Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea


Why don't we do the extraction ourselves? If that is as easy as we talk
 
Mkuu mradi wa gas mliona hauna tija bali bwawa la Nyerere bora tuuze hiyo gas kwa wahitaji ili sisi tusubirj umeme wetu maana tuliaminishwa umeme wa gas ni ghali kuliko huo wa maji..
Hayo mengine yanajijibu yengewe...
 
Tanzania kwa sasa mteja mkubwa wa natural gas si viwanda wala sekta binafsi bali ni Serikali yenyewe kupitia Tanesco. Wakati huo huo Serikali inajenga JNHS, hivyo kupunguza utegemezi wa gas katika uzalishaji wa umeme.

Viwanda vya sekta binafsi vinavyotumia gas ni vichache na hii inasababishwa na ukubwa wa gharama za miundombinu kutoka kwenye pipeline ya gas kwenda viwandani.

Hivyo, kupanua soko na kuangalia uhitaji, Kenya anahitaji gas yetu katika viwanda vyao na possibly hata kwenye uzalishaji wa umeme wao baadae. Kwa ukubwa wa uchumi wa Kenya tumechelewa kuwauzia gas.

Hivyo kuwauzia Kenya kunapanua soko hususani kwenye uzalishaji wa gas. Huu si uamuzi wa Mama tu bali mpango huu ulikuwepo hata kabla ya Mwendazake. Kwa miaka 6 ya Mwendazake biashara ya natural gas ilidumaa kwa sababu ya siasa za protectionism.

Hakuna maana kusifika kuwa na 58 tcfs na tuogope kufanya biashara. Ingekua hivyo basi Urusi isingeuza gas Ulaya. Leo hii Gazprom ni moja ya makampuni makubwa duniani, ingekua wanatumia mawazo yako kusingekuwa na Gazprom.

Ifike mahali tukubali kufanya biashara na tufungue nchi. Mawazo ya kijima hayana nafasi karne hii.

Pia uzalishaji wa gas unavyoongezeka na kukua, fursa ya kuwekeza Tanzania inaongezeka. Itafika mahali itakuwa ni cheap kufungua viwanda Tanzania kuliko Kenya.

Kwenye biashara ya ndege, kukujibu kwa ufupi tu, bila Air Tanzania kushirikiana na mashirika mengine, hususani safari za nje ya nchi basi kifo chake kiko karibu zaidi.

Mama Samia anafanya sahihi. Ni muhimu kufungua nchi na kufanya biashara kuliko kubweteka na kukalia woga.
 
Suala la uoga hasa kuogopa ushindani na Kenya ni upuuzi walionao Wabongo wengi, inferiority complex imewatawala ndiyo maana wanadhani protectionism ndiyo mtetezi wao pasina kujua ya kuwa inadumaza maendeleo.
 
Huenda sijakuelewa au sijaelewa swali lako maana naona kama swali lako limechanganya 2 economic flows (flows ya goods& services na flows ya capital). Monopolistic competition haijalishi ikiwa ni ndani au nje ya nchi, cha muhimu ni yale mazingira ya ushindani yanatawaliwa na sifa zipi. Na kimsingi hakuna essence yoyote ya kwamba unawekeza nje ya nchi ikiwa tu ndani kuna ushindani mkubwa uliofanya faida iwe ndogo kiasi cha kwenda kuitafuta nje kwani neno faida nalo lina tafsiri pana katika context ya uwekezaji. Hata hivyo wawekezaji wengi wanaoenda kuwekeza nje wanakuwa wameanza na uwekezaji ndani ya nchi zao.
 
Kenyatta anapush biashara zake za maziwa brookside..

Enzi za Magufuli , Sukari ilikua ilukua ya mtibwa na maziwa ni darfresh, tangafresh, asas, au azam..

Brookside yalitoweka kabisa..
 
Kwaiyo mama hana tofauti na chief MANGUNGO?

Any way kasema watanzania watapeleka mahindi badala ya kupeleka sembe?
Utamtofautishaje na Mangungo...kajidhoofisha kijinga sana..yeye anafikiri kupewa heshima ya kuutubia bunge ni kupendwa...Wakenya ni mafisi
 
Hivi tumewasahu wakenya jam an I!? Sawa tuwe na mashirikiano nao Ila Kwa uangalifu mkubwa Sana kwanza turekebishe mifumo yetu iwe ya kicapitalist kwelikweli kama wao laasihivyo watatupiga kwelikweli tukumbuke tangu enzi ya mwalimu JK hatujawahi kuwa na uhusiano mzuri na hawa watu ikaja Kwa kikwete wakatufanyia rohombaya waziwazi Kwa manufaa yao tunakumbuka sote sakata la madereva Wa utalii,kuzuia bidhaa za unga kuingia kenya,figisu walizozifanya kuzuia bomba la mafuta kutoka Uganda lisijengwe kuja tz mpaka raid wao alienda ufaransa kukutana na mabosi wa total wakaja na reports zao feki kuhusu mazingira na kuharibu ecolojia ya wanyama iwapo bomba litajengwa aisee hawa watu hawajawahi kutupenda jamani hata kipindi za Hayati walikua wanazuia madereva kuingia kwao lakini wa nchi nyingine wanaruhusiwa swali ni je saivi wamewaruhusu hayo mahindi yameondolewa sumu?! Je ile barua iliyoandikwa na wizara ya kilimo ya kenya kuyachafua mahindi ya tz imekanushwa?! Maana kibiashara ametuchafua na ilitangazwa kwenye media zao zote je madereva hawana corona?! Kenya nawapenda Sana yupo tayari kukufanyia roho mbaya kwa manufaa ya wakenya sisi tunawafanyia roho nzuri kwa manufaa yao tena
 
Kwanini hatuundi magari yetu wenyewe? Ndege? Vijiti vya meno n.k?

Something is wrong with our thinking. We dont want to pay the price of getting the development. We just want things for free
 
Ni kweli ila mama alitakiwa asimamie kwenye Sembe na si mahindi(malighafi) ingependeza sana.
Mkuu lazima kwanza tubadilike kwa ajili ya soko la nje. Ikiwa sembe letu la ndani bado lina kiwango hafifu je tunaweza kuwakubalisha watu wa nje kulikubali? Wako baadhi ya wafanyabiashara wanaopeleka sembe na mchele na si mahindi. Ila hawa wakina mimi ndo bado wanapeleka mahindi kwa tamaa zao wakizuiwa ni shida nyingine...
 
Nakubaliana na wewe ila kwanini mama akuwaanda wafanyabiashara wa ndani then angeitisha safari kwenda Kenya ili angeongea na Uhuru wangekubaliana kuuza Sembe na sio mahindi mkuu.

All in all mama alitakiwa kuandaa mazingira mazuri kwa raia wake kuhusu kuuza semba sio mahindi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…