Kwa bahati mbaya, jana sikupata fursa ya kufuatilia ziara ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano huko kisiwani Pemba!! Kutokana na hilo, leo nikaamua kuperuzi peruzi hapa JF na kukutana na quote ifuatayo kutoka kwa member aliyekuwa analeta updates:
Binafsi nashindwa kuamini ikiwa ni kweli hayo yamesemwa na Mheshimiwa Rais ingawaje nikipata fursa nitataza video! Sitaki kuamini ikiwa hiyo ni kauli ya Rais aliyechaguliwa kidemokrasia kwenye sanduku la kura... sitaki kuamini! Sasa ikiwa ni kweli mtu ameshindikana na Mheshimiwa Shein; yeye Mheshimiwa JPM atamfanya nini huyo mtu ndani ya hizo dakika 5?! Ni wapi tunaelekea kwenye hili taifa?! Mbona ikiwa mambo yenyewe kama ndo haya mbona hayo magereza yenu hayatatosha kufunga "wachochezi"?
Nafahamu wapo wanaofurahia na kushadadia kauli kama hizi lakini mnapaswa kufahamu fika kwamba; wote nyinyi hata kama mna kadi za CCM bado ni vidampa tu mbele ya yule Kingunge Ngombale Mwiru wa CCM!! Hata kama mna kadi tangia enzi za TANU, wote nyinyi ni vidampa tu mbele ya mtu kama Lowassa au Fredrick Sumaye wa enzi za CCM! Na si ajabu, ni vidampa hata mbele ya mtu kama Lawrence Masha aliyepata kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchi hii!!
Hii maana yake nini? Usidhani vitisho kama hivi wewe havikuhusu kwa sababu tu wewe ni kada wa CCM! Kama ndivyo unavyodhani, basi uelewa wako ni mdogo kupitiliza! Nimewataja hapo akina Kingunge ambao miezi 30 tu iliyopita wangedhani kauli za vitisho kama hizo zingewahusu! Je, mtu kama Lowassa ambae hapo kabla angedhani kauli kama hiyo haimuhusu leo anaweza kudiriki kusema hivyo? Who are ndani ya CCM compared to Kingunge Ngombale Mwiru? Ingawaje Kingunge ameetoka CCM; hivi unaamini vigogo kama Mzee Mwinyi au Pius Msekwa anaweza kukuamini kada wewe ambae kuliko Mzee Kingunge?!
Endeleeni kufurahia kauli za kutisha kama hizi lakini kaa mkifahamu hili si la mmoja! Wakati inapitishwa Sheria y Mitandao niliamini kwamba hainihusu kwa kile nilichoamini nikiwa na kauli yangu timamu siwezi kuingia online na kuanza kutukana watu hovyo, kuanza ku-post picha za utupu n.k! I swear to God, niliamini hainihusu kabisa na hata hapa niliwahi kuandika kwamba "A black cat may be a bad lucky only if you're mouse!" Lakini leo hii hakuna sheria ninayoigopa kwenye hii nchi kama sheria ya mitandao ambayo, practically imebadilika kutoka Sheria ya Mitandao to Sheria Ya Kubana Maoni!
Ajabu ni kwamba, utakuta wengi wanaoshabikia kauli kama hizi hapa JF ni vijana wadogo wengine wakiwa below 30. Don't be stupid, you've a very long way to go!! Hilo hilo unaloshabikia leo wakati hata direction ya maisha yako haija-ssettle ndio hilo hilo litakalokutafuna kesho kwenye harakati zako za kimaisha!
Ikiwa kupinga kauli ya Rais ni UCHOCHEZI, am ready to face consequences lakini kauli hiyo ya Rais haileti picha nzuri kutoka mdomoni mwa Rais aliyechaguliwa kwa sanduku la kura. Haipendezi kutoka mdomoni mwa Commanding In Chief ambae Majeshi ya Ulinzi na Usalama yapo chini yake!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Hawa watu kule kwao wanaishije?
Anthropology- Wakikubabikizia mchawi? Hata ukiwa na sura ya kutisha
Sasa ukiwa na nyenzo unaweza kufanya nini?