Zari amlipua Diamond kwamba hatoi hela ya matunzo ya watoto wake baada ya kutangaza kulipa kodi za kaya 500

Zari amlipua Diamond kwamba hatoi hela ya matunzo ya watoto wake baada ya kutangaza kulipa kodi za kaya 500

Kuna tofauti kati ya Dhambi na Uovu.

Dimond anaiogopa dhambi na kuukumbatia uovu!
Huyo mama ana matatizo yeyemwenyewe na kupenda Kiki za kipuuzi issue yake Ni ndogo ila anaikuza Iwe kubwa zari amemblock diamond,watoto kawazuia kuja huku Tanzania kumuona baba yao, angekuwa kweli ana Nia ya dhati ya kusaidiana na diamond kwanini anamuwekea diamond kauzibe? Kwanini inakuwa ngumu kwake kumpa diamond ushirikiano alafu aone Kama kweli diamond atatoa huduma.
 
Yeye kataka kushindana na mwanaume wake,haiwezekani ukambadilisha uraia mtoto bila kumshirikisha mwanaume,kisa una hela alafi mwanaume akuchekee

Mbona Hamisa sasa hivi halalamiki na mtoto huwaga anampeleka kwa baba yake siku moja moja,yy mtoto kambadilisha uraia kilazima na kwa baba yao hutaki kuwa peleka.Mbona hajaumia mwaka jana alivyo kabizi pikipiki kwa bodaboda wa Tandale,kutoa matank kwa baadhi ya shule za tandale pamoja na Insurance.

Yeye tatizo anajiona ana hela,yeye kiburi kakutana na jeuri na ndio maana baadhi ya wanaume tunaogopa kuoa wanawake wenye hela.

Mwisho wa siku anawavuruga watoto wanakuwa kama digidigi manake baba Mtanzania,Mama Mganda,Watoto wana uraia wa Afrika kusini,wakati yy hajaukana uraia wa Uganda ila kwa makusudi kawapa watoto uraia wa SA.

Hiyo haitoshi unawapeleka watoto Kanisani,wakati baba yao muislam.
Sijaona sababu ya msingi ya Diamond kuto kuhudumia watoto wake either wamekosana au wana elewana na mzazi mwenzake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo amefura kama kifutu kwanini Zari anamsema Chibu Ake
[emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka sana
1569528_20842129_1429550570443323_1178979454123691461_n.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Issue ya Zari inanikera ndo maana wanawake wenzake wengi wanamchukia kutokana kujiona boss lady ajifunze kwa madam Rita kinachomtokea baada ya kufa mengi sasa tunakuja na kauli kila #Nyuma ya boss lady Kuna sponsor.Mwambie aache ujeuri ashirikine na mwenza wake watengeneneze familia vizuri kuliko kutafuta kiki + public sympathy haitamsaidia.

Kama kuchukiwa hata Diamond anachukiwa, celeb wote wana fans na wana haters what’s your point here. Diamond hatunzi watoto wake na hana historia nzuri ya malezi period ndio ulikuwa mjadala wa msingi hapa. Kama unaona Zari anafaidi kujifanya Bosslady na wewe jifanye ili muende sawa maana sioni point ya wewe kulikazania hilo.

Mi ni fan wa Diamond we all knows hapa JF unlike nyie mashabiki wa Diamond hamuwezi kabisa kumkosoa Diamond anapokosea, Cha ajabu wahusika wote wa WCB wanalea watoto wao ni Diamond tu analeta pride sababu ni star mkubwa, nonsense!

Mwisho Zari ni kati ya wanawake ambao hawajawahi kuvictimize, hivyo usifikirie kuwa anatafuta huruma ya jamii, amemblast Diamond watu wamjue side yake ya pili and thats it!
 
Unalalamika babaako hakukutunza .halaf na ww hutinzi wa kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona issue Ni mbili tofauti baba yake alimkataa ila kwa issue hii ya zari huyo zari ndio mwenye matatizo yeye ndo anaweka kauzibe kwanza kamblock kuanzia kwenye simu mpaka kwenye social network ,kawazuia watoto wasije Tanzania kuonana na baba yao anashindwa kutoa ushirikiano mzuri kwa mzazi mwenzake alafu eti anaenda kulalamika apewi huduma public hizi Kama sio Kiki Ni Nini ampe ushirikiano mzuri diamond aone Kama diamond atatoa huduma.
 
