Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Serikali ya Tanzania inatarajia kusaini Makubaliano ya Mkopo wa Riba Nafuu wa takriban Tsh. Trilioni 6.51 kutoka Serikali ya Korea Kusini kupitia ziara itakayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 31, 2024 nchini Korea

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu Tanzania, mkopo huo utakuwa wa miaka 5 kuanzia 2024 hadi 2028 ambapo Tanzania ni nchi ya pili Afrika kupokea Mikopo hiyo kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi Korea (EDCF)

Ziara hiyo ni mwaliko wa Rais Yoon Suk Yeol wa Jamhuri ya Korea ambayo itamalizika Juni 6, 2024
IMG_20240530_105458.jpg
IMG_20240530_105524.jpg


======

Pia soma:

- Tanzania na Korea: Ziara ya Rais Samia kufungua fursa mpya kwa Watanzania
 
Mikopo tumechoka sasa tunataka ndoo au pipa. Utani!
Huo mkopo ukichukuliwa msisahau kuboresha pale mlima Kitonga naona kuna mkandarasi hajiwezi.
Walau pia nimeona kuna mradi wa kutanua barabara njia ya Kimara/
 
Ile nguvu 1.3 trilion ya covid ilichangamsha nchi maeneo yote,ila zilizofuata,hazina nguvu.
 
Serikali ya Tanzania inatarajia kusaini Makubaliano ya Mkopo wa Riba Nafuu wa takriban Tsh. Trilioni 6.51 kutoka Serikali ya Korea Kusini kupitia ziara itakayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 31, 2024 nchini Korea...
HII NCHI ISHAANZA KUUZWA.
 
Huku kukopakopa kuna Siku tutakuja kutapishwa fedha za wenyewe bila kupenda.
 
we can't move as a country, sheria ya kali kama korea au japan should be set.

hizi hela nani analipa.
 
Tuwe tunaambiwa ni miradi ipi na gharama za kila mradi vinginevyo tutabiwa zimetumika kwenye mradi fulani wakati uligharamiwa na pesa za ndani.
Hii ni point kubwa sana...Tusiambiwe tu tumekopa kiasi fulani - tuambiwe pia hizo pesa zinakwenda kwenye miradi ipi.
 
Back
Top Bottom