Zanzibar: Simai Mohamed Said, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale ajiuzulu siku mbili baada ya kutangaza uhaba wa pombe kwenye hoteli na migahawa

Zanzibar: Simai Mohamed Said, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale ajiuzulu siku mbili baada ya kutangaza uhaba wa pombe kwenye hoteli na migahawa

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Simai Mohamed Said ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo usiku.

Mhe. Simai ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, ametangaza kujiuzulu akisema ni kutokana na kile alichokiita "MAmazingira yasiyo rafiki ya kazi."
---

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt. Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.

“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni.

Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.” - sehemu ya taarifa yake ya kujiuzulu


Siku mbili zilizopita, Januari 24 Waziri huyo mwenye dhamana ya Utalii alitangaza uhaba wa pombe katika hotel na migahawa

“masikitiko yamekuwa makubwa na imenibidi niitishe kikao kwa sababu nimeanza kunyooshewa mkono na Wadau, mimi kama Baba wa Mahoteli na Migahawa lazima nionane nao kwani Sekta ya utalii si vyema ikachezewachezewa”

“Tumeona maamuzi ya Bodi ya Vileo Zanzibar imewaondosha wale waliokua wanahusika kama ZMMI, Scoch na One Stop, nimeanza kuona athari hoteli nyingi wameanza kukosa huduma ya Vinywaji baada ya Bodi ya Vileo kufanya maamuzi hayo, niwaombe Wawekezaji waendelee kuwa Wavumilivu wakati huu ikitazamwa namna ya kutatua jambo hili”

Mwisho wa kunukuu. Zaidi soma Waziri: Zanzibar inakabiliwa na upungufu wa Pombe kwenye Mahoteli
Saudia wameona mbali sana, wakaamua kuruhusu pombe mapema tu, vingenevyo wananchi wa Saudia wangeweza kuja kupindua serikali huko mbeleni sababu ya kuwakosesha pombe, maana wengi ili wanywe pombe hulazimika kusafiri hadi Afrika, Ulaya na Marekani.
 
Jamaa alikuwa ana mipango na visheni kubwa Zanzibar iwe kitovu cha utalii majengo malikale kama Greece ipokee walau watalii milioni 5 kabla ya 2023
1706264419539.png

Picha: mitaa ya Corfu Greece.

Waziri alitaka mji mkongwe wa Stone Stone ufikie level za Corfu Greece n.k Nasi kule Bagamoyo moyo mji wetu wenye majumba kale nao ungejikonjoja kukarabati majengo kuvutia utalii wa mapumziko na pwani ya mchanga mweupe kama Oia Santorini Greece, Copa Cabana au Cancun Latin America n.k.


TOKA MAKTABA:






Muscat - Oman 13-02-2023
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Mheshimiwa Simai Mohammed Said akiambata na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe na Mkurugenzi wa Makumbusho na Mambo ya Kale wapo ziarani nchini Oman kwa lengo la kukuza uhusiano baina ya Zanzibar na Oman huku nchi mbili hizi kufikia muafaka wa uwekaji saini baina ya Serikali ya Oman na Kampuni Nandhra Engineering and Construction Company Limited ya Tanzania kwa ajili ya kuanza ukarabati mkubwa wa Jengo la Makumbusho la Bait Al Ajaib.
Ujenzi huu ambao utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Millioni 21 (21Mil US$, takribani Shilingi Bilioni 50) unatakiwa matayarisho yake kuanza mwezi huu February 2023 na Mkandarasi anatakiwa kuanza rasmi ujenzi wake ndani ya miezi mitatu ijayo na unatakiwa ukamilike ndani ya muda wa miaka mitatu.

Katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, Mheshimiwa Simai ameeleza kwamba ujenzi huo unatarajiwa kuanza mapema ndani ya miezi mitatu mara tu ya utiaji saini wa mkataba huo na fedha hizo zitatumika katika kutayarisha mambo yanayohitajika kuufanikisha ujenzi huo.

Jengo hilo la kihistoria linatarajia kuwa na Makumbusho kubwa ya kisasa kwa ajili ya kuihifadhi na kuitangaza historia ya Zanzibar kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.

Aidha, Mhe.Simai amesema, utiaji saini wa Mkataba huo kutapelekea kuzileta nchi mbili hizi karibu zaidi pamoja na kukuza na kuendeleza ushirikiano uliopo, huku akiongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale itaendelea kushirikiana na Serikali ya Oman katika kuliendeleza na kulisimamia Jengo hilo ambalo ni urithi Mkubwa na mashuhuri Barani Afrika.
Ujumbe wa waziri wa Utalii na mambo ya Kale wa Zanzibar Mheshimiwa Simai Mohammed Simai unatajiwa kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya makumbusho na ngome za Kihistoria kama vile Ngome kongwe ya Nizwa (Nizwa Fort), Makumbusho ya Taifa ya Oman na Royal Opera House ikiwa ni sehemu ya kujionoea na kujifunza uhifadhi wa historia ya nchi zetu.

