kumshangilia Mzee.
Lakini niliposikia kauli ile tu kutoka kwenye kinywa chake, Nyanga nikaweka chini, Ngoma nikatoboa zote, Marimba nikavunja vunja, na Moto wa kupashia Ngoma nikazima, nikawaacha wasaidizi wangu wakinishangaa.
Mimi huyooo huku nikisikia kizungu zungu cha tamko nikaenda kulala.
Hivi sasa sipati tabu, nimekaa chini ya mti na 277 yangu ya urithi tu kusikiliza matamko.
Akisema " hatotoa mkono mimi sawa, akisema Mwangaruka mimi mswano tu, akisema Ulimola mimi Kwangu tawile, mradi nasikiliza matamko.
Lakini Ngoma, Manyanga, Marimba, na vifaa vingine vyote ambavyo vilikuwa vinanifanya nimshangilie nimevunjilia mbali.
 
Naona mnapata sana shida kila kukicha Rais Rais Rais, kama mnaona hawafai si mhame nchi tu, nendeni nchi mtakazo kama Sudan Kusini, Libya, Syria, Zimbabwe, Uganda nk ili povu lisiendelew kuwatoka kila kukicha. Rais anafanya kazi na ndo kwanza hata mwaka haujaisha, ss nawaonea huruma mana mpaka mitano iishe halafu tumwongezee mingine mitano, mate yatakuwa yamewaisha mdogo kwa kuchonga kelele msizozijua. Hiv mlitaka rais awe nani ss????? Rais ni mmoja tu na ndo anaetambulika rasmi na dunia wengine mliosalia makap......
 
haaaaaaaaaa kwan yy ndo anaamua nan apate posho au n sheria????
 
Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu
Tulipoficha mundu za kupondea wezi
Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya?
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne
Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango
Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni
Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako
Wanashangaa mbona ghafla
Samahani sana mgeni
Wapishi wameniomba kwamba
Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba
Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje
Sizonje chumba hiki naomba usiingie
Ukimaliza nitakwambia kwanini
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa
Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa
“USIYEMTAKA KAJA”
Hatukuwahi kuelewa maana yake
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia
 
Back
Top Bottom