Zembwela ajutia kuingia sakata la DP World

Zembwela ajutia kuingia sakata la DP World

Haya si yangu. copy n paste toka twitani (sasa X):

"Mtangazaji wa Kipindi cha Good morning kinachorushwa kwenye kituo cha Wasafi FM anayetambulika kwa jina maarufu la Zembwela ameelezea masikitiko yake kufuatia matusi na maneno yasiyokuwa ya kiungwana anayoshambuliwa yeye binafsi na familia yake iliyomzunguka kwa kile kinachodaiwa kusababishwa na uwepo wa sakata la DP World linaloendelea kushika kasi hapa nchini kwa sasa.

Akizungumza kwenye Kipindi hicho leo, Jumanne Julai 25.2023 Zembwela ambaye hivi karibuni aliambatana na Watangazaji wenzake Maulidi Kitenge na Gerald Hando kufanya ziara ya kutembelea nchini Dubai kwa lengo la kujionea jinsi kampuni ya DP World inayotajwa kuingia mkataba wa makubaliano ya uwekezaji Bandarini baina yake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mamlaka ya usimamizi wa Bandari, amesema walichokifanya Watangazaji hao ni kuonesha ubunifu wa kuandaa Kipindi chao ili kutengeneza maudhui yatakayowavutia watu wengi zaidi kuwafuatilia kwakuwa uendeshaji wa vipindi na vyombo vya Habari kwasasa unahitaji ubunifu mkubwa ili 'kuteka' watu, jambo ambalo ni tofauti na vile ambavyo baadhi ya watu wameitafsiri safari hiyo.

Ametolea mfano uwepo wa baadhi ya makampuni ambayo yaliwahi kutajwa kufanya uwekezaji hapa nchini huko nyuma lakini baadaye makampuni hayo yalikuja kugundulika kuwa ni hewa na yaliisababishia taifa hasara ya mabilioni ya fedha hivyo moja ya jambo walilolenga kulifanya kwenye ziara hiyo ni pamoja na kwenda kujionea na kujiridhisha kama kampuni ya DP World ipo na kama inajishughulisha na masuala ya bandari au la, jambo ambalo amethibitisha kuwa wamejionea na kujiridhisha baada ya kuunganishwa na baadhi ya Watanzania wanaoishi Dubai"
...kuna wale jamaa ambao wanamiliki klabu ya Kikapu kule wakatusaidia kutuunganisha, kwahiyo tukaenda tukaiona DP, kweli tukakuta wana Ofisi na sio richmond style, tukakuta kweli wanafanya shughuli za Bandari, tukatembelea Bandari yao, ila walikataa kuzungumzia hiki kinachoitwa makubaliano sijuwi mkataba kwasababu sio level yetu na wale tuliowakuta Ofisini sio level yao...""

...return yake ilikuwa Watanzania wanataka sisi ambao hatujuwi vifungu vya sheria tukifika pale DP tuwaulize kwenye mkataba pale kifungu cha 3C, kifungu kidogo cha 4D ibara ya 5 mmesema mtachukua Bandari kwa upana gani..., matokeo yake Mimi, walionizunguka, Wazazi wangu, Viungo vya mwili vya Wazazi wangu na mimi mwenyewe, wote tuliingia katika vinywa na maandishi ya Watanzania na nadhani mpaka sasa bado wanaendelea kututusi, kwahiyo njia pekee ambayo mimi niliichukua ni hiyo ya kukaa kimya".

"

MY TAKE
Zembwela na kina Kitenge na waandishi wengine waliosombwa msobe msobe kuingia sakata la DP World, wajijue kuwa wana upeo finyu sana.
Sakata hili waliingia kulipigia tafu sasa wanaona matokeo yake kwao binafsi.

Waendelee na comedy zao na hakuna mtu atawasumbua,
Siasa wawaachie wajuvi, ama sivyo wataumia.
Tena anabahati hapa JF matusi hawaruhusu lakini mimi huwa kila naposikia sauti zao wakitangaza ktk radio huwa nawaporomeshea mitusi ya haja kimoyo moyo maaamke zao.
Hizo gharama za kwenda huko aliwalipia nani? Watu tunazungumzia mkataba mbovu wao wanaenda kuangalia kampuni kama ipo si UK...ma huu? Kuna Mtanganyika yeyote anatatizo na kujua kuwa hii kampuni ipo au haipo? Zembwela na mabasha zao walipaswa kunyongwa kwa usaliti. Washukuru tuu hayo matusi wanayo pata kuwa ni kidogo sana kulingana na uovu wao kwa taifa.
 
Hali ngumu ilikuwapo tangu zamani, tena zaidi ya hii, watu tumenunua unga wa muhogo kwa lazima maduka ya kaya, kwa kuandikiwa kilo kwenye kitabu kwa mujibu wa ukubwa wa familia.

Kwenda Nairobi ilikuwa big deal kwa sababu watu walikuwa wanarudi na dawa ya kupigia mswaki na sabuni.

Kuna wakati mpaka wa Tanzania na Kenya ulikuwa umefungwa. Nyerere alivyotangaza mpaka kufunguliwa watu wakapumua.

Nakuelezeni habari tulizoishi, watoto waliozaliwa 1992 wengi hawazijui.

Mtu aliyekuwa anajielewa 1980 mpaka 1985 atajua naondika nini.

Mpaka Mzee Rukhsa Alhaji Ali Hassan Mwinyi "Nzasa" akatutoa katika lindi lile la fedheha.

Lakini hatukuwa na uchawa wa kiwango hiki.

Ni watu tu kujiachia.
Mkuu hiyo "Nzassa" maana yake ni nini?
 
Mkuu hiyo "Nzassa" maana yake ni nini?
Nzasa ni sehemu ya ardhi inayokuwa majimaji au chepechepe daima, haikauki milele.Aghalabu, hali hii huonekana sana kwenye njia za vijijini zilizo karibu ya bwawa au chemchemi ndogo.

-Ali Hassan Mwinyi "Mzee Rukhsa; Safari ya Maisha Yangu".
 
Zembwela na kina Kitenge na waandishi wengine waliosombwa msobe msobe kuingia sakata la DP World, wajijue kuwa wana upeo finyu sana.
 
Hii bandari ni moto sana, watu hawataki masihara nayo kabisa!
 
Back
Top Bottom