ZECO yailipa TANESCO 500m/- kila mwezi


"Kwanza niwaambie (waandishi wa habari),deni hili ni la zamani sana ila ,SMZ imekuwa ikilipa kila mwezi na hata hivi sasa tumepokea shilingi milioni 500 za malipo ya umeme kwa Zanzibar tu," alisema.

"Nawaambia mkawaambie wote wanaosema kwamba Zanzibar inadaiwa na TANESCO kuwa huo ni uongo na kama mtu hajafanya utafiti hana haki ya kuzungumza," alisema.
Chanzo: Zanzinews[/QUOTE]

Kwa kauli hizi za Maswi ndio zimeleta mkanganyiko zaidi kwa sababu hizi:-
- Amethibitisha kuwa Zanzibar inadaiwa na Tanesco deni hilo la Bilioni hizo 47 pale anaposema "deni hili ni la zamani sana".
- Amethibitisha kuwa Zanzibar wanailipa Tanesco Mil 500 kila mwezi bila kufafanua kama hayo ndio matumizi ya umeme Znz au wanapunguza deni hilo la zamani (Bil.47) wanalodaiwa.
- Anasema mkawaambie wanaosema Znz inadaiwa na Tanesco ni uongo, lakini hasemi hilo deni aliloliita la zamani (Bil.47) limelipwaje.
FULL KUJICHANGANYA!
Alipaswa kujibu hoja hizi kitaalam kwa cheo chake cha Katibu Mkuu, bila kumfikiria Mh. Kafulila.
Ingefaa aende mbele kidogo kwa kueleza Tanesco wanalipa shilingi ngapi kila mwezi kwa IPTL, AGREKO, SYMBION, na SONGAS nikitaja "virusi" vichache vya Tanesco.
 

Tabu ya nchi hii hatuna Waandishi wa Habari, bali tunao Maripota (Reporters) na Wahandisi wa Habari tu, ambao hawashirikishi vichwa vyao hata kidogo. Kazi yao ni kukimbizana na bahasha za kaki tu kwenye makongamano, semina, warsha na press conference kama hii ya Maswi.
 
Maswi uliye m-quote anafanya kazi Tanesco. teh teh teh
 
Maswi uliye m-quote anafanya kazi Tanesco. teh teh teh

Nguruvi3,

hata ukijitoa fahamu basi leo mpaka zitakurudia hizo fahamu zako,

Hebu msome maswi hapa

" KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, Eliakim Maswi, amekanusha tuhuma za Shirika la Umeme (TANESCO) kwamba linaidai Zanzibar kiasi cha shilingi bilioni 47 kutokana na matumizi ya umeme.

Alisema wamekuwa wakipokea shilingi milioni 500 kila mwezi kutoka Shirika la Umeme Zanzibar, ikiwa ni malipo ya umeme unaotumiwa Zanzibar.
'"


Nafikiri hapa utajua kuwa Maswi amesema wazi kuwa TANESCO ndio wanaowadai Znz na Sio Wizara ya Nishati ya Muungano. Kumbuka kuwa Tanesco ipo chini ya Wizara ya Nishati na maswi ndio katibu mkuu wa wa WIZARA HIYO. HATA HILI ULIJUI KWELI AU NDIO KUJITOA UFAHAMU?

Sasa suala langu kwako unaposema Znz ichangia pesa wizara ya mambo ya ndani au wizara ya mambo ya nje au ilmu ya juu na nyingine ulizobainisha. NDIO NIKAKUULIZA WACHANGIE PESA HIZO KWA NANI, NA KWA ACCOUNT GANI? NA NANI ANAYEDHIBITI ACCOUNT HIYO? lakin kubwa hapa je kuna makubaliano yoyote ya kisharia kuwa Znz wachangie hizo Wizara? na kama yapo wachangie kupitia account ipi? na nani msimamizi wa hiyo account ambaye atakuwa na mandate ya kuandika invoice kwa Znz?


