Simulizi : ZAWADI TOKA IKULU SEASON 2
Mwandishi : EMMANUEL VENANCE
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES
SEASON 2
SEHEMU YA 79
Maumivu makali yaliutawala mwili wangu tulikuwa tukimwagiwa maji na kushushiwa viboko mfurulizo kwa takiribani dakika kumi na sasa kuna jamaa anakuja na kutukuta tumechakazwa vilivyo alisimama mbele yetu na kutuangalia kisha akauliza
“Imekuwaje hawa watu ?”
“Tumewakuta eneo la Jeshi na tulipowasachi mmoja alikuwa na bastora mbili na risasi zake kama kumi na mbili hivi na hii inaonesh wazi kuwa hawa watu ni waharifu na huenda walipania kutuvamia hapa kambini”
Nikweli kimbo alikuwa na bastora mbili na hizo risasi zilizotajwa lakini hatukuwa na lengo la kuvamia kambi ya jeshi “eti jamani tuvamie kambi ya jeshi sisi hatujipendi?” Baada ya hayo maelezo yalionesha nikweli Kimbo alikuwa nazo hizo bastora mbili na risasi zake kumi, ndoto zakujinasua ziligonga mwamba.
Kuna bwana mmoja alikuja na kusimama mbele yetu kwenye sare yake ya kijeshi kulikuwa na kitambaa cheupe kwenye mkono kuelekea mabegani kilichoandikwa kwa maandishi mekundu herufi mbili na zikasomeka MP (Miritary Police) huyu ni asikali wa jeshi nakazi yake ni kurekebisha tabia za wanajeshi pale jeshini wanapokosea aliwaamuru wale wanajeshi kutupeleka mahabusu. Kitu ambacho Kimbo hakukikubali hata, wakati tukiwa tumebaki peke yetu Kimbo aliniambia hayuko tayari kupelekwa mahabusu za jeshi kwani tutakufa mateso ya huko siyo mchezo na hapo tulipo tunahesabika kama mateka tuliotaka kuivamia kambi ya jeshi si ajabu tukakabiliwa na adhabu ya kifo hivyo tunapaswa kuwa makini zaidi. Nikweli aliyoyasema lakini tutajinasua vipi mikononi mwa hawa watu? Hilo ni swali lakimiujiza.
Baada ya kukamilisha mazungumzo yao huko walikokuwa sasa wanarejea wanajeshi watano walifika wawili wakachomoa visu na kuzikata zile kamba walizotufunga huku tukianguka kama magunia, lakini baada ya kusimama kutoka chini alipoanguka Kimbo anazua balaa lingine lililoushitua moyo wangu na kubaki najiuliza maswali. Nilishangaa wakati tunapelekwa mahabusu alianza kuwatambua majina kwa kuwaita wale asikari wa kijeshi.
“Frenk Mchunguzi na wewe Samson Marwa leo hamnitambui siyo?” wale askari waligeukiana na kutazamana kwa hofu na mikono yako ikiwa imewahi kushika bastora kitendo kilichofanyika haraka zaidi, hapa sasa nagundua Kimbo alikuwa anakitafuta kifo tena kwa nguvu, lakini Kimbo hakuwa na wasiwasi hakuishia hapo akaendelea.
“MP Jackson Mkinga umekuwa kijana wangu leo unakiburi mpaka unanikabiri mimi mlezi wako siyo, nyie wote ni wanafunzi wangu mbona mnanishangaza” askari mmoja alimsogelea ili amtizame vizuri.
“kuwa makini wewe mbwa adui siyo mama yako.” Kauli ilitoka kwa askari mwenziye.
“Oooh! Generali Kimbo ni wewe” Frenk Mchunguzi alimtambua, vijana walishangaa sana na kujikuta wanampigia saluti na kubaki wameganda mpaka alipo kubali na mwisho wanamkumbatia kwa furaha.
Ndani ya ofisi ya mkuu wa kikosi Kimbo anakutana na Meja Athanas Ngayoma bila hata kuuliza Meja anapiga saluti na kushangazwa na kitendo cha Kimbo kuonekana mchafu mbele ya ofisi yake.
“Vipi Meja Jenerali Kimbo inakuwaje uko katika hali hii?”
