Napenda kuandika kidogo tu kulingana na uwelewa wangu juu ya Ziara ya Mama nchi Kenya na mikataba mlio tiana sign.
1. Ujenzi wa bomba la gas kutoka Tanzania kwenda Mombasa kwa ajili ya matumizi ya viwanda nchini Kenya,hapa mama unefail pakubwa sana maana yake nikwamba bidhaa za Kenya zitakuwa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi na kuteka soko la Africa Mashariki kuliko Tanzania. Tutarudi miaka ya nyuma tena kila kitu Made in Kenya.
a. Hii sera yetu ya viwanda itakufa maana hatuweza kushindana tena na product kutoka Kenya na vijana wetu watazidi kuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka nje.
b. Kenya itatumia mwanya huu kuvutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza Kenya kuliko kuja kuwekeza Tanzania.
c. Tunasafirisha gas kama kuna surplus ya viwanda vyetu na matumizi yetu kama Taifa.Viwanda vyetu bado vinahitaji nishati ya gas lakini bado upatikanaji wake umekuwa mgumu na kwa gharama kubwa
d. Kenyatta amecheza karata yake vizuri katika ujenzi wa gas kuliko Mama sijui washauri wake wamekwama wapi natarajia kuona Kenya ikinufaika zaidi katika utawala wa Mama kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Tanzania na Kenya.
2. Ushirikiano wa anga..hapa Kenyatta anatafuta namna ya kuisaidia Kenya airways..inakwenda ku dominate soko na anga tena kama huko nyuma.hapa kumbuka faidia kubwa ya Kenya Airways inatokana na safari za Tanzania. Dsm, Zanzibar na Kilimanjaro.
Hapa tutalajie Air Tanzania ikifa kifo cha mende kutokana kutoweza kumudu ushindani na Kenya airways. Otherwise kufanyike changes za haraka katika Management ya Air Tanzania.
3. Soko la utalii hapa Kenyatta amecheza vizuri kama pele.
Tutalajie kuona vijana wetu wakiwa watazamaji kama kipindi cha nyuma na soko la utalii nikirudi mikononi mwa wakenya tena.(hapa kwenye utalii wenye fan zao wanaweza kudadavua kwanini Kenyatta amecheza kama Pela)
4. Biashara sioni jipya ni yale yale, hapa Mama ametoka 0-0
Note: Mama washuri wake wamshauri vizuri kabla yakwenda kufanya mikataba kwa niaba ya Watanganyika. Otherwise akubali kutuachia Tanganyika yetu!
Inaonesha una hofu zaidi. Nategemea