Zembwela/ Manara Wana maisha mazuri kuliko Profesa wa Tanzania

Pamoja na kuwa na Elimu za Kuunga-unga Zembwela na Manara Wana maisha decent kuliko Maprofesa hapo SUA na kwingineko nchini
NOTE: HII COMENT HAIJAANDIKWA KWA MADHUMUNI YA KUJISIFIA BUT NATAKA NKUFUNGUE AKILI, I GUESS YOU WILL LEARN A FEW THINGS

Mimi ni mtoto wa professor kwenye moja ya reputable universities hapa nchini

First, jifunze kutofautisha Flashy life style (maisha ya online) na Humble lowkey life style, celebrites wengi wapo kwenye spotlight kwahio lazima aishi kwa kuonesha ana good life iwe money, cars, houses n.k

wapo celebrities wenye maisha mazuri wapo pia wenye maisha ya kawaida sana.


turejee kwenye point ya university proffesors.

My dad ni kama rafiki yangu, katokea humble beginings, yani kijijini interior, kitu pekee kilichomfikisha hapa ni baraka za mwenyezi Mungu, na toka amezaliwa he was very very smart, kichwani he was very very gifted.

mimi binafsi najivunia yeye kua mzazi wangu, he is a true example of a self made man, he is an Academic hustler, yani yeye katumia kichwa chake kumfikisha hapa alipo.

My dad ukiacha mshahara wake, kajiwekeza sehemu nyingi mno, ana real estate za kutosha hapa mjini, nkisema real estate i mean viwanja, mashamba(ambayo yote yamechimbwa visima vya maji), fremu za kupangisha, apartments, family houses za kurent etc.

analima na nkisema kilimo na maanisha kilimo cha kisomi na kilimo cha umwagiliaji, kilimo cha more than 50+ acres.

bado ana businesses zake zingine ukiachana na hizo real estate, magari kwake have never been an issue ana magari ya kumtosha kabisa, magari ya kazi, magari mengine ambayo hata akitoka lazma heshima yake utampa.

bado kajiwekeza kwenye stocks( ana hisa kwenye makampuni mengi ya ndani ya nchi na nje ya nchi) analipwa divends/gawio kutoka kwenye hizo kampuni kila mwisho wa mwaka.

kajiwekeza kwenye treasury bonds, ana fixed accounts ndani ya nchi, ana foreign fixed accounts za pesa za kigeni zinazomzalishia interest kila kwezi.

kazunguka sehemu nyingi sana duniani, ana fahamiana na watu wengi kwenye siasa anatumika kwenye moja ya wizara kama mshauri, kuna raisi mmoja wa nchini ni rafiki yake sanaa, yani najaribu kukuelezea tu kwa kifupi.

lakini ukimwona huwezi hata kumdhania, he is very very humble, because haishi maisha ya show off, na pia hayupo kwenye spotlight so huwezi sema ana good life.

je unajua salary ya university proffesor ni kiasi gani?, pia kuna associate proffesor na full proffesor hao wote wana mishahara tofauti, je unajua kiasi wanachopokea kila anapokanyaga darasani?

bado wanatumika kwenye consultancy, unajua rate ya kumchukua na kumtumia proffesor in consultancy?

wanaandika miradi mingi tu mikubwa, na hio miradi/projects nyingi wanalipwa na donors kwa foreign currency iwe USD, pound, euro n.k

University professor analipwa kwa kila mwanafunzi wa Phd anaemsimamia, bado wana research zao wakifanya wana funding wanapata, kwa kifupi hawategemei chanzo kimoja cha mapato

kuna ma proffesor wengine hawajiongezi, wala kujiwekeza, bado wanaendekeza anasa, multiple families, multiple children hawezi kutoboa licha ya mshahara mkubwa, but bado wana maisha mazuri ya kuwazidi wengi ya celebrities wenu wenye majina makubwa.

usidanganyike na life ya mtandaoni, most celebrities wana fake life, na wapo wengi tu pia wana maisha mazuri.

ila kuna watu wengi tu sio celebrities na wanamaisha ambayo hawa celebrities wangeyajua wangewaonea wivu na kuyatamani.
 
Wewe humjui profesa kabuni ambaye aliita binadamu mwenzie Mungu
Au mitandaoni umeingia juzi?
 
1. Kwanza ume-declare interest wewe ni mtoto wa Professor nchini, japo ni jambo zuri lakini linafanya uwe biased kwenye analysis yako.

