Zelensky: Ni bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi umempigia mtu magoti

Zelensky: Ni bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi umempigia mtu magoti

WhatsApp Image 2025-03-01 at 02.35.09.jpeg
 
Ukraine ni kama mtu aliyefuga mbwa Kwa kutegemea kinyesi Cha mlevi wale waliomhamasisha kupigana hawampi tena misaada hapo ndio utaelewa siasa za misaada hawatoi bure wanasababisha vita ili wakuuzie silaha wachukue rasilimali
Wakina nani hao walioanzisha vita and how??
 
Urusi ilitoa ofa ya kukaa mezani na Ukraine au bunduki ndio zitoe suluhisho.
Hata wew ungekuwa Zelensky ofa hizo hazibebeki. Ni ngumu sana nchi itaanguka ndio maana jamaa kaona ni bora nchi ianguke akiwa anapigana kuliko kuiachia kirahisi anajua Kuna vizazi kwa miaka mingine mingi vinakuja Hivyo anaweka Alama kwamba japo tulishindwa lakini tulijaribu
 
Zelensky angetakiwa pia amkubushe JD Vance kuwa Alisha sapoti misimamo ya hilter wazi wazi na akaja kuomba msamaha Hivyo haoni tabu kwa yeye kum sapoti Putin.

Ila nimependa msimamo wa raisi wa Ukraine waafrika tuige mfano
JD ndio muanzilishi wa ulemkutano kuharibika kiasikile, ukimsimiliza utaona anavyo jipendekeza kwa Tramp kichawachawa.

Mpaka anamkumbusha Zelensk maneno aliyoongea Penslovania kipindi cha campeni zauchaguzi kitu ambacho hakikuwa na maana yoyote.



Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Hii ni kauli ambayo raisi wa Ukraine ameiishi pale White House mbele ya Donald Trump ambayo ilitolewa na mwana mapinduzi na mwanaharakati Dolores Ibarruri huko Spain miaka ya 1936 chini ya utawala wa mkono wa chuma wa dikteta Franco.

Alichofanya Zelensky mbele ya Trump na makamo wake JD Vance ndio nimeamini pasipo chembe ya shaka kuwa wazungu sio wanafiki na sio machawa wanasimamia kile wanachokiamini bila kujali wewe ni nani na hawapepesi macho kukwambia ukweli kama unajaribu kuupindisha.

Trump anataka madini ya Ukraine pasipo na hakikisho kamili la usalama kwa Ukraine lakini hapo hapo anafanya vikao vya siri na Russia hakuna mzalendo anayeweza kukubali hiki kitu labda kama anataka kuuza nchi yake na tunajua mambo haya huwa yanatokea wapi lakini Zelensky kasema hata kama anapambana na nchi zenye mabavu lakini nchi yake haiuzwi.

Ni bora wafe wakiwa wanapigana not otherwise.
Trump Hana regac za uongozi sijui watu wa USA wanafikiria nini ??
 
Nilikuwa najua kusutana ni tabia za wanawake wa kiswahili tena wa uswazi.

Mpaka pale nilipoona Ikulu ya Marekani imemuweka Zelensky mtu kati na kuanza kumsuta.

Tangu jamaa anapokelewa kulikuwa na viashiria vingi vilivyotosha kupima kitachoenda kujadiliwa.

Hakupokelewa vizuri, walianza kumfanyia dhihaka kuhusu mavazi yake kitu ambacho hakikutakiwa kuwa big issue kwa nchi kama Marekani ambayo ina amini sana kwenye uhuru binafsi wa mtu.

Lakini pia kum crash kila wakati anapokuwa anataka kutoa ufafanuzi au kuelezea jambo ilionesha pia kuwa mazungumzo ya jana yalikuwa yamepangwa yafanyike vile au pengine zaidi ila kutokana na Zelensky kuto paniki ikabidi iishie vile.
KWAHIYO ZELENSKY HAKUPANIKI?
 
JD ndio muanzilishi wa ulemkutano kuharibika kiasikile, ukimsimiliza utaona anavyo jipendekeza kwa Tramp kichawachawa.

Mpaka anamkumbusha Zelensk maneno aliyoongea Penslovania kipindi cha campeni zauchaguzi kitu ambacho hakikuwa na maana yoyote.



Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Ilionesha wazi JD na mwenzake wana chuki ya wazi wazi kisa tu jamaa kagoma kuwa mnyonge
 
Back
Top Bottom