“Ni vijana wako wamenikuta kambini kwao bwana si unajua tena sisi tunavyopenda, wamenishughulikia vyakutosha”
“Pole sana mkuu nitawashughulikia”
“hapana wape uhuru nilisha kufundisha usemi usemao usimulee adui maana..”
“siyo mama yako”
“Mimi sijasema bali umesema wewe” wote waliangua kicheko, tulibadilishiwa mavazi na kupewa chakula na kuhesabika kama wageni mhimu sana ndani ya eneo hili. Na baada ya hapo Kimbo alikuwa na maongezi na meja Ngayoma, Kimbo alimuomba atupe msaada kwani tunasakwa na familia ya Gao cha kwanza ni kutuhakikishia usalama hasa mimi kwani tunasakwa kama swala. Pili alimueleza jinsi Goro alivyofanya mauaji na sasa tunasakwa sisi kama wahusika wa mauaji pale Nyota Tv. Ngayoma alisema yuko tayari kutusaidia na aliahidi atalisimamia hilo swala na kulifatilia kwa karibu zaidi. Kimbo alirudi na kuniambia mambo yote yako poa chakufanya sasa ni kurudi jijini Dar, Ngayoma ni kijana wangu huyu nimemfundisha miaka ya nyuma walipokuja kwenye mafunzo maalumu kipindi hicho nikiwa arusha, ameahidi kunipa ulinzi mpaka tufike kwa rais ili tukalimalize hili swala maana tukiliendekeza Gao atatuhamisha nchini.
Basi maandalizi yalikamilika na kusindikizwa mpaka uwanja wa ndege kwaajili ya safari. Tuliondoka Mwanza tukiwa na usindikizaji wakutosha maasikari watano wa jeshi la wananchi tena waliofuzu mafunzo maalumu wakiwa wamevaa kiraia ndio waliotusindikiza, walikuwa wakitulinda na kutuhakikishia usalama wakutosha.
*****************************
Mbele ya kadamnasi mzee Manguli akitabasamu baada ya kuwa amemkabidhi binti yake kwa Von Gao kijana wa rafiki yake kipenzi shangwe na ndelemo zikazizima ukumbi mzima ukarindima kwa furaha na sasa maharusi hawa wawili walikuwa mbele ya padre Josephat kwaajili ya kuikamilisha ndoa yao.
Nyuso zao zinaonekana za furaha kwa kuwatazama lakini hatuwezi kujua mioyoni mwao wamehifadhi nini. Lakini navutiwa na furaha mioyoni mwa watu kwani kila mtu alilifurahia penzi la hawa vijana wawili toka familia mashuhuri licha ya kupendeza lakini walivutia hata kuwatizama tu ilitosha kuilidhisha mioyo ya watazamaji. Na sasa ulikua ni wakati wa kufungishwa ndoa yao rasmi, au pingu za maisha na pia tunaweza kuita mkataba wa maisha ambao ulisindikizwa na maneno haya ya viapo…..
“Pius Von Gao. Je, unakubali kumuoa Jesca Joseph Manguli awe mke wako kwenye shida na raha, uzima na maradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha?”
“Ndiyo ninakubali mpaka kifo kitakapotutenganisha”
“Jesca Joseph unakubali kuolewa na Pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na amaradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha? ” kimya kilitanda, hakuna jibu lolote lililotolewa hali iliyomfanya Padre kurudia tena kuuliza.
“Jesca Joseph unakubali kuolewa na pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na maradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha ” bado jibu likawa ni kimya na awamu hii uso wa Jesca ulikuwa ukitokwa machozi. Padre hakukata tamaa alirudia tena.
“Jesca Joseph unakubali kuolewa na Pius Von Gao awe mume wako kwenye shida na raha, uzima na amaradhi mpaka kifo kitakapo watenganisha? ”
“Hapana!” watu aaaah! Minong’ono, Padre alirudia tena kupata uhakika zaidi jibu lilibaki kuwa hapana na hata aliporudia tena bado ilibaki kuwa hapana. Mzee Manguli alikuwa kafula kwa hasira na asijue chakufanya upande wa mzee Gao alikuwa kasimama walijitahidi kuvumilia lakini wakashindwa alijaribu kujikanyaga walau kuzificha hasira lakini ilishindikana. Ni aibu, aibu ambayo haitaweza kusahaulika ni mbele ya wageni marafiki kutoka nchi mbali mbali, marafiki maarufu kutoka mataifa tofauti, wafanya biashara na watu mashuhuli ni aibu kubwa si yakusimulika.