2. Nchini, hakuna Professor anayelipwa kwa kuingia darasani zaidi ni fixed salary ambayo GROSS haizidi 6m TZS (kabla ya makato kibao=Pension fund, Health Insurance, PAYE, workers union etc), unless iwe ni part-time (anayolipwa kwa saa = 60,000/= TSH) sasa ukilinganisha hiyo amount na endorsement za Manara utaona Professor anapunjwa ukilinganisha na kisomo (academic qualifications na work experience vs Ngomaru Manara/Zembwela/Steve Nyerere).

3.......
 
Hakuna profesa anayeweza kulipa Kodi ya 8m, hata Vice Chancellor hawezi kulipa hiyo rent
 
Mtoto wa zembwela mmoja alisoma Taboragirls Alevel,
Zembwela ana hela sio utani salary scale ya pale wasafi ni kubwa sana kuliko profesa, mshahara wa profesa nasikia ni 6m, means take home ni 4m, hiyo 4m kwa zembwela ni pesa ndogo sana
 
Sasa mwanafunzi wa PhD anapewa laki1 kwa kukusanya data hiyo pesa mbona ndogo? Wakati Mkuu wa Idara halmashauri posho ni 250,000/-
Hizo pesa za consultancy Bado ni ndogo wenzio wanaingia mikataba kwa mwaka 200m na makampuni mbalimbali
 
Sasa mwanafunzi wa PhD anapewa laki1 kwa kukusanya data hiyo pesa mbona ndogo? Wakati Mkuu wa Idara halmashauri posho ni 250,000/-
Hizo pesa za consultancy Bado ni ndogo wenzio wanaingia mikataba kwa mwaka 200m na makampuni mbalimbali
Nimesema hiyo ni nje ya gharama za malazi so kwa siku akikusanya data ni laki 1 means kwa say mwezi mzima ni million 3 na huwa zinaenda mpaka miezi 3 especially kama ni qualitative. Hapo supervisor obvious anakula sio chini ya laki 3 kwa siku akiwa field kwenye hizo project.

Unaposema consultancy fees ni ndogo je wafanyabiashara au la saba wote wanaweza ingia mikataba ya 200 million? Maana hapa tuna compare wasomi na wasiosoma.

Tanzania wafanayabiashara ni zaidi ya million 5 trust me ni less than 20% ndio wanaweza kuingiza hizo faida za 200 million wengi ni SMEs tu za faida ya 10-100 million pekee per year.

Ila Tanzania maprofessor au PhD holders in academics are less than 10k... Trust me zaidi ya 80% wana uwezo wakuingiza zaidi ya 200m kwa mwaka. Basic tu salary ni 5m for PhD level meaning ni 60m from salary only achilia mbali consultancy fees, supervision, allowances, n.k

So we conclude kwamba PhD holders are more likely to make more money than an average businessman in Tanzania
 
Mtoto wa zembwela mmoja alisoma Taboragirls Alevel,
Zembwela ana hela sio utani salary scale ya pale wasafi ni kubwa sana kuliko profesa, mshahara wa profesa nasikia ni 6m, means take home ni 4m, hiyo 4m kwa zembwela ni pesa ndogo sana
Hana hela maskin yule
Na hajasoma 😂😂 ngumbaru
 
Mpoki ana jumba, V8, endorsements na bado yupo kazini vs prof wa jalalani mwenye Toyota Corolla anakaa nyumba ya taasisi na mshahara take home (3.8m)
Ila Prof kasoma🤣🤣mnataka kuhalalisha watu wasiende shule?Basi msipeleke watoto wenu shule wake kuwa ngumbaru na chawa Kama zembwela tajiri anayeishi uswazi😂
 
Hizo data anakusanya Kila siku?
Hizo laki tatu ni kwa vyuo hivi kama Extended High school,udom,sua nk?
-wapi mimi nimesema la saba wote? Mimi nazungumzia kina zembwela Niko specifically, ambao kimsingi Wana pesa kiwazidi Maprofesa
-kama basic salary ni 5m maana yake take home ni 3,250,000/- ambayo kwa mwaka take-home ni 39M, Sasa 39m kwa zembwela ndio ujilinganishe naye wewe profesa
-kwa Nini unafanya conclusion kwa hoja ambayo haipo? Tunazungumzia bussisman au tunazungumzia kina zembwela et al?
-hizo consultancy fees sio za mtu mmoja ni za department au faculty unaweza kukuta faculty nzima mmetengewa 200m kwa mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…