Zelensky: Ni bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi umempigia mtu magoti

Matteo Vargas

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2019
Posts
803
Reaction score
1,329
Hii ni kauli ambayo raisi wa Ukraine ameiishi pale White House mbele ya Donald Trump ambayo ilitolewa na mwana mapinduzi na mwanaharakati Dolores Ibarruri huko Spain miaka ya 1936 chini ya utawala wa mkono wa chuma wa dikteta Franco.

Alichofanya Zelensky mbele ya Trump na makamo wake JD Vance ndio nimeamini pasipo chembe ya shaka kuwa wazungu sio wanafiki na sio machawa wanasimamia kile wanachokiamini bila kujali wewe ni nani na hawapepesi macho kukwambia ukweli kama unajaribu kuupindisha.

Trump anataka madini ya Ukraine pasipo na hakikisho kamili la usalama kwa Ukraine lakini hapo hapo anafanya vikao vya siri na Russia hakuna mzalendo anayeweza kukubali hiki kitu labda kama anataka kuuza nchi yake na tunajua mambo haya huwa yanatokea wapi lakini Zelensky kasema hata kama anapambana na nchi zenye mabavu lakini nchi yake haiuzwi.

Ni bora wafe wakiwa wanapigana not otherwise.
 
Nilikuwa najua kusutana ni tabia za wanawake wa kiswahili tena wa uswazi.

Mpaka pale nilipoona Ikulu ya Marekani imemuweka Zelensky mtu kati na kuanza kumsuta.

Tangu jamaa anapokelewa kulikuwa na viashiria vingi vilivyotosha kupima kitachoenda kujadiliwa.

Hakupokelewa vizuri, walianza kumfanyia dhihaka kuhusu mavazi yake kitu ambacho hakikutakiwa kuwa big issue kwa nchi kama Marekani ambayo ina amini sana kwenye uhuru binafsi wa mtu.

Lakini pia kum crash kila wakati anapokuwa anataka kutoa ufafanuzi au kuelezea jambo ilionesha pia kuwa mazungumzo ya jana yalikuwa yamepangwa yafanyike vile au pengine zaidi ila kutokana na Zelensky kuto paniki ikabidi iishie vile.
 
Zelensky angetakiwa pia amkubushe JD Vance kuwa Alisha sapoti misimamo ya hilter wazi wazi na akaja kuomba msamaha Hivyo haoni tabu kwa yeye kum sapoti Putin.

Ila nimependa msimamo wa raisi wa Ukraine waafrika tuige mfano
 
Hii ni kauli ambayo raisi wa Ukraine ameiishi pale White House mbele ya Donald Trump ambayo ilitolewa na mwana mapinduzi na mwanaharakati Dolores Ibarruri huko Spain miaka ya 1936 chini ya utawala wa mkono wa chuma wa dikteta Franco.

Alichofanya Zelensky mbele ya Trump na makamo wake ndio nimeamini pasipo chembe ya shaka kuwa wazungu sio wanafiki na sio machawa wanasimamia kile wanachokiamini bila kujali wewe ni nani na hawapepesi macho kukwambia ukweli kama unajaribu kuupindisha.

Trump anataka madini ya Ukraine pasipo na hakikisho kamili la usalama kwa Ukraine lakini hapo hapo anafanya vikao vya siri na Russia hakuna mzalendo anayeweza kukubali hiki kitu labda kama anataka kuuza nchi yake na tunajua mambo haya huwa yanatokea wapi lakini Zelensky kasema hata kama anapambana na nchi zenye mabavu lakini nchi yake haiuzwi.

Ni bora wafe wakiwa wanapigana not otherwise.
LAKINI SASA mbona na yeye ANAKUWA haelewani na KILA MTU NA misimamo yake haitabiriki? YEYE haoni KAMA raia wanakufa NCHINI KWAKE? Hilo halimuumi?
 
Zelesky ameonesha kipimo Cha uzalendo kwa nchi yake, viongozi wenye misimamo kama hiyo duniani ni wachache sana! "Kwamba pamoja na umaskini wangu siwezi kuwa mtu wa ndio mzee kwa Kila jambo"

Nashindwa kupata picha ingekuwa ni Hawa viongozi wetu sijui kingetokea Nini😅 kwa ile mtu kati naamini wangejikojolea kwa hofu na uoga.

Trump sio mtu wa kuheshimu viongozi wenzake,huwezi kutaka kumdhalilisha vile kiongozi wa nchi eti kisa una power!! Big no! Hongera sana zelesky
 
Inaonekana sasa kawajua nia yao ilikuwa nin wakati wanamuingiza kwenye vita.

Ni muda muafaka kwake kumalizana na Putin kiume, kama ndugu, kama majirani
Na Putin akiipata Ukraine kwa zile raslimali itakuwa tajiri kuliko na Putin anamezea mate kile Trump anachokitaka lakin NATO na Biden walizuia hilo lakin mzee wa madili Trump anazitaka
 
Hii ni kauli ambayo raisi wa Ukraine ameiishi pale White House mbele ya Donald Trump ambayo ilitolewa na mwana mapinduzi na mwanaharakati Dolores Ibarruri huko Spain miaka ya 1936 chini ya utawala wa mkono wa chuma wa dikteta Franco.

Alichofanya Zelensky mbele ya Trump na makamo wake JD Vance ndio nimeamini pasipo chembe ya shaka kuwa wazungu sio wanafiki na sio machawa wanasimamia kile wanachokiamini bila kujali wewe ni nani na hawapepesi macho kukwambia ukweli kama unajaribu kuupindisha.

Trump anataka madini ya Ukraine pasipo na hakikisho kamili la usalama kwa Ukraine lakini hapo hapo anafanya vikao vya siri na Russia hakuna mzalendo anayeweza kukubali hiki kitu labda kama anataka kuuza nchi yake na tunajua mambo haya huwa yanatokea wapi lakini Zelensky kasema hata kama anapambana na nchi zenye mabavu lakini nchi yake haiuzwi.

Ni bora wafe wakiwa wanapigana not otherwise.
1740861445582.jpeg
 
Back
Top Bottom