Jesca hakuishia hapo alisogea karibu na kipaza sauti mbele ya ukumbi huku watu wakimshangaa na wakinong’ona kila mtu alichokijua yeye, maana tayari alikuwa ametibua nyongo za watazamaji na washiriki wote katika harusi hiyo alianza kuongea kwa huzuni.
“Mabibi na mabwana nasimama mbele yenu, kuzungumza nanyi najua mlijua leo ni siku yangu mhimu katika historia ya maisha yangu na ndiyo maana mmejitokeza kwa wingi kuja kuniunga mkono katika safari hii mhimu.” Alipumzika kidogo!!.
“Kinyume na matarajio yenu nimefanya uamzi tofauti ila naamini ni uamzi sahihi maana ndoa ni pingu ya maisha ukikosea kuingia kwenye ndoa nahisi utakuwa umeyavuruga maisha. Nafanya uamzi huu mbele yenu kuiahirisha ndoa niliyoilidhia mwenyewe hapo awali baada ya kuyaona mapema makucha ya mwenzi wangu aliyokuwa kayaficha. Nibora uonekane hufai katika jamii, uonekane mjinga katika jamii, usiogope aibu na kushindwa kuisimamia haki. Leo mnaona kama nimetia aibu lakini kuna kitu hamkijui, yanini niogope aibu kwa kuwafurahisha ninyi na wazazi wangu ilihali naenda kuishi maisha ya mateso kama mnyama wa mwituni?”. Alimeza mate kidogo huku ukumbi ukiwa kimya na ilikuwa kimya kweli maana Jesca aliongea maneno mazito kuliko umri wake.
“Mpumbavu huu ongopa ukweli na muongo daima huwa mnafiki maana huamua asilo likusudia, najua mnanishangaa na wengine kujiuliza kama sikutaka kuolewa yanini nivae gauni la harusi. Ukweli ni kwamba Familia ya mzee Gao wanayaingilia maisha yangu binafsi na lengo lao ni kuyavuruga maisha yangu hivi leo mnafanya hivi nikiwa kwetu nakesho nitakapokuwa ndani ya familia yenu itakuwaje?. Jesca alisita kidogo na kisha kumgeukia Von Gao Mchumba wangu Von maana katu huwezi kuwa mume wangu cha kwanza tambua kuwa sikukupenda toka awali, pili acha kufanya unachokifanya kwa watu wasio na hatia au mnataka niseme kinachoendelea?”
“sema… sema… tueleze…” aliendelea baada ya kelele za watu kumtaka aseme “familia ya Gao inahusika na kuharibu maisha yangu kwanza walimteka na kumtesa na kumfirisi kijana Jamae Justine huku wakihusika na kuichoma moto Kampuni yake, pili wanamtafuta kumuua mpaka hivi tunavyoongea ni watu kumi na wawili wameesha poteza maisha wakiwemo wafanyakazi wa Nyota Tv katika msako wa kumuuwa Jamae lengo ni kuhakikisha wanayapoteza maisha ya Jamae” watu wanashika midomo kwa mshangao, Mzee Gao kajiinamia na mwanae alikuwa akipumua kwa taaabu huku akitetemeka.
“Nina ujauzito wa miezi mnne lakini baba yangu aliamuru niolewe tu na Von pamoja na kuwa na mimba ya Jamae… familia yangu haitendi haki kwangu na wala hawazijali hisia zangu juu ya kipi ninachokipenda. Nahitaji kuheshimiwa na kulindwa lakini wakwe zangu na wazazi wangu namaanisha watu wa karibu zaidi ndiyo wananiangamiza”
Watu walikuwa kimya wasiamini kilichokuwa kikiendelea.
Mzee Manguli aisimama na kwenda mbele alipokuwa kasimama binti yake alifika na kumbamiza bonge la kibao shavuni kisha alishika mike kwa hasira.
