Ziara ya Lissu Uganda: Alimsifia Nyerere kwa 20% lakini alimdhalilisha pia kwa 80%

Ziara ya Lissu Uganda: Alimsifia Nyerere kwa 20% lakini alimdhalilisha pia kwa 80%

Vigazeti uchwara vimeanza kuibuka kuelekea uchafuzi mkuu mwaka huu. Wahariri lugha ya Kingereza haipaandi ndiyo maana hawakuelewa na alichosema Lissu na wameamua kupotosha, CCM ina upuunguani sana.
Kingine Lissu ali downplay umuhimu wa vita vya Uganda. Anaona ilikuwa ni mchakato wa Nyerere kumrudisha madarakani Milton Obote.

This is crazy!! Leo Afrika Mashariki na Kusini haijatulia kwa sababu ya instability ya DRC inayosababishwa na PK wa Rwanda.

Kuyatoa majeshi ya M23 ambayo ni vibaraka wa Rwanda hakuna tofauti na JK Nyerere alivyomfagia Iddi Amin ambaye alitaka kujimegea ardhi ya Tanzania.

Huyu Lissu anataka ku UNDO historia ya Tanzania wakati familia yake inaishi Belgium, hastahili heshima yeyote
 
Kusema ukweli ni kudhalilisha? Kweli nchi ishaharibika hii, so kwa sasa ni sifa tu na mapambio kwa wakubwa? kuna mahali Lissu alimsingizia mzee? Au alikua mtakatifu hasemwi alipokosea? Nchi hadi leo ni shithole ni nani aliifikisha ilipo? Bila kujua makosa mnarekebisha vipi mipango yenu?
Kwanza alieleza wazi kuwa katiba hii ni haiko sawa pia aliona akili zetu akaweka ukomo wa utawala unadhani ingekuwa je. Tusiruhusu vichaa wachache waharibu legacy

Pia aliongeza kipengele cha haki za binadamu muda mfupi kabla hajaondoka, la sivyo detention order zingemaliza watu.
 
Kwa hiyo hizo point mbili zinafuta makosa yake mengine yote? Legacy ni strengths na weaknesses sio mijisifa tu, hamna mtu anaweza kuifuta/kuharibu, elimu yetu imeharibiwa sana kama nyie ndo wasomi wenyewe!
 
My take is:
as long as Mwalimu Nyerere alikuwa ni Binadamu, ki-ubinadamu, ni lazima kuna makosa aliyatenda, tusitake kumfanya Mwalimu kuwa alikuwa ni malaika

Na kuna hotuba yake moja alishawahi sema baada ya kun'gatuka kuwa mazuri aliyoyafanya yachukuliwe na mabaya yaachwe, ingawa alishangaa uongozi wa awamu hio kuyaacha hata yale mazuri aliyoyafanya
 
Mkuu hizo ndio reference ya huko Uganda? Aliiongea zaidi ya siku 4 zilizopita, leo ndio hizo tissue paper zinatoa mrejesho?
Hata kama angeongea mwaka mzima uliopita, penye kumsahihisha lazima tumsahihishe.
 
View attachment 3265526

Kwa kweli Mwalimu JK Nyerere alifanya mambo makubwa kwa taifa hili na bara la Afrika na duniani na pengine wengi wetu tumefikia mafanikio tuliyoyapata kielimu, kazi na hata afya kwa sababu ya sera zake za kujali wanyonge na kuiishi falsafa ya binaadamu wote ni sawa kwa vitendo.
Mtu kwenda Kampala na kutumia vitu vidogo kujitafutia umaarufu haiingii akilini. Kufuta au kuichafua legacy ya Mwalimi siyo rahisi.
RIP our beloved father of our great nation.
Haya ni magazeti ya Uganda siyo..?

By the way, jamaa alitoa lecture almost a week now...

Cha ajabu wahariri wa vijikaratasi vya Lumumba baada ya kujifungia kwa siku nne kuandaa uzushi eti leo ndiyo yanatoka na uchafu huu...

Loooh, that's too bad for you...
 
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa hata yeye ana madhaifu yake na alitenda mambo ndivyo sivyo hakuna BINADAMU ambaye yuko perfect.

Definition moja ya "Uchawa" ni kusifia tu hata kama mhusika ana side nyingine ambayo alifanya makosa au alikosea.
 
EEeeeenHEEEEEE!

Ni kichekesho kwelikweli kwa watu kama nyinyi kumkumbuka Mwalimu nyakati kama hizi!
Ili aendelee kuheshimiwa na kukubalika na wote Lisu aache mara Moja kupambana na NYERERE na Magufuli
Hivi huyu jamaa anashida gani na marehemu?
 
Ili aendelee kuheshimiwa na kukubalika na wote Lisu aache mara Moja kupambana na NYERERE na Magufuli
Hivi huyu jamaa anashida gani na marehemu?
Mimi sitetei hayo "mapambano" kama kweli yapo, na hili nilisha liandika humu siku nyingi sana za nyuma.
Lakini ni muhimu pia ufahamu hawa wanao kazania na kukumbushia hili nia yao ni nini hasa.

Lissu hawezi kamwe kupata umashuhuri wowote kwa kupambana na kivuli cha Mwalimu Nyerere, naye hili nina hakika analitambua vyema.
 
Kwa hiyo hizo point mbili zinafuta makosa yake mengine yote? Legacy ni strengths na weaknesses sio mijisifa tu, hamna mtu anaweza kuifuta/kuharibu, elimu yetu imeharibiwa sana kama nyie ndo wasomi wenyewe!
Makosa gani hayo aliyofanya, yataje!! Kama wewe ni mbumbumbu hata upelekwe Havard utapata SIFURI tu kama Bashite
 
Back
Top Bottom