Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Kidiplomasia kwa lipi sasa? Huyo mtalii alienda kupumzika na kulala, maandishi kwenye gari yalimhusu nini? Kutopenda Palestina kwake,ndo kufanye wengine wasiandike wanavyotaka?
Kama ni hivyo, basi hata majina ya Hoteli wengine hawayapendi.
Je,akiingia bara si ndo atajinyonga!
 
Akili kibajaji hizi! Basi serikali ikishapiga marufuku ije na kwenye Bendera za Israel/ Saudiarabia kwenye biashara kadhaa....Ikitoka apo ije ipige na masanamu ya imani fulani kwenye majumba yetu maana nayo yanawakwaza watu wengine nk nk nk.... Biashara ni huru sehem X inakukwaza kwa huduma zao nenda sehem Y.... Ndo wale wale waliokua wanamsema Mzee Azam kua ni mdini lakini Mzee Marehem Mengi sio...Poor mindset
 
Habari imeandikwa kwa kiingereza kwamba..."they were complaining "..!Unajua lugha ya mzungu ni sumbufu kwangu.Neno linaloendana na fujo sijaliona zaidi ya aliyeleta kutueleza kwenye kichwa cha habari.Anaitwa "green rajab"!
 
Sishangai, ni kwakuwa huna experiences na utoaji wa huduma hizo
 
Tofautisha uwekaji wa bendera,misalaba,nyota na mwezi,kengele na sanamu sehemu za makanisa au imani fulani na kuweka hizo alama,bendera na mabango kwenye huduma za umma.Utakapo kufanya hayo ni vema ukawapa watumia huduma hadhari au bango linalojieleza kabisa.
 
Unaishi maisha ya kukariri na kifua chako kimejazwa chuki uliyoimeza kwa hiyari yako.Nikikuuliza:Ni nini kibaya Waizraeli wamekufanyia wewe kama wewe utatusaidia jibu?
So kwa ufinyu wako wa Medula neno "Free Palestine" ndo liwakwaze hao mashoga.... Kwanza wamecheleweshwa ilapaswa kua historia kwa sasa.....
 
Sishangai, ni kwakuwa huna experiences na utoaji wa huduma hizo
Nina experience kubwa sana, wabongo mnapenda kufanya kazi kwa mazoea na kutoweka u serious unaostahili, serikali yenye imeshalalamika watalii wengi wakija bongo mara moja hawarudi tena.
 
Umetafakari kwa kina au umekurupuka kumbuka Hilo ni gari binafsi ni kama wewe ukiwa na gari yako ndani umeweka bendera ya Chadema afu ukalipaki kazini kwako afu wafuasi wa CCM walalamike
wageni wameleta pesa badala ya kuwabembeleza unafukuza meneja wa hoteli anatakiwa atoe maelezo
 
Aliyeitoa hiyo taarifa naona hajui impact ya hicho alichokifanya, Zanzibar inategemea sana watalii na wanatakiwa kujua asilimia kubwa ya watalii ni Wazungu na sio waarabu sasa kwa kuleta mambo kama hayo naona kabisa wanachochea moto wa kifuu, siku watalii wakisusa wasianze kulia Lia
 
Kwaiyo wajadiliane nini hapo zaidi ya ao Waisrael kukuambia toa ilo gari? Mbona mmejaza bendera za Israel kwenye magari yanu hakuna anaewapigia kelele?
 
Sasa hizi ni story zako za kufikirika nje ya habari iliyoletwa hapa, hakuna sehemu katika habari imeelezwa hivyo.

Tuseme ilikuwa hivyo, umeona usalama wako uko hatarini ndio ufanye fujo? Usalama ukiwa hatarini best option ni kuhama hoteli au kufanya fujo?
 
Unajuaje kama walitaka kurudishiwa pesa zao Hotel wakaanza kuleta danadana??
 
Unajuaje kama walitaka kurudishiwa pesa zao Hotel wakaanza kuleta danadana??
Hizo pia ni stori za kufikirika, guys... tujadili kilicholetwa hapa.
 
H


Hata Marekani Kuna watu wanavaa tisheti zimeandikwa free palestine, wakati fulani free Mandela. Hiyo sio tatizo, ingekuwaje wangekuta mtu kaweka bendela ya Israel kwenye gari lake wangelalamika
Labda kama bango lemewekwa hotelini hiyo sio sawa
Ile ni biashara, inayohudumia wageni mbalimbali. Kwenye migogoro ya kimataifa hawakupaswa kuonyesha upande wao ni upi.
Sasa tofauti na ww kununua tshirt na kuvaa au mwingine yoyote
 
Uko sahihi kwenye suala hili.

Wanatakiwa kukumbuka kwamba mabaya huvuma zaidi kuliko mema. Isitoshe, watalii wengi sana hapa duniani wanatokea ktk nchi nyingi ambazo zinaunga mkono upande wa Israel na washirika wake wa Magharibi na Marekani.
Jambo hili walipaswa walidhibiti ili kusudi lisisambae kama hivi ilivyotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…