“katika kizazi changu sikuwahi kufikiria kuwa na mwana mpumbavu kama huyu binti na nahisi hawezi kuwa mwanangu pengine mama yake anapaswa kutueleza vizuri alimtuoa wapi huyu binti?” Mzee Manguli alikuwa akiongea kwa hasira sana.
“Tunasikia porojo nyingi zisizo na ukweli, yanini kumsingizia mzee wa watu maswala yako yakijinga unayoyavuruga wewe mwenyewe? Jesca binti yangu kanitia aibu tena aibu ya mwaka na mimi kamwe staikubalia aibu hii initafune. Ninajua nitafanya nini na ulimwengu utaamini kuwa sina hatia, ndani ya familia yangu siishi na makahaba, siishi na watu waongo, siishi na watu wanafiki na mwana mpumbavu biblia inatueleza ni mzigo wa mamaye bali mwana mwenye hekima humfurahisha babaye najua mmeesha jua hili ni zigo la nani” alikaa kimya kidogo huku akirekebisha miwani yake.
“kuropoka ni jambo rahisi sana oooh! Gao jambazi, mwizi , sijui tapeli unaushahidi?”
“tusipende kuchafuana na kukosana na ndugu kwa sababu ya upuuzi wetu… wahenga walisema ukilikoroga lazima ulinywe.. yanini kusingizia watu ilihali wewe ndiye chanzo?”
“Jesca sasa utalazimika kutupa ushahidi wa hiki ulichokisema bila hivyo stakubali umudhalilishe mzee wa watu, na uzuri unanijua zaidi ni nini nitakiamua baada ya hapa mana uko ndani ya himaya yangu”
“Nina taka ushahidi la sivyo askari wataondoka na wewe hapa nahesabu mpaka tatu….. moja …….. mbili …….ta..
“ushahidi tunao Mh. Rais mimi ni Evarist Kimbo hata nisipojitambulisha unanijua vizuri mno” Mzee Gao na Mwanae macho yaliwatoka baada ya kumuona Kimbo akiingia akiwa hai maana hawakutarajia kabisa.
“Mimi ndiye niliyetumwa na Mzee Gao kwenda kumuuwa Jamae ili Von amuoe binti yako kwasababu Jesca alitaka kubadili mawazo baada ya kukutana na Jamae ambaye ndiye mpenzi wake wa siku zote, mimi ndiye niliyemteka Jamae na kukaa naye mateka zaidi ya wiki mbili kisha nilimuachia baada ya mzee Gao kushindwa kukamilisha makubaliano yetu, ukweli ni kwamba familia ya Gao ndiyo iliyo husika na kuchomwa kwa ofisi za Himaya Chapakazi wakishirikiana na aliyekuwa mkurugenzi msaidizi aliyejulikana kwa jina la Dominic Martine walifanya hivyo baada ya Domi kukomba pesa zote na walimlipa pesa zingine akatimukia nchini Urusi, ni familia ya Gao hii uliyonayo hapa na nashangaa unavyopambana kuwapa mwano, nayaongea haya mbele yako na mbele yao na niko tayari kwa lolote ikiwa ni pamoja na kutoa ushahidi popote nitakapohitajika, ninakumbukumbu za sauti za simu walizonipigia na simu zao zote na pia ujumbe wa maandishi.
Familia ya Gao imeyaharibu mno maisha yangu na siko tayari kuendelea kuona yanaharibika. Tafadhali familia ya Gao mwacheni Jamae hana kosa mtu wa watu, najua zisingekuwa juhudi zangu leo huyu kijana angekuwa ameesha kufa maana hapa ninavyoongea na wewe wameeshatumia kila njia kuhakikisha wanamteketeza lakini si yeye tu hata mimi wamejaribu kuniua asubuhi ya leo na pia mchana walitaka kumuua Jamae na bahati nzuri nilikuwa namlinda kwa karibu mno, kwa juhudi zangu nikamuokoa. Nalitafuta kosa lake silioni lakini wanataka kumuangamiza sidhani kama wivu wa mapenzi unaweza kuwa na athali kubwa kiasi hiki.
