Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

To him,
“You do not respond to a mosquito bite with a hammer." by Prof Lumumba
 
Huyu ndiye Rais muafaka kwa wakati muafaka na kwa kuirudisha nchi kwenye line. Mtanyooka tu hiyo bembeleza bembeleza ndoo imeifikisha nchi mahali hapa.
Unaweza jikuta ww ndie umenyooka, wenzio wako vile vile!!!
 
Seif yupo sahihi maana alipokonywa ushindi wake halali wa Uraisi kwaiyo inakuwa inafiki kumpa mkon mtu ambaye ujamsamehe
Hata kama ila ikumbukwe kwambwa wahenga husema muugwana havimbi mashavu. Kilichokusudiwa ktk msemo huo ni kwamba kukasilika ni moyoni na, sio kila mtu afahamu hasira zako
 
Mmmh kwa hizo kauli za rais ya jamhuri yetu ni dhahiri kuna visasi na uhasama, lakin ukiwa kiongozi ambaye chini yako kuna watu hutakiwi kua na vinyongo na jaziba kwani hutatoa hukumu za haki, raisi ni ngazi ya mwisho ambapo mtu anaweza kupeleka malalamiko yake anapohisi hajatendewa haki na vyombo vya kutoa haki, sasa raisi akiwa ndo wakwanza kutoa hukumu za namna hiyo je, atakaeonewa na vyombo vya kutoa haki utaenda wapi kupeleka malalamiko yake?? Ni dhahiri atakuwa ameonewa maxima.
 
Sawa na wewe unaona sawa sheria zivunjwe kirejareja hovyo!! Kwani Magu hana namna nyingine ya kushughulikia migogoro badala ya kutoka povu kama siye?!! Inamuharibia huo siyo urais

Sasa yeye Maalim Seif kwa nini alifanya kibri mbele dhidi ya mamlaka halali?
 
Mi nadhani kuna makosa makubwa sana ya kiuongozi, nimesikia mpaka nimeogopa. Tuombe Mungu tuvuke salama
 
Nakwambia wewe mzee una huruma ingekuwa mimi hihihiiii
 
Katika imani ya dini ya kiislam imekatazwa kabisa kulipiza ubaya kwa ubaya, Ni dhambi kulipiza kisasi kwa mtu ambaye unahisi kua hajakutendea jema.Katika kitabu kitukufu cha Quran inatamkwa kua ni mwiko kabisa kulipa kusasi.Sijui vitabu vingine vinasemaje katika hilo lakini naamini sio jambo njema na haviruhusu hali hiyo.


Inaruhusiwa kutompa mkono mtu ambaye unahisi amekiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu,na ni mtu ambaye amejiandaa kuitia mikono yako katika Shari! Si kosa kukataa kumpa mkono yeyote ambaye wewe unahisi anakula haramu huku akijua kua haramu ni kosa.


Ikumbukwe kua Suala la kumhudumia Maalim Seif sio la Dkt Shein wala Rais Magufuli bali ni utaratibu wa kikatiba. Seifu analazimika kukubali kuhudumiwa na kinachotokana na katiba ya wananchi wa Zanzibar, Dkt Shein naye analazimishwa na katiba kufanya hivyo maana pengine kwa nafsi yake asingekubali.Anayemtunza Maalim Seif kama waziri kiongozi na Makam wa Rais mustaafu ni Wananchi wa Zanzibar na sio Dkt Shein.


Kwahiyo kusikiliza maneno aliyoyasema Rais Magufuli tutapandikiziana mbegu za ubaguzi,Chuki na kuendelea kusababisha utengano katika jamii. Dkt Shein anatakiwa kuangalia imani yake inasemaje na sio misukumo ya kisiasa.Sisi sote ni ndugu, taifa ni moja tuepuke kauli za kutubagua.
Alichoongea JPM kuwa kama angekuwa yeye ndiye aliyenyimwa kupewa mkono na Maalim wakati wa msiba wa Aboud Jumbe na yeye asingesaini malipo ya pensheni ya Maalim Seif, hiyo ni 'pure' ulevi wa madaraka.

Suala la pensheni ya Maalim ni suala lililo ndani ya Katiba ya nchi, kwa hiyo siyo suala la Rais aliyeko madarakani kutaka au kutotaka.


Kwa muendelezo wa matamko mbalimbali ya JPM ya kuisigina Katiba ya nchi waziwazi ni uthibitisho mwingine kuwa Katiba ya nchi ingawa aliapa kuitii na kuilinda, lakini kwake yeye anaiona si lolote wala chochote bali yeye ndiye EACH and EVERYTHING.....
 
Alichoongea JPM kuwa kama angekuwa yeye ndiye aliyenyimwa kupewa mkono na Maalim wakati wa msiba wa Aboud Jumbe na yeye asingesaini malipo ya pensheni ya Maalim Seif, hiyo ni ulevi wa madaraka.

Suala la pensheni ya Maalim ni suala lililo ndani ya Katiba ya nchi, kwa hiyo siyo suala la Rais aliyeko madarakani kutaka au kutotaka.

Kwa hiyo ni takwa la kikatiba Maalim kulipwa hiyo pensheni.

Kwa muendelezo wa matamko wa matamko mbalimbali ya JPM ya kuisigina Katiba ya nchi waziwazi ni uthibitisho mwingine kuwa Katiba ya nchi ingawa aliapa kuitii na kuilinda, lakini kwake yeye anaiona si lolote wala chochote bali yeye ndiye EACH and EVERYTHING.
1473041370479.jpg
 
sasa mbona yeye anasema msema kweli ni mpenzi wa Mungu, ni Mungu wa alphabet inayoanzia na m au M?
Kwa kweli watu wengi tunashindwa kumuelewa JPM anaposema mtu mkweli ni mpenzi wa Mungu na rai yake ya mara kwa mara kwa watanzania kuwa wamwombee kwa Mungu huwa anamaanisha nini?

Kwa kuwa kitendo chake cha kutangaza hadharani kuwa anapendekeza Jecha apewe nishani ya utumishi uliotukuka, wakati ndani ya nafsi yake anajua kabisa kuwa Jecha 'aliyapindua' matokeo halali ya uchaguzi uliokuwa huru na wa haki wa tarehe 25/10/2015, kwa kweli yale maneno hayakupaswa kabisa kutolewa na Mkuu wa nchi.

Ningemuelewa vyema JPM endapo angependekeza nishani hiyo ya utumishi uliotukuka badala yake angesema apewe Jecha kutokana na umahiri wake wa 'kuyapindua' matokeo halali ya wapiga kura wa Zanzibar kwenye uchaguzi mkuu wa October 25 mwaka jana..........
 
Back
Top Bottom