Ziara ya Rais Ruto: Yule Mkalimani achukuliwe hatua za kinidhamu!

Mi naona sio kwamba mkalimani alikosea hapana ni mgongano wa maneno kama unavyoona wahubiri wa injili kwa kingereza na mkalimani wa kiswahili
 
Hizi kazi za kupeana kwa kujuana ndio matatizo yake kama hayo !! Na ilishatokea tena na tena. Sio sasa tuu !!
 
" (Mkalimani)Utanichanganya zaidi"-Ruto
 
Kwani hata huyu rais wenu nae hajui kingereza?
 
Huu utetezi wa kijinga kidogo.
Flimsy excuses for non performance, ndio maana hata idara husika kiongozi wake awajibishwe.
 
Dah wewebhiyo clip ni nyingine na unachoongea kingine..
 
Huu utetezi wa kijinga kidogo.
Flimsy excuses for non performance, ndio maana hata idara husika kiongozi wake awajibishwe.
Sasa kama ruto amesema hataki mkalimani ndio unataka mkaliman afukuzwe?

Kwani alikataa because ya kazi yake mbaya ?

Mbona alitafsiri salam tu ndio ruto akasema hapana
 
Sasa kama ruto amesema hataki mkalimani ndio unataka mkaliman afukuzwe?

Kwani alikataa because ya kazi yake mbaya ?

Mbona alitafsiri salam tu ndio ruto akasema hapana
Inaelekea mkalimani ni yule yule wakati wa msiba wa Magu.
 
Inaelekea mkalimani ni yule yule wakati wa msiba wa Magu.

Sio Yule ni watu 2 tofaut kabisa, huyu wa Ruto ni Yule alikuwa anakaliman wakati wa mambo ya makanikia Yule wa msiba ni mwingine kabisa ana kipara
 
Kama hujasikiliza rudia kusikiliza hata yale maneno ya kwanza tu ilikuwa ni aibu. Ruto alichosema na alichokisema mkalimani ni vitu viwili tofauti. Ruto aligundua akaamua kutufichia ile aibu. Ukizingatia Ruto na wakenya wanajua kiswahili ingelikuwa ni aibu wa mwaka. Tumshukuru Ruto kutusetiri.
 
Kitu kama hicho kiliwahi kutokea mwaka 1975. Wiki chache baada ya Msumbiji kupata uhuru, Rais Samora Machel alikuja Tanzania kwa ziara rasmi kuja kuishukuru Tanzania kwa misaada iliyotoa mpaka kupatikana kwa uhuru wa Msumbiji. Kufuatana na itifaki Rais Samora alianza kutoa hotuba kwa Kireno na akawepo mkalimani wa kuwafikishia Watanzania yasemwayo kwa Kiswahili. Baada ya muda mfupi Rais Samora akaingilia kati na kuanza kusema moja kwa moja kwa Kiswahili.
 

Duh, yan mkaliman hajui hata salamu acheni mambo yenu bwana, weka clip tusikie
 
Kwenye hili Ruto ni Mshenzi sana hapa watanzania mnapaswa kujua historia, Wakenya feels with ego akija Tanzania aongee English, huyu mjinga Ruto used Kiswahili fully in his campaign for his ascendance to the presidency, In fact ni dharau kubwa Kwa host country na Rais wake, look kinly at his confidence alifanya upumbavu sana huyo Ruto, he should have used his Kenyan Swahili dialect simple as that.

Ruto alitukosea heshima mjinga yule.
 

Lakini mbona aliomba

Alisema Swahili yake sio mzuri sanaaaaa Bora akaongea English

Me sioni shida kabisa,
 
Lakini mbona aliomba

Alisema Swahili yake sio mzuri sanaaaaa Bora akaongea English

Me sioni shida kabisa,
Hapana kwani baada ya pale alitimiza ahadi yake ya kurudia Kwa Kiswahili? Yeye alijifanya kama waliohudhuria ndio walengwa wakati Ile hafla imerushwa live kwa public. Wahusika wajipange wakati mwingine
 
Hivi mtu mzima na akili zake timamu anaweza poteza muda na nishati ya akili yake kuandikia jambo dogo km hili lisilokuwa na impact yoyote mahali popote, hii ni sawa na kuwasha tochi mchana, kichaa ndio anaweza kufanya hivi..hakuna mjuzi wa lugha isiyo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…