Familia ya Gao najua mko hapa achaneni na mnachokifanya Jamae hana hatia mmeharibu maisha yake vyakutosha sasa tuseme yatosha, kumbukeni mmemnyang’anya mpenzi wake kwa nguvu, mmemfilisi na sasa ni masikini wakutupwa bado haitoshi mnataka kumuua hii sasa ni laana.” Niliingia ukumbini pale huku nikisindikizwa na Wale askari watano tulikuja nao Jesca alifurahi mno hakuamini baada ya kuniona alinikimbilia na kunirukia kwa furaha huku akinikumbatia kwa nguvu na kuanza kupata denda.
Watu walipiga makofi, wengine walinuna lakini hatukuwa jali kila mtu na maisha yake na kila mtu na furaha yake tumefanikisha kulirudisha penzi letu. Jesca alinishika mkono tukatoka nje ya ukumbi huku Von na baba yake wakitutizama kwa ghadhabu na wasijue chakufanya. Tuliwaacha na suti zao sisi tukaingia zetu ndani sijui walichokiwaza ila mtoto nilikuwa nimejibebea kiulaini bila wasiwasi hapa sikuwa nawaza kitu kingine zaidi ya furaha kutoka kwa mpenzi wangu.
Nahisi Jesca amerudi mikononi mwangu na amedhihilisha upendo wakweli na msimamo wakweli katika mapenzi na sasa tuliingia ndani. Chumba chetu kiliimarishiwa ulinzi na Kimbo akiwa mkuu wa ulinzi kwa wakati huo si Rais wala mfanya kazi yeyote hakutakiwa kukisogelea pamoja na kuwa ndani ya Himaya ya Ikulu. Tulisikia ving’ora vya gari la polisi hapo nje na tulipochungulia tunawaona Gao na mwanae mikono ikiwa imepigwa pingu huku wakiwekwa kwenye gari la polisi na ndoa imeahirishwa.
Tulikumbatiana na kufurahi pamoja Jesca alikuwa na furaha sana kwani alinihakikishia kuwa ananipenda na sasa aliniambia kuwa ni mjamzito na ameesha hakikisha tunatarajia mtoto wa kiume, ilikuwa ni furaha mpya iliyoleta na kujenga tumaini jipya katika mapenzi na sasa tunakumbatiana tena na kupiga kelele kwa furaha huku tukibusu na kupongezana. Ni mapenzi ya dhati baina yetu sasa nayadumu milele ni mimi na malikia wangu wangu Jesca Manguli tumejipumzisha ndani ya jumba la Ikulu bila wasi wasi tukila na kunywa kwa upendo.
Part I inaishia hapo
Tukutane part II ujue kiliendelea nini
Asanteni
Baada yakufunga safari kutoka Mbezi beach nilikokuwanaishi na familia yangu niliamua kwenda kumtembelea rafiki yangu Goodluck Bembe rafiki yangu kipenzi sana, aliyehamia hivi karibuni maeneo ya Kibaha Maili moja sikuwahi kufika na pia sina mawasiliano yake ila kwa alivyo nielekeza naamini ninakumbukumbu yakutosha hivyo siwezi kupotea.
Ni majira ya jioni yapata saa kumi na moja nilikuwa tayari niko eneo la maili moja wilayani Kibaha, nageuka kushoto kwangu ninauona ubao mweupe ulioandikwa kwa mandishi ya buluu na mekundu kwakukolezwa yalisomeka hivi “Mkunguni High School” bila shaka ilikuwa ni shule ya Sekondari ya binafsi iliyokuwa mashughuli sana wilayani Kibaha na Dar es salaam kwa ujumla na alama hii ni moja ya alama nilizoelekezwa na mwenyeji wangu naamini nilikuwa karibu sana kumfukia alipo.
