Zelensky amemjibu Trump kwamba alipokea dola bilioni 100 tu za msaada wa Marekani kama ruzuku, sio mkopo

Zelensky amemjibu Trump kwamba alipokea dola bilioni 100 tu za msaada wa Marekani kama ruzuku, sio mkopo

Marekani kashtuka baada ya kuona anatumia pesa nyingi bila Faida huku China ikiendelea kuimarika kiuchumi,hapo lazima hayo madini yatachukuliwa tena akijichanganya atauliwa
 
Kuna mlio bado hajatoa Zelensky kwa spana anazopigwa na Trump.
Ila sioni kama atakuwa madarakani in next three months.
Sio kuwa tu madarakani, nina wasiwasi anaweza asiwe hai pia.
Mtu kama Trump anamwambia hiyo dola bilioni mia ya wavuja jasho wa Marekani kwamba alikubaliana na Biden itoke kama msaada.
Huyu jamaa hawajui wamarekani maskini, hajui ni mashetani kiasi gani, wangeweza kuzungumza walau kama angekua amewashinda warusi vitani, ila hapa watamuua na hiyo pesa watazungumza na Urusi awabakizie maeneo ya Ukraine yenye mali arudishe gharama.
 
Wanaukimbi.

Zelensky anasema kwamba alipokea msaada wa dola bilioni 100 pekee kama ruzuku, sio mkopo.

"Hatutambui deni la Ukraine la dola bilioni 500 kwa Marekani.

Sitambui hata dola bilioni 100. Tulikubaliana na Biden kwamba ilikuwa ruzuku, sio deni."
===============
JUST IN: Zelensky says that he received only $100 billion in U.S. aid as grant, not a loan.

"We don't recognize Ukraine's $500 billion debt to the US.

I don't even recognize $100 billion. We agreed with Biden that it was a grant, not a debt.

View: https://x.com/megatron_ron/status/1893694220742832307?s=12&t=mTROWpaJUT8H393JMgWOvw

Mwamba sijui kama ana muda mrefu wa kuendelea kuliona jua.
 
Wameshapata mbadala wak,e hivyo wameanza kumchafua kwa wananchi.

Vizuri naye kajieleza, ingawa hatoshinda propaganda za Russian an marekani.
 
Vita mbaya sana. Dola bilioni moja zinaweza maliza kabisa kabisa njaa duniani.
Ni kweli kabisa! Duniani kuna takribani jumla ya watu bilioni 10. Sasa piga hesabu dola bilioni 500 zingegawiwa kwa idadi ya watu duniani kila mtu angepata dola ngapi? Jumlisha na za vita vingine vinavyotokea sehemu mbali mbali duniani.
 
Zele na Ukraine wote ni losers

Alitegemea atapata ulinzi kwa kuwa mwanachama wa NATO imeshindikana wamemkataa

Madini yatakayochimbwa yatakuwa na thamani zaidi ya hiyo misaada aliyopewa, Marekani itafadika zaidi kuliko Ukraine

Wakati huo Russia imeshachukua 20% ya ardhi ya Ukraine yenye utajiri wa madini na ardhi yenye rutuba katika uzalishaji wa ngano

Ukraine imeambulia kupoteza mamia ya maelfu ya askari, mamilioni ya Waukraine wamekimbia nchi yao, wamepoteza karibu 20% ya ardhi yao na uchumi na miundombinu mingi imeharibiwa
Hii sio mechi ya Simba na Yanga kwamba iandikwe kishabiki kirahisi rahisi hivi. Unavyoona Urusi ilikuwa ikisherehekea hii miaka mitatu ya “special operation”? - badala ya wiki tatu walizopanga mwanzoni?

NATO na Marekani wasingeingia kama Zelenskyy na wapiganaji wa Ukraine wasingeonyesha ujasiri na ushujaa wa kukabiliana na Urusi kama walivyofanya. Walitegemea mambo yatakuwa kama jinsi jeshi la Afghanistan lilivyotoweka mbele ya Taliban pamoja na kuachiwa mabilioni ya pesa, silaha na vifaa.

