Zanzibar: Serikali yalaani vitendo vya unyanyasaji wa kidini vinavyoendelea visiwani

Zanzibar: Serikali yalaani vitendo vya unyanyasaji wa kidini vinavyoendelea visiwani

View attachment 2949080

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imehimiza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutenda mema na kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Zanzibar ni nchi yenye historia kongwe ya uvumilivu wa kidini ambapo Uislamu na Ukristo uliingia mapema kuwa sehemu muhimu ya utamaduni uliodumu kwa karne nyingi. Hii inatufundisha kuhusu ustaarabu wa Wazanzibari kuvumiliana kidini na ndio msingi wa mshikamano miongoni mwetu.

Serikali inalaani vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea kufanyika sehemu mbalimbali Zanzibar, kadhia hiyo ni kinyume na misingi ya kuvumiliana katika imani za kidini.

Aidha, Serikali inawahimiza wananchi kujizuia kwa namna yoyote ile kuingilia uhuru wa mtu binafsi katika kuabudu.

Ikumbukwe Zanzibar inaongozwa kwa Katiba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mamlaka ya kullinda Katiba ya nchi na watu wake, hivyo hatua yoyote ile yenye kuhatarisha Umoja, Amani na Mshikamano haitavumiliwa.

Serikali itaendelea kulinda haki na uhuru wa mtu kuabudu kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Hivyo, tuendelee kudumisha amani na upendo kama mafundisho ya dini zetu yanavyotutaka, tofauti zetu za kidini zisiwe chanzo cha kuvuruga amani, umoja na mshikamano.
Upuuzi mtupu, meneno mengi hakuna dhima hata moja,.
 
1711805402150.png

Blabla tupu!!

Yaleyale ya hili mkalitazame
 
Serikali ya Zanzibar imelaani vitendo vya kinyanyasaji vinavyoendelea kuripotiwa katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa matendo hayo ni kinyume na ustaarabu wa Zanzibar na misingi ya kuvumiliana katika imani za kidini.

Hayo yamebainishwa na Msemaji wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Charles Hillary kwenye taarifa yake kwa Umma.

Hillary ameendelea kuwakumbusha wazanzibar kuwa nchi hiyo inaongozwa na katiba na sheria na hatua yoyote ile yenye kuhatarisha umoja, amani na mshikamano haitavumiliwa bali itachukuliwa sheria mara moja.

Serikali ya Zanzibar imetoa taarifa hiyo kufuatia kusambaa kwa video kadhaa katika mitandao ya kijamii zikionesha wananchi wakiwachapa viboko nwananchi wenzao kwa madai ya kula hadharani msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
 
View attachment 2949080

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imehimiza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutenda mema na kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Zanzibar ni nchi yenye historia kongwe ya uvumilivu wa kidini ambapo Uislamu na Ukristo uliingia mapema kuwa sehemu muhimu ya utamaduni uliodumu kwa karne nyingi. Hii inatufundisha kuhusu ustaarabu wa Wazanzibari kuvumiliana kidini na ndio msingi wa mshikamano miongoni mwetu.

Serikali inalaani vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea kufanyika sehemu mbalimbali Zanzibar, kadhia hiyo ni kinyume na misingi ya kuvumiliana katika imani za kidini.

Aidha, Serikali inawahimiza wananchi kujizuia kwa namna yoyote ile kuingilia uhuru wa mtu binafsi katika kuabudu.

Ikumbukwe Zanzibar inaongozwa kwa Katiba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mamlaka ya kullinda Katiba ya nchi na watu wake, hivyo hatua yoyote ile yenye kuhatarisha Umoja, Amani na Mshikamano haitavumiliwa.

Serikali itaendelea kulinda haki na uhuru wa mtu kuabudu kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Hivyo, tuendelee kudumisha amani na upendo kama mafundisho ya dini zetu yanavyotutaka, tofauti zetu za kidini zisiwe chanzo cha kuvuruga amani, umoja na mshikamano.
A stitch in time, maana huku Bara tungeamua kujibu mapigo Wanzibari wangerudi kwao Mchambawima!
 
Kwaiyo hatua gani ina/itachukuliwa juu ya waathirika wa mashambulizi ayo?

Shida watu wanajilazimisha kushinda njaa badala ya kufunga, ilitakiwa watu wapewe elimu ya iman zaidi juu ya mfungo
 
Kwanini ile kampuni imepigwa fine kwa mtalii kula hadharani? Watawachukulia hatua gani walio fanya hivyo? Wanafanya hivyo kwa sheria gani?
 
Wale police walikuwa wamesema wamekamata watu 12 wanaokula mchana wao ni police wa nchi gani??
 
Watu wakiamua kwa dhati kuacha kutumia akili (reasoning), wapo busy kutumia hisia kwa mambo yanayohitaji kuwaza, no hatari sana. Nile mimi, wewe ukwazike, nile mimi, funga yako iharibike..that's total shyte.
 
Tunataka kuona wahusika wakichukuliwa hatia na mhanga aombwe radhi kwa kudhalilishwa hadharani!
 
Kulingana na waraka huo, anayeingilia uhuru wa kuabudu wa mtu mwingine, ni anayekula hadharani wakati wa mfungo.

Swali linabaki pale pale, Sheria inasemaje?

Na Serikali ya MAPINDUZI Zanzibar Ina dini?
Aliyeingilia uhuru wa mwenzake ni aliyefunga wakati wengine wanatakiwa kula!
 
Uvumilivu ni kitu muhimu sana katika mfumo wa Maisha...ukila ng'ombe wengine ni myama muhimu katika kuabudu kwao....
 
SMZ inaogopa kuchukua hatua kali kwa waliotenda makosa matokeo yake inaishia kulaaani tu.

Siasa za Zanzibar ni mbaya mnooo,
Mwinyi anajua fika akitumia nguvu juu ya suala ilo iyo itakua mbaya san kwake kwenye uchaguzi wa 2025.

Anajua fika akitumia nguvu ya kuwashughulikia hao walionyanyasa watu upinzani ndo itakua ajenda yao kuu ndio maana serekali imekuja kulaani tu na sio kuchukua hatua kali za kisheria.
 
Back
Top Bottom