Kushoto kwangu kulikuwa na jumba moja la kifahari ambalo hakika sina mfano wake, ni jumba lililomvutia kila mpita njia, halikuwa jumba tu bali waweza kuliita hekalu kulingana na ukubwa wake lakini pia uzuri wa muonekano wake. Hakuna mpita njia ambaye aliizuia shingo yake na kuyanyima uhondo macho yake wakuliangalia jumba hili la kifahari lililokuwa sehemu hiyo. Kuitizama tu ile nyumba ilikuwa ni ufahari, niufahari pia kwenda kuwaeleza ndugu jamaa na marafiki kuwa kuna nyumba nzuri na yakifahari katika eneo Fulani ambayo niyakwanza kukutana nayo katika taifa hili masikini. “Dar wanajenga ila kibaha aaah! wanajenga zaidi.” Nilijisemea kimoyo moyo.
Ilinilazimu kuegesha gari maana sasa sikuwa na namna, hakuna mpita njia aliye nishangaa maana ilikuwa ni jadi kwa eneo hili kukuta watu wamefurika wakiliangalia jengo hili lisilo na gorofa hata moja ila ni kivutio kikubwa kwa wapiti njia. Katika akili yangu nilijuaa wazi jengo lile ilikuwa ni hoteli wala sikuwa na shaka nikamuuliza jamaa mmoja wa makamo mpita njia mwenzangu.
“samahani kaka hii hoteli inaitwaje kaka?”
“hoteli?.. hoteli ipi unayohoji?
“si hii kaka?... “
“Au unamaanisha hii nyumba?”
“ndiyo…. Hii nyumba”
“nyumba ya mtu hiyo kaka, siyo hoteli ni nyumba yakuishi kaka”
“una maanisha kuna mtu anaishi kwenye hili jumba lakifahari?”
“bila shaka hujakosea. Watu wanapesa zao bwana”
“humu wanaishi watu?”
“kaka eeh! Unataka waishi punda siyo?, umeuliza MASWALI nimejibu sasa maswali mia nane yanini…..” Bila shaka maswali yangu yalikuwa yememkera jamaa alikuwa ameesha kasirika …. yule! alitokomea huku akinung’unika na maneno sikuyasikia.
Ukuta ulionakishiwa na rangi pamoja na maumbo ya kufinyanga yenye michoro ya wanyama mbalimbali mashughuli duniani, unakwenda kukutana na geti la rangi ya dhahabu lililokuwa na mvuto usioelezeka, ni geti lakuvutia ambalo kwa kuliangalia tu halikuwa geti lakawaida kuwahi kuliona katika taifa hili, mimi nimtembezi ila hili geti hapana sina chakusema maana lilikuwa nijipya katika upeo wa macho yangu na kumbukumbu zangu zilinielez wazi ndo kwanza nakutana nalo.
Bustani nzuri iliyotiririka maji kama chemichemi ya asili iliyojengwa kwa majabali ilionekana kupitia sehemu,mbalimbali za uwazi pembezoni mwa ukuta ule wa lile jengo huku sehemu hizo zikizibwa na nondo ngumu ila ziliruhusu kuona. Kibwawa kikubwa kilicho nakishiwa kwa vigae na marumaru pembezoni kiliifanya hiyo sehemu kuvutia zaidi. Mita kama hamsini toka bwawa lilipo ilionekana nyumba ya kifahali iliyojengwa mjengo wakimagharibi, iliezekwa kwa vigae vya kijani kwa mitindo yakuvutia, madirisha yake ya vioo yalionekana mwanana huku mbele ikipambwa na bustani nzuri ya majani ya ukoka yaliyohifadhiwa vizuri ili kuongeza mvuto.
Muonekano ule ulinifanya nisogee nikitamani kujua zaidi niliposogea nililiona eneo kubwa la wazi lililozungushiwa ukuta kushoto mwa lile bwawa niliona kuna sehemu iliyojengwa kiasili namaanisha iliezekwa kwa majani lakini ilipambwa na kuvutia na kulipangwa vinywaji vya kila aina. Nje kulipaki magari ya bei ghali kama vile Mercedes Benz, Hummer, Jeep nakadharika, hali iliyozidi kunikata nguvu. Macho yangu sasa yalitamani kushuhudia zaidi maana nilivutiwa zaidi nahii nyumba lakini pindi nageuza jicho mkono wakulia nilikutana na mashine zitumikazo kwenye sheli zamafuta zilikuwa na nembo ya kampumi kubwa ya mafuta hapa nchini GBP.