Kama kuchukiwa hata Diamond anachukiwa, celeb wote wana fans na wana haters what’s your point here. Diamond hatunzi watoto wake na hana historia nzuri ya malezi period ndio ulikuwa mjadala wa msingi hapa. Kama unaona Zari anafaidi kujifanya Bosslady na wewe jifanye ili muende sawa maana sioni point ya wewe kulikazania hilo.

Mi ni fan wa Diamond we all knows hapa JF unlike nyie mashabiki wa Diamond hamuwezi kabisa kumkosoa Diamond anapokosea, Cha ajabu wahusika wote wa WCB wanalea watoto wao ni Diamond tu analeta pride sababu ni star mkubwa, nonsense!

Mwisho Zari ni kati ya wanawake ambao hawajawahi kuvictimize, hivyo usifikirie kuwa anatafuta huruma ya jamii, amemblast Diamond watu wamjue side yake ya pili and thats it!
Kwan diamond hawamfahamu watanzania? huyo anatafuta Kiki na si tunamfahamu vizuri Sana zari, zari Ni mwanamke wakutafuta Kiki Sana hata kwenye mambo ambayo ni useless mbona hamisa mobetto alalamiki Tena walikuwa awapo vizuri na diamond wakaa chini na wakayamaliza na hamisa mobetto akakili kabisa wakati anafanyiwa mahojiano na Sam wa misago akasema diamond anahudumia vizuri Sana na sometime anawaona watoto wake?huyo zari anashindwa vipi kukaa na diamond wakajenga kuliko kukimbilia public
 
Sijaona sababu ya msingi ya Diamond kuto kuhudumia watoto wake either wamekosana au wana elewana na mzazi mwenzake

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kwako unaweza ukaona hamna sababu ya msingi,ila yule demu ana kiburi za fedha,kwake anaona fedha ndio kila kitu.

Hivi wewe kweli kama mwanaume,unaweza ukakubali ,ukakubali mtoto wako abadilishwe uraia? Yote tisa kumi unawapeleka Kanisani,manake swala kama la imani swala jingine kabisa,kama Mondi angekuwa mtu wa swala tano hii kesi kubwa,sometimes inaweza hata ukasababisha kupotea kwa uhai wa mtu.

Siku zote mwanaume anahitaji kusikilizwa na kuheshimiwa ila kama mwanamke akikuzidi kipato ni ngumu sana kukusikiliza,wachache sana ambao wana hofu ya Mungu wanaweza wakamsikiliza mwanaume ambaye amemzidi kipato.

Zari na Mondi wanaonyeshana,Zari tokea mwanzo anamwonyesha Mondi sio kitu anaweza somesha na kuwapatia mahitaji yote muhimu bila Mondi ndio maana kaamua,kumbadilisha uraia na kuwapeleka kanisani.

Mondi nae kaona kazarauliwa ,watoto baki ukitaka huduma yangu basi lazima wafuate vile nitakavyo mimi.

Na ndio maana mahusiano kama haya mnapoteza mda mwingi kwenye mashindano,baada ya kulea watoto.Hapo kila mtu inabidi asimame kwenye nafasi ya asili.
 
Kweli kwako unaweza ukaona hamna sababu ya msingi,ila yule demu ana kiburi za fedha,kwake anaona fedha ndio kila kitu.

Hivi wewe kweli kama mwanaume,unaweza ukakubali ,ukakubali mtoto wako abadilishwe uraia? Yote tisa kumi unawapeleka Kanisani,manake swala kama la imani swala jingine kabisa,kama Mondi angekuwa mtu wa swala tano hii kesi kubwa,sometimes inaweza hata ukasababisha kupotea kwa uhai wa mtu.

Siku zote mwanaume anahitaji kusikilizwa na kuheshimiwa ila kama mwanamke akikuzidi kipato ni ngumu sana kukusikiliza,wachache sana ambao wana hofu ya Mungu wanaweza wakamsikiliza mwanaume ambaye amemzidi kipato.

Zari na Mondi wanaonyeshana,Zari tokea mwanzo anamwonyesha Mondi sio kitu anaweza somesha na kuwapatia mahitaji yote muhimu bila Mondi ndio maana kaamua,kumbadilisha uraia na kuwapeleka kanisani.

