Zelensky wa Ukraine alia tena, asifu ujasiri wa watu wake

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kwa mara nyingine Urusi imeendelea kupiga maeneo mbali mbali ya Ukraine ambapo jengo moja la ghorofa 9 limeporomoshwa huko Oblast ya Kherson.

Katika hotuba yake ya usiku wa jana raisi Zelensky wa Ukraine amesifu uzalendo wa wananchi wake ambao wameshiriki katika shughuli ya uokoaji wa wahanga wa shambulio hilo.

Katika hotuba hiyo hiyo amezihimiza nchi za magharibi za NATO kuleta mitambo ya kivita ambayo wameijaza kwenye maghala yao wakati askari wa Ukraine wanaisubiri walipize kisasi.

Kwa upande wake waziri mkuu wa Uiengereza Sunaka amesema hivi karibuni watapeleka vifaru aina bora ya challenger huko Ukraine ili visaidie kuwasukuma nyuma jeshi la Urusi.

 
Hana akili kabisa☹️ silaha huna unategemea misada halafu unajitia kiburi☹️hao Marekani wanao kuponza wananchi wao wanakula bata wewe unawaponza wakwako kwaakili zakushikiwa? Wakupe silaha zakutosha Basi sio mdomdo. Kwani ukikubali yaishe kunanini☹️na unajijua kabisa uwezo huna.
 
Mataifa ya NATO zaidi wanapeleka silaha zao kimajaribio na kusafisha maghala yao. Silaha kadhaa zinasifiwa sana zikifika zinashindwa kufanya kazi. Bado hajatia akili tu huyu Zelensky. Siku yake ya kushikwa haiko mbali.
 
Ukishambulia ukaenda kujificha kwenye nyumba ya raia unawaponza raia wako waache kutumia raia kujifichia.
Ndio majibu ya hovyo hayo kama ya Marekani. Ukipigwa unasema watoto na wanawake ni miongoni mwa waliouliwa. Na ukipiga unasema walijificha katika ya raia wawache kutumia raia kama kinga. Kelele zikiwa nyingi unajidai utaunda tume halafu unakaa kimya.
 
Zelensky anatumika na wazungu kuidhoofisha Urusi , mwisho wa Siku watu innocent wanakufa , ....Urusi na Ukraine wasinge pigana bila USA kuchochea ugomvi, Uarabuni imekuwa hivyo sababu ya marekani VITA MIAKA YOTE.....South na North korea wanataka kupigana sababu ya marekani, China na Taiwan sababu ya marekani
.........marekani is the devil himself , ninyi mwasema Urusi amevamia Ukraine kwa maslahi yake...lakini nawaambie Urusi alivamia Ukraine sababu ya Marekani, ameona jirani yake anamletea maadui zake karibu .na nchi yake....
 
Exactly...viongozi wa Ukraine wapumbavu sana....wanahatarisha usalama wa watu wao kwa kumfurahisha marekani...

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ€πŸ€πŸ€πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‡·πŸ‡ΊπŸ’ͺ
 
Hauna akili hivi wewe unaona huyu shujaa aisalimishe nchi kwa maadui wavamizi ndio akili?

Mbona anapambana nao tangia mwanzo?

Wewe naona akili zako ni za kuazima na ndio maana hata shule ulifeli
angalia unavyoandika siraha

Sijui una elimu gani hapo kiingereza ndio kabisaa hata haujui neno 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…