dah!
hii wizara mikataba yote inayoingia ni majanga.
huu mkataba wa milioni 500 kwa mwez hauna tofauti na ule wa sh. 3 kwa sh. 97.
umeme mwez mzima mikoa mitano kwa mil. 500? halafu huyo m***ge anasema kwa kujidai na huku watanganyika tunakamuliwa paye na vat madukani.
cjui nani katuroga watanganyika
Ukitaka kujua kuwa tumerogwa soma hii hapa, halafu nikunyambulie kidogo
The Zanzibar Electricity Company (ZECO) General Manager Mr Hassan Ali Mbarouk said his office had received a letter from TANESCO demanding the settlement of 70bn/= debt, threatening to cutoff power to Zanzibar.
"I do not know why TANESCO uses the press to give false information with regard to the power debt in Zanzibar.
We owe them about 44bn/- and we recently agreed to pay the debt on monthly installments," ZECO manager said."
ZECO and TANESCO Boards of Directors have met to discuss this debt, agreeing to settle it gradually on monthly basis. But Zanzibar government has asked the union government to pay 18bn/- accumulated from Pay As You Earn (PAYE) in 2011."
The manager said that the union government has been asked to settle the PAYE debt by paying directly to TANESCO to reduce Zanzibar's electricity debt of 44bn/-, not 70bn/-.
"He said that Zanzibar government has agreed with the union government on how to share the PAYE from the union government civil servants working in Zanzibar. TANESCO supplies 60 megawatts in Zanzibar generated from the national grid.On average, Zanzibar is supposed to pay 3.4bn/- on monthly basis. By ISSA YUSSUF, Tanzania Daily News
Kwanza anayetoa habari hii ni meneja wa ZECO.
Meneja anasema deni ni bilioni 44 ingawa waliotoa umeme wanasema ni bilioni 70.
Kumbukumbu zote zinaonyesha kuwa deni la zanzibar kwa uchache si chini ya bilioni 60.
Wale wanaosema haidaiwi watueleza lini znz imeweza kulipa hizo bilioni 44 anazosema meneja wa ZECO?
Kwa hesabu za haraka haraka, mapato ya znz ni bilioni 400.
Kiasi cha kadiri ya bilioni 50 ni sawa na 1/8 ya mapato au zaidi ya asilimia 11 ya mapato yao.
Hapo chini inaonyesha, na meneja kathibitisha kuwa walikuwa walipe kwa installment.
Kiasi kilichokubaliwa ni bilini 3.5 kwa mwezi, wao wanalipa flat rate ya milioni 500.
Wanasema ilikuwabaliwa kuwa PAYE ilipie kiasi cha bilioni 18. PAYE ya mwaka huu kulingana na waziri wa fedha i bilioni 15. Yaani znz wamepewa bilioni 15 kama kodi ya wafanyakazi wa muungano.
Ile PAYE ya JMT ndiyo inatumika kuhudumia muungano ikiwa ni pamoja na kulipa bilioni 18 walizoomba.
Hapo wana sababu kwavile ni JMT na hivyo wanaweza kuchota chochote. Kwa bahati mbaya ile bilioni 15 kwa mujibu wa Nkuya inakwenda SMZ na haiwezi kulipa deni lolote la Tanganyika. Hii maana yake ni kuwa cha Tanganyika ni chetu, chao ni chao.
Lakini pia tujiulize,kwanini wapewe PAYE? Hivi si wana asilimia 21 ya ajira za muungano.
Yaani tunawalipa ili wamalize tatizo la unemployment.
Nje ya muungano znz haina uwezo wa kuajiri kiwango cha asilimia 21 ya sasa ya wafanyakazi wa muungano.
Hao wa SMZ haiwezi kuwalipa, hawa wa muungano wanalipwa na nani?
Ndipo inakuja hoja kuwa kila wanapotaka free ride wanakimbilia JMT. Ni hao hao hawatambui JMT na hata kudharau katiba ya JMT.
Tatizo si kulogwa, ni kuwa Tanganyika haionekani. Hakuna mtu wa kusimamia masilahi ya Tanganyika.
Tanganyika imekuwa shamba la bibi kila mwenye njaa anaingia kujichukulia.
Fikiria hivi, wznz walitaka wajumbe sawa wa tume. Wakati wa malipo wakasema hilo ni suala la JMT. Yaani ile PAYE yako ndiyo inafanya kazi hadi kwao. Ile ya kwao inabaki huko huko. Kiingilio walicholipa ni ZAN na kutaka usawa.
Hebu tafakari kuwa wale wabunge 81 wanalipwa na PAYE yako. Hawana masilahi yoyote na Tanganyika, uwepo wao ni kwa ajili ya znz. Kwanini kama wanapata PAYE ya muungano wasibebe zigo la kuhudumia wabunge wao?
Hili la bunge la katiba ndilo kidogo limeanza kuonyesha hasira za Watanganyika. ZNZ imelazimika kuwalipia wabunge wake kuokana na kiburi walichoonyesha kulipia gharama za tume ya Warioba.
Wengine tunashindwa kuelewa, kwanini hamuoni tatizo hilo. Hakuna njia ya kuzuia wizi na ukupe wa znz bila kuwepo Tanganyika. Ukisema Tanzania kitu cha kwanza wanaleta bakuli lenye nembo ya ZAN watiliwe.
Hawana mchango wowote katika chungu iSIpokuwa herufi za ZAN
Kwa minajili hiyo, deni la bilioni 18 linafidiwa na wewe na mimi kwa kulipa umeme zaidi wa kwenda visiwani wasikotutambua.
Hayo yakitokea wao wameshaondoa gesi na mafuta.
Tena kwa jeuri ZECO imelamba bilioni 20 kwa ufisadi. Well, SMZ imeachia tu wale kwasababu mjomba Tanganyika atalipa.
Nasi tunasema hewala. Hatuwezi kujinasua hadi pale Tanganyika itakapoonekana na kusimamia rasilimali zake.
Kwa mwendo wa sasa ukisema TANZANIA, wanakuja na bakuli la ZAN, utawahoji vipi? Ndizo hizo bilioni 18 unatakiwa lipe wewe Mtanganyika kwa umeme usioutumia.
Ukumbuke pia wanakomba 4.5 ambayo tunajua Mkapa aliipandisha hadi 7 kwa pato la taifa. Pato la taifa ni la Tanganyika kwasababu lao wenyewe haliwezi kuwapa 4.5 wanayosema.
Mbali ya hayo nakisi ya bajeti yao inatoka JMT.
Ukitaka kuona vituko, mwaka jana 2013/14 ofisi ya makamu wa rais ilipewa bilioni 32 kwenda znz zisizo na sababu. Kwa mwendo huo, wanauwezo wa kulipa deni la umeme kwa kodi yako. Wanachukua na mkono wa kulia wanakurudishia na wa kushoto wakisema wamechanga.
Hapo ndipo Watanganyika wanatakiwa waone. Katika kuficha ukweli wznz ni wazuri sana wa vinywa. Leo wanasema Maswi kasema, hawakubali ya meneja wao wa ZECO. Ukitaka kumpendeza mznz mwambie habari njem tu, ukimwambia ukweli mtakaosana sana.
Kupe yupo mgongoni ananyonya damu kwa raha zake.