Serikali ya Tanzania inatarajia kusaini Makubaliano ya Mkopo wa Riba Nafuu wa takriban Tsh. Trilioni 6.51 kutoka Serikali ya Korea Kusini kupitia ziara itakayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 31, 2024 nchini Korea
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu Tanzania, mkopo huo utakuwa wa miaka 5 kuanzia 2024 hadi 2028 ambapo Tanzania ni nchi ya pili Afrika kupokea Mikopo hiyo kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi Korea (EDCF)
Ziara hiyo ni mwaliko wa Rais Yoon Suk Yeol wa Jamhuri ya Korea ambayo itamalizika Juni 6, 2024
View attachment 3003469View attachment 3003470