Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Hii habari imekaa kishabiki kuliko uhalisia, upande wa pili sio habari za kushabikia ikiwa mnapenda kuongeza mapato ya kitalii.
Kama ni kweli kuna tukio kama hilo, suluhisho lilikuwa majadiliano na kulimaliza kidiplomasia.
Sio sahihi sana kuweka itikadi kwenye biashara.
Kidiplomasia kwa lipi sasa? Huyo mtalii alienda kupumzika na kulala, maandishi kwenye gari yalimhusu nini? Kutopenda Palestina kwake,ndo kufanye wengine wasiandike wanavyotaka?
Kama ni hivyo, basi hata majina ya Hoteli wengine hawayapendi.
Je,akiingia bara si ndo atajinyonga!
 
Serikali ya zanzibar ipo na inajivunia kupata hela kupitia utalii, ipige marufuku stika zote za namna hiyo ili kuepuka kukwaza wateja kutoka kwenye mataifa yanayosigana na mahasimu wao. Hata bara upuuzi huo wa mabango hayo upigwe marufuku, hela za watalii wa kiisrael na washirika wao tunazihitaji tufanye maendeleo yetu
Akili kibajaji hizi! Basi serikali ikishapiga marufuku ije na kwenye Bendera za Israel/ Saudiarabia kwenye biashara kadhaa....Ikitoka apo ije ipige na masanamu ya imani fulani kwenye majumba yetu maana nayo yanawakwaza watu wengine nk nk nk.... Biashara ni huru sehem X inakukwaza kwa huduma zao nenda sehem Y.... Ndo wale wale waliokua wanamsema Mzee Azam kua ni mdini lakini Mzee Marehem Mengi sio...Poor mindset
 
Mkuu, maelezo yote yapo. Kuwa walilalamika na kuleta fujo. Sasa kama walileta fujo wangeachwa tu?
By the way, kilichowakwaza wao nini? Ingekuwa gari ya mteja mwenzao wangetaka iondolewe? Au kisa gari ya manager?
Supposedly, hiyo gari ni ya mtu mwingine tu tumfukuze kisa we unakwazika na maandishi yaliyo kwenye gari ya mtu?
Habari imeandikwa kwa kiingereza kwamba..."they were complaining "..!Unajua lugha ya mzungu ni sumbufu kwangu.Neno linaloendana na fujo sijaliona zaidi ya aliyeleta kutueleza kwenye kichwa cha habari.Anaitwa "green rajab"!
 
Mtakuwa mliwaamisha Hotel yenu ni kubwaaa kwenye marketing au website yenu wanafika wanakuta watu wanapishana kwenye corridor kiubavu ubavu halafu humo humo wanabishana mipira ambayo wao hata hawaijui, au mnafanyia birthdays na vi kitchen parties, hapo lazima pachimbike.
Sishangai, ni kwakuwa huna experiences na utoaji wa huduma hizo
 
Akili kibajaji hizi! Basi serikali ikishapiga marufuku ije na kwenye Bendera za Israel/ Saudiarabia kwenye biashara kadhaa....Ikitoka apo ije ipige na masanamu ya imani fulani kwenye majumba yetu maana nayo yanawakwaza watu wengine nk nk nk.... Biashara ni huru sehem X inakukwaza kwa huduma zao nenda sehem Y.... Ndo wale wale waliokua wanamsema Mzee Azam kua ni mdini lakini Mzee Marehem Mengi sio...Poor mindset
Tofautisha uwekaji wa bendera,misalaba,nyota na mwezi,kengele na sanamu sehemu za makanisa au imani fulani na kuweka hizo alama,bendera na mabango kwenye huduma za umma.Utakapo kufanya hayo ni vema ukawapa watumia huduma hadhari au bango linalojieleza kabisa.
 
Unaishi maisha ya kukariri na kifua chako kimejazwa chuki uliyoimeza kwa hiyari yako.Nikikuuliza:Ni nini kibaya Waizraeli wamekufanyia wewe kama wewe utatusaidia jibu?
So kwa ufinyu wako wa Medula neno "Free Palestine" ndo liwakwaze hao mashoga.... Kwanza wamecheleweshwa ilapaswa kua historia kwa sasa.....
 
