Komeo
JF-Expert Member
- May 3, 2011
- 2,498
- 1,172
"Kwanza niwaambie (waandishi wa habari),deni hili ni la zamani sana ila ,SMZ imekuwa ikilipa kila mwezi na hata hivi sasa tumepokea shilingi milioni 500 za malipo ya umeme kwa Zanzibar tu," alisema.
"Nawaambia mkawaambie wote wanaosema kwamba Zanzibar inadaiwa na TANESCO kuwa huo ni uongo na kama mtu hajafanya utafiti hana haki ya kuzungumza," alisema.
Chanzo: Zanzinews[/QUOTE]
Kwa kauli hizi za Maswi ndio zimeleta mkanganyiko zaidi kwa sababu hizi:-
- Amethibitisha kuwa Zanzibar inadaiwa na Tanesco deni hilo la Bilioni hizo 47 pale anaposema "deni hili ni la zamani sana".
- Amethibitisha kuwa Zanzibar wanailipa Tanesco Mil 500 kila mwezi bila kufafanua kama hayo ndio matumizi ya umeme Znz au wanapunguza deni hilo la zamani (Bil.47) wanalodaiwa.
- Anasema mkawaambie wanaosema Znz inadaiwa na Tanesco ni uongo, lakini hasemi hilo deni aliloliita la zamani (Bil.47) limelipwaje.
FULL KUJICHANGANYA!
Alipaswa kujibu hoja hizi kitaalam kwa cheo chake cha Katibu Mkuu, bila kumfikiria Mh. Kafulila.
Ingefaa aende mbele kidogo kwa kueleza Tanesco wanalipa shilingi ngapi kila mwezi kwa IPTL, AGREKO, SYMBION, na SONGAS nikitaja "virusi" vichache vya Tanesco.