Wasingeweza kutoa msaada wa wapiganaji kuilinda Ukraine.

Show some respect to Zelenskyy and the gallant Ukrainian fighters AND keep watching this space uone kitakachotokea mwishowe. Hizo tabiri za kishabiki zibakie huku uswahilini tu.
 
Kuna mlio bado hajatoa Zelensky kwa spana anazopigwa na Trump.
Ila sioni kama atakuwa madarakani in next three months.
Ila Trump ni kigeugeu pia ni katapeli fulani.
Kama kweli utawala uliopita ulimpatia hicho kiasi kama grant kwanini amgeuke na anadai ni mkopo. Ambane tu kuanzia sasa si kuleta ulaghai kwa kugeuza mambo.
Nasikia na starlink wanaenda kuwazimia internet pia.
Zelensky siku zake ziko numbered na bila shaka kitakachofuata ataanza kutuhumiwa kwa kutumia vibaya pesa ya misaada kwa kujinufaisha.
 
Mkuu ni Urusi au ni Putin binafsi unayempenda kiasi hicho?

Manake si kawaida na rahisi kwa kiongozi wa nchi tena ya kidemokrasia kukabidhi nchi yake na rasilimali zake kwa nchi nyingine. Ni ajabu sana hata kufikiria hivyo.
Mkuu, assume wewe ni raisi wa Zanzibar, umeitenga Zanzibar na Tanganyika. Kipi ni rahisi kwako, kumpa Kenya madini yako ili muwe washirika against Tanganyika au kurudi na kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar?
 
Ila Trump ni kigeugeu pia ni katapeli fulani.
Kama kweli utawala uliopita ulimpatia hicho kiasi kama grant kwanini amgeuke na anadai ni mkopo. Ambane tu kuanzia sasa si kuleta ulaghai kwa kugeuza mambo.
Nasikia na starlink wanaenda kuwazimia internet pia.
Zelensky siku zake ziko numbered na bila shaka kitakachofuata ataanza kutuhumiwa kwa kutumia vibaya pesa ya misaada kwa kujinufaisha.
Zelensky wananchi ndo walimuweka madarakani na sio trump
 
Sio kuwa tu madarakani, nina wasiwasi anaweza asiwe hai pia.
Mtu kama Trump anamwambia hiyo dola bilioni mia ya wavuja jasho wa Marekani kwamba alikubaliana na Biden itoke kama msaada.
Huyu jamaa hawajui wamarekani maskini, hajui ni mashetani kiasi gani, wangeweza kuzungumza walau kama angekua amewashinda warusi vitani, ila hapa watamuua na hiyo pesa watazungumza na Urusi awabakizie maeneo ya Ukraine yenye mali arudishe gharama.
Kama ulikuwa hujui putin kabla hata ya vita ameshajaribu mara nyingi sana kumuua zelensky na kashindwa mambo sio marahisi kama kukaa nyuma ya keyboard na kuandika
 
Putin alikuwa anasema eti kisa muda wa uchaguzi umepita, hivyo zelensky si rais halali so naona trump anaunga mkono. Lakini wanajitoa ufahamu kama vile hawajui kuwa ukraine inaongozwa kwa martial law kwa sababu ya vita
Sikuwahi tegemea kuna siku putin ataomba mbeleko baada ya mambo kuwa magumu tena kwa adui wake marekani maisha yanaenda kasi sana
 
Sikuwahi tegemea kuna siku putin ataomba mbeleko baada ya mambo kuwa magumu tena kwa adui wake marekani maisha yanaenda kasi sana
Putin na trump wanaongea lugha moja. Huoni wamewatenga kuanzia ulaya na ukraine mwenyewe wakafanya mkutano wa vita huku wahusika wengine wakiwa hawapo. Bado anataka kumwondolea vikwazo putin.
Watu wanadai trump anataka kuitenganisha russua na china.
 
Russia - China ni dude baya kwa USA/ Europe
 
Back
Top Bottom