Tunakuomba MAJIBU yako hapo.
 
Nimekuambia account hiyo inachangiwa nini na nani? Pili, Mwaka 2013/2014 znz ilipewa bilioni 32 tu, nani amezikagua na zimetumika vipi.

Kama hakuna makubaliano inkuwaje hapo juu umesema wizara ya ulinzi wa znz inachangiwa na JMT.
Wapi JMT inapoanzia na wapi inapoishia.

Tatu, account ya pamoja ni kati ya nani na nani?

Nne, Account hiyo inachangiwaje ikiwa znz haina uwezo wa kuendesha account hiyo kwa wiki 2. I mean account ya pamoja inapaswa kuhudumia JMT. Sasa mishahara ya wafanyakazi wa JMT ni bilioni 360 yaani mapato ya znz ya mwaka mzima bila. Hiyo account unatgemea iwe na pesa za nani. Just think about it.

Kuendesha wizara ya ulinzi na usalama kwa mwaka 1.2 trillion, znz inahitaji makusanyo ya miaka mitatu. Account hiyo znz itachangia nini yarabi. Hebu ona aibu kidogo mkuu, hata wewe, tutauliza Warabai na wavuvi wapoje?
 
CCM wa bara akiwemo Ali Kessy wanasema umeme wa bara kwenda Zanzibar ni faida za muungano kwamba Zanzibar wanatumia umeme wa bure muungano udumu, Kumbe Zanzibar inalipia umeme ghali kuliko ata hao watanganyika wenyewe.

Tanganyika ndio tegemezi kwa Zanzibar ndo mana wanangangania muungano, TRA inakusanya kodi za wazanzibari kila siku ili Tanganyika waweze kutimiza milo 3 kwa siku. Ni aibu nchi kubwa Tanganyika inaitegemea nchi ndogo ya Zanzibar kwa kila kitu
 

Nguruvi3

Suala lako la nne naomba nikujibu kama ifuatavyo.
Hivi itawezekana vipi nchi yenye watu 1.5 Mil watoe pesa za kuwalinda watu zaidi ya 45 Bil,
Hivi nchi yenye ardhwi ya 2000 sq Km itoe ulinzi kwa nchi yenye ardhwi 885,800 Sq Km.
Je huoni kuwa ni dhulma sana kwa Znz hapo.

Lakin vile unaposema Znz haina uwezo wa kuchangia ...LABDA NIKUULIZE JE TANGANYIKA ANACHANGIA MUUNGANO WENU KATIKA ACCOUNT GANI? NA WANACHANGIA KIASI GANI? NA NANI MSIMAMIZI WA HIYO ACCOUNT ANAYEWEZA THIBITISHA KUWA TGK WAMECHANGIA?

Lakin kubwa hapa kama mliona Znz haina uwezo jiulize JE KWANINI NI NYERERE ALIYEFUNGA SAFARI KWENDA ZNZ KUOMBA WAUNGANE?

Nilikubainishia huko nyuma ASILAN ABADAN haiyumkiniki Znz na TGK kuchangia sawa kwa sawa katika huo Mvungano. Ni laazima iwekwe formula maalum kwa vigezo vya ukubwa wa nchi na idadi ya watu wa nchi wanachama wa mvungano huo, ili ijulikane kila mtu anatakiwa kuchangia kiasi gani, lakin kubwa pesa hizo wanazochangia laazima ziwe zinasimamiwa na nchi hizo wanachama katika kujua mapato yanayotokana na michango ya nchi hizo, misaada na mikopo na kujua mgawanyo wake kwa nchi hizo.

Je kwa akili yako unataka Znz wachangie pasu kwa pasu na Tgk katika huo mvungano? je unatumia kigezo gani?

Pole sana kwa kila wakti nakwambia UCHUMI NI TAALUMA NA SIO BLA BLA.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…