Itakumbukwa kuwa Jengo la kihistoria la Bait Al-Ajaib lilijengwa na Mfalme wa pili wa Zanzibar Sultan Barghash Bin Said hapo mwaka 1883 na mnamo Disemba mwaka 2020 jengo hilo liliporomoka sehemu kubwa na kulazimika kufanyiwa ukarabati mkubwa.
Jengo la Bait Al Ajaib ni moja ya sehemu muhimu ya Hifadhi ya Mji mkongwe unatambulika kimataifa na Jumuiya ya UNESCO.
 
Si haba wameanza mdogo mdogo.....
Ati unaambiwa usinywe Pombe ya Duniani subiri mpaka UFE halafu utaenda kunywa huko MBINGUNI.🤨🤨😝🤣🤣

Mimi nasemaga hivi CHANGANYA NA ZAKO Ulabu ni hapa hapa Breweries nyingine Stori tu.

Ila kunywa kistarabu.
 
Wabara ndo mana mtazidi kuwa maskini na kukosa maendeleo hadi kiama. Uongozi ni utumishi sio ajira. Mawazo yenu ya kuwaza uongozi ni ajira ndo mana mnaendekeza maslahi binafsi na mnashindwa kusimamia ukweli kwenye masuala ya msingi.

Hongera sana kwa huyu Waziri aliyejiuzuru. Anaonekana tu ni mtu smart na ndo mana Zanzibar inapiga hatua sana kwenye maendeleo. Inaelekea Mwinyi anajali sana smartness kuliko machawa na watu maslahi
Kwani amejiuzuru kwenye serikali ya Mapinduzi Zanzibar au serikali ya Muungano? Kama amejiuzuru kwa kuwa ni smart, basi ametofautiana na watu ambao sio smart, na ambao kimsingi wapo kwenye serikali aliyojiuzuru (ya Zanzibar)
 
Watanzania tuna shida kubwa sana. Inataka mtu mmoja tu kusema ‘mow’, wengine wote tunafuatia kuitikia ‘mow’.

Like seriously, habari ipo wazi chanzo cha tatizo ni kubadili utaratibu wa kuagiza na kuleta suppliers wapa (ambao kazi awaiwezi) hadi kupelekea mapungufu.

Habari aina uhusiano wowote na Zanzibar kuzuia pombe, wala imani yake kuhusu pombe kama sababu ya waziri kujiudhuru.

If anything rushwa kama ilivyo taratibu zetu, kuna uwezekano mkubwa kapokea hongo kubadili mambo; matokeo yake kapeleka madhara ya uhaba na kaamua kuachia nafasi akatumbue vizuri hela zake za zawadi.

Hivi watu uwa mnasomaga hata hizo main posts kabla ya kuchangia, au mnasoma michango tu na kuwa influenced nayo based on your ideological biases.

Such a gullible society.
 
Kwani zenji pombe hamna ? Kama hujawahi kufika basi unadanganywa ..Zenji pombe zipo miaka kibao kwa sababu ya utalii...Zenji hawana ubaguzi watu kibao wanatoka bara wanaenda kufanya biashara za kujiuza kwa watalii


Zenji jaribu kufika utaona huku bara tunaleta porojo...zenji wapo peace kwa sana ...
Wee jamaa hebu acha uongo Zenji ipi hakuna ubaguzi!!
Wewe jamaa wee mimi ni muslim lakini swala la ubaguzi zenji mtu unabaguliwa hadi kwenye swafu katika swala unaongea nini aisee huwa mnafanya watu hawajafika Zenji ama?
Eti Zenji hakuna ubaguzi!!!
 
Islamic state na pombe, wapi na wapi!! Tena mpaka inaadimika!! Maana yake watu wanagigida tu kama wapo ile mitaa ya starehe mfano Sinza, nk.
 
Wee jamaa hebu acha uongo Zenji ipi hakuna ubaguzi! Wewe jamaa wee mimi ni muslim lakini swala la ubaguzi zenji mtu unabaguliwa hadi kwenye...
Hakuna ubaguzi acha porojo watu wasingeenda ...Ubaguzi upi au umezaliwa mwaka 2000..Sehemu yenye ubaguzi hata kwenda huwezi kwenda wala walikuwa wakisema wabara wana vichongo , wakija huku tunawaita wazenji wamelegea wazee wa urojo.

Huu ni utani wa karne miaka kibao.. kubaguliwa ulipigwa ukauliwa ,ulikosa huduma kisa ni mbara?
 
Back
Top Bottom