Sishangai, ni kwakuwa huna experiences na utoaji wa huduma hizo
Nina experience kubwa sana, wabongo mnapenda kufanya kazi kwa mazoea na kutoweka u serious unaostahili, serikali yenye imeshalalamika watalii wengi wakija bongo mara moja hawarudi tena.
 
Umetafakari kwa kina au umekurupuka kumbuka Hilo ni gari binafsi ni kama wewe ukiwa na gari yako ndani umeweka bendera ya Chadema afu ukalipaki kazini kwako afu wafuasi wa CCM walalamike
wageni wameleta pesa badala ya kuwabembeleza unafukuza meneja wa hoteli anatakiwa atoe maelezo
 
Aliyeitoa hiyo taarifa naona hajui impact ya hicho alichokifanya, Zanzibar inategemea sana watalii na wanatakiwa kujua asilimia kubwa ya watalii ni Wazungu na sio waarabu sasa kwa kuleta mambo kama hayo naona kabisa wanachochea moto wa kifuu, siku watalii wakisusa wasianze kulia Lia
 
Hii habari imekaa kishabiki kuliko uhalisia, upande wa pili sio habari za kushabikia ikiwa mnapenda kuongeza mapato ya kitalii.
Kama ni kweli kuna tukio kama hilo, suluhisho lilikuwa majadiliano na kulimaliza kidiplomasia.
Sio sahihi sana kuweka itikadi kwenye biashara.
Kwaiyo wajadiliane nini hapo zaidi ya ao Waisrael kukuambia toa ilo gari? Mbona mmejaza bendera za Israel kwenye magari yanu hakuna anaewapigia kelele?
 
Wao walikuwa concerned na usalama wao .Sababu pale ni hoteli .Ina maana walipoingia hawakuona kitu kama hicho .Yawezekana huyo meneja baada ya kuona kuna waisrael hapo na ukereketwa wake wa kidini akaenda kuandika gari yake Free Palestine kwa makusudi ya kuwasuta au kuwapa mipasho hao wateja wake wayahudi.Hotel sio sehemu ya mwenye hotel au meneja kuwasuta au kuwapa mipasho wateja wake.Alichokifanya ni kuwapa mipasho na kuwasuta wateja wake kwa maandishi kwenye eneo la kupaki magari.Kibiashara haiko sahihi
Sasa hizi ni story zako za kufikirika nje ya habari iliyoletwa hapa, hakuna sehemu katika habari imeelezwa hivyo.

Tuseme ilikuwa hivyo, umeona usalama wako uko hatarini ndio ufanye fujo? Usalama ukiwa hatarini best option ni kuhama hoteli au kufanya fujo?
 
Unajuaje kama walitaka kurudishiwa pesa zao Hotel wakaanza kuleta danadana??
 
H

Hata Marekani Kuna watu wanavaa tisheti zimeandikwa free palestine, wakati fulani free Mandela. Hiyo sio tatizo, ingekuwaje wangekuta mtu kaweka bendela ya Israel kwenye gari lake wangelalamika
Labda kama bango lemewekwa hotelini hiyo sio sawa
Ile ni biashara, inayohudumia wageni mbalimbali. Kwenye migogoro ya kimataifa hawakupaswa kuonyesha upande wao ni upi.
Sasa tofauti na ww kununua tshirt na kuvaa au mwingine yoyote
 
Hii habari imekaa kishabiki kuliko uhalisia, upande wa pili sio habari za kushabikia ikiwa mnapenda kuongeza mapato ya kitalii.
Kama ni kweli kuna tukio kama hilo, suluhisho lilikuwa majadiliano na kulimaliza kidiplomasia.
Sio sahihi sana kuweka itikadi kwenye biashara.
Uko sahihi kwenye suala hili.

Wanatakiwa kukumbuka kwamba mabaya huvuma zaidi kuliko mema. Isitoshe, watalii wengi sana hapa duniani wanatokea ktk nchi nyingi ambazo zinaunga mkono upande wa Israel na washirika wake wa Magharibi na Marekani.
Jambo hili walipaswa walidhibiti ili kusudi lisisambae kama hivi ilivyotokea.
 
Back
Top Bottom