Hamaki iliongezeka na nikataka kuupata ukweli wakati nazidi kuzungusha macho nilikutana na mandishi yaliyokuwa yameandikwa kwa rangi nyeupe “Barclays Bank ATM 24hours” yakiwa na maana ya mashine yakutolea fedha ya benki ya Barclays inafanya kazi masaa 24.”bila shaka mwenye hii nyumba siyo mtanzania ….. siyo mtanzania!” Nilijisemea huku nikishusha pumzi ndefu. Hakuna mtanzania mwenye fedha kiasi hiki, toka nizaliwe sijawahi kuona mtanzania wa dizaini hii, fedha mpaka zakuweka sheli nyumbani kwake hapana hii ni zaidi ya kukufuru, lakini vipi kuhusu ATM mashine… hili sidhani hata sheria za nchi kama zinakubali.
Sasa nilishapoteza uelekeo kwanza sikumbuki nilifuata nini huko maili moja, nilikuwa nanung’unika mwenyewe huku nikitembea kurudi lilipo gari langu. Nilifungua mlango na kuubamiza kwa hasira niliiwasha kwa hasira na kuondoka zangu. Yanini kuwa na mali kiasi hiki huku watu wanakufa njaa, yanini kumiliki fedha mpaka zikakufanya mwendawazimu?, yanini! Manung’uniko haya hayakuishia moyoni tu bali yalijidhilisha wazi usoni kwangu, sikupendezwa na hali hii iliniumiza na iliendelea kunitesa ndani ya moyo wangu.
Sijui ni wivu, chuki au maumivu tu sikukubaliana kabisa na utaratibu alioutumia yule sijui bwana/bibi katika uwekezaji wa pesa yake. “hata kama unafedha kiasi gani huwezi… huwezi kuustajabisha ulimwengu kwakujifanya wewe ndiye fahari waajabu katika huu ulimwengu. Sidhani kama hata tajiri namba moja wadunia amewahi kuwaza kufanya ujinga kama huu.
Nilipokelewa na mke wangu kipenzi baada ya kufika nyumbani akiwa mwenye furaha nilijitahidi kuificha hudhuni niliyokuwa nayo maana haikumhusu, ingawa nilijua roho inaniuma balaa sikujua kwanini niliumia vile yule jamaa kuwa na nyumba nzuri, sikuiona sababu lakini niliumia sana, pamoja na kujaribu kuikwepa hali ile lakini sikufanikiwa. Jesca mke wangu kipenzi alinikaribisha ndani nikaketi na pembeni kulikuwa na kitanda kidogo kilichokuwa kimembeba mwanangu kipenzi Eric Jamae akiwa na miezi miwili tu tangu amezaliwa nilikisogelea na kumkuta akichezesha mikono nilimbusu na kumpapasa kisha nikaingia zangu bafuni kulipunguza joto na kujaribu kukituliza kichwa kilichokuwa na lundo la mawazo kwa maji ya baribi.
Baada ya kupata maji nilibadili nguo na kumfuata Jesca alikuwa jikoni akihangaika kuandaa chakula, nilifika na kuanza kumtania kidogo tulicheka nilijaribu kumsaidia lakini hakukubali alikataa kabisa akaniomba nikapumzike. Mke wangu hakupenda kuniona namsaidia kazi za jikoni ingawa mimi nilipenda sana kufanya hivyo. Haijalishi alitoka familia gani ila Jesca alipenda kuishi katika uhalisia aliamini jiko ni mahali pa mwanamke.
Na alipokuwa jikoni aliamini yuko sehemu sahihi. Niliondoka zangu na kwenda kujipumzisha sebuleni. Niliketi Tv ilikuwa ikiendelea na vipindi vyake ambavyo havikunivutia lakini sikuhangaika hata kubadili stationi maana nilijua nitapoteza muda wangu bure. Picha iliyokuwa ukutani ni picha ya Jamae Justine na Jesca Manguli vijana waliopitia mikikimiki mingi mpaka kuya vaa mavazi waliyokuwa nayo hapo pichani. Ni picha ya ndoa kati yangu na Jesca ndoa iliyopitia vikwazo vingi lakini ilifungwa.
********
ITAENDELEA
BURE SERIES