Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Umeielewa vibaya kauli ya Raisi nadhani. Kama na ww ni mmoja wa hao wanaotaka kuleta vurugu hiyo kauli lazima ikutishe lakin kama ni mmoja wa wapenda amani hiyo kauli hata haikuhusu kabisa
 
Sasa kama atashughulikiwa mara moja kisheria, ni kwanini basi aambiwe yeye hata kwa kunong'onezwa?! Kwanini asingetoa agizo kwa mamlaka husika na badala yake anataka aambiwe yeye?!
 
Nilopoiona hiyo kauli jana ni kaungana na T. LISSU kuwa RAIS ni dikteta.

Pia hii hapa "Mhe: Rais, Dr. Shein kama kuna tuzo za heshima utatoa na omba Jecha pia apewe". Amesimamia uchaguzi vzr sana. Hii ni kauli ya dharau kwa vyombo vya kusimamia demokrasia nchini na kwa waangalizi wa uchaguzi uliopita 2015 Kimataifa.

Nadhani Tz haina haja ya kuwa na vyama vya upinzani, wala CENTRE OF DEMOCRACY wala tume za haki za binanadamu, Rais ndie kila kitu.
 
Sasa kama atashughulikiwa mara moja kisheria, ni kwanini basi aambiwe yeye hata kwa kunong'onezwa?! Kwanini asingetoa agizo kwa mamlaka husika na badala yake anataka aambiwe yeye?!
kuna maamuzi ya kiutawala hayahusu mahakama. maamuzi ya kiutawala yapo kwa mujibu wa sheria. rais ana mamlaka kisheria ya kutenda na kuamua mengi. ila kama unamchukia kwa sababu binafsi kila alifanyalo utaona sivyo. kama hupendi anavyozungumza hilo ni tatizo lako. yeye ni rais wa jamhuri kwa mujibu wa katiba na sheria.
 
Umeielewa vibaya kauli ya Raisi nadhani. Kama na ww ni mmoja wa hao wanaotaka kuleta vurugu hiyo kauli lazima ikutishe lakin kama ni mmoja wa wapenda amani hiyo kauli hata haikuhusu kabisa
Hudhani busara ingekuongoza kuielezea hiyo kauli vizuri?! Au ni mwendelezo wa utani wa Mheshimiwa Rais?
 
Kwani Magufuli alienda Zanzibar kufanya nini? Sijaona jambo lolote alilogusia kwenye dhumuni la ziara yake

cc. FaizaFoxy
 
Toa mfano mmoja tu!!
 
Yeye ni bosi kuliko katiba na sheria zingine ? Muhimu kupenda lakini inapofika kujenga hoja jitahidi utumie kichwa na sio moyo ndugu
 
Mnachanganya kati ya UKALI na VITISHO!
 
kwa hiyo m wanachagua rais kutokana na matakwa ya Chadema? Kesho Chadema wakitaka Rais mvuta bange CCM mtamchagua sio?
 
Kufurahi au kutofurahia hali ilivyo ukifuatilia kwa undani ni mambo ya maslahi tu
 
Kazi tunayo.

Namuona ADOLF kwa mbali.
Mi simo... usije ukasema ulikuwa unachangia mada yangu! Mi simo kabisa!! Lile hitimisho la kwamba "...am ready to face...!" ni utani tu ule jombaa!!!
 
A Acha kulalamika fanya kazi mshukuru mungu kwa kupata raisi tuliekua tunamlilia siku zote.
 
A
Acha kulalamika fanya kazi mshukuru mungu kwa kupata raisi tuliekua tunamlilia siku zote.
Labda wewe na hao wenzako lakini binafsi na wote ninaowafahamu hatujapata katika maisha yetu "kumlilia" rais anayedhani vitisho ndiyo suluhu ya matatizo!!
 

ufisadi ndio unafanya mnapigania CCM
 
Ulikuwa unategemea aseme atakayeshindikana kwa Dr Shein ataitwa na Magu wapate juisi ikulu Kikwete aliwalea mkajisahau .
 
Kesho atajitokeza waziri wa muungano atasema rais alikuwa anawatania watani zake wapemba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…