Mondi nae kaona kazarauliwa ,watoto baki ukitaka huduma yangu basi lazima wafuate vile nitakavyo mimi.

Na ndio maana mahusiano kama haya mnapoteza mda mwingi kwenye mashindani,baada ya kulea watoto.
Ukiacha hivyo huyo mama kawazuia watoto wasimuone baba yao Kama mama utoi ushirikiano kwa mzazi mwenza unakuja kulalamika public ili iweje
 
Bitter truth charity begins at home watu aina ya domo wapo wengi sana unakuta ndugu zake maskini wa kutupwa lakini yeye anaponda mali na washkaji, akipata matatizo familia inabeba mzigo, kuna jamaa alishaga tangulia mbele za haki maisha yake yalikua starehe na washkaji tu na michepuko hata mkewe alikua hana sauti ya kumuuliza matanuzi yake akaugua stroke ghafla ilipiga upande wote wa kulia jamaa akawa hata kibaruani haendi mkewe kajitahidi wee wapi ndugu aliowazarau walijichanga visent wapi mke akipigia simu wale rafiki mara waje mara visingizio kibao na wakija pangu pa kavu, watoto ada zikaisha shule walikua shule za maana sio kayumba ghafla wakaacha shule zao wakarudishwa kayumba mke kaomba sana misaada kwa marafiki za mume washkaji wanakimbia visingizio kibao mara nimesafiri mara family matters...nk familia yako ni kitu cha kwanza hayo mengine domo ni mbwembwe tu wanao ndio urithi wako mali huisha fame pia huisha, ipo siku wale watoto watakua wakubwa sijui utawaambia nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
GurU
 
hapa ndio tofauti ya mwanamuziki na msanii huwa inaonekana.

ili uwe kama diamond inabidi uwe mtu wa ajabu kabisa katika jamii.bahati mbaya ana backup kubwa ya mashabiki nzige,hata afanye nini wao ni kusujudu tu.

zari ni kielelezo cha udhaifu wa mtoto wa kike asibezwe.ila kama anayoongea yana ukweli haipendezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachokiona ni kwamba Zari ana muonekano mzuri ila ni jeuri ndani ya nyumba, kiburi chake huenda ndio kimemkimbiza Diamond, mwanamke hata umeremete kama dhahabu ikiwa huna adabu kwa mumeo unataka umpande kichwani hovyo hovyo, hayo ndio madhara yake, utaileza nini dunia, watoto wanauraia wa southafrica, mama raia wa uganda. Iweje atokee mtanzania mmoja aseme yeye ndo baba? Watafutie watoto baba yao wakizulu huko, acha mahoka, tulia watu walipiwe kodi wewe.
kiburi chake ndio kimekimbiza diamond[emoji874]

wema,peni,hamisa,tanasha nini kilimkimbiza mond!!!

huyu jamaa anaishi kisanii,tatizo wanazi wake hamuelewi kama mwenzenu anaishi kisanii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye kataka kushindana na mwanaume wake,haiwezekani ukambadilisha uraia mtoto bila kumshirikisha mwanaume,kisa una hela alafi mwanaume akuchekee

Mbona Hamisa sasa hivi halalamiki na mtoto huwaga anampeleka kwa baba yake siku moja moja,yy mtoto kambadilisha uraia kilazima na kwa baba yao hutaki kuwa peleka.Mbona hajaumia mwaka jana alivyo kabizi pikipiki kwa bodaboda wa Tandale,kutoa matank kwa baadhi ya shule za tandale pamoja na Insurance.

Yeye tatizo anajiona ana hela,yeye kiburi kakutana na jeuri na ndio maana baadhi ya wanaume tunaogopa kuoa wanawake wenye hela.

Mwisho wa siku anawavuruga watoto wanakuwa kama digidigi manake baba Mtanzania,Mama Mganda,Watoto wana uraia wa Afrika kusini,wakati yy hajaukana uraia wa Uganda ila kwa makusudi kawapa watoto uraia wa SA.

Hiyo haitoshi unawapeleka watoto Kanisani,wakati baba yao muislam.
Jf kuna makurutu wengi sana

Umeandika kwa huruma n kama
Ww ndo umetelekezwa

stidy
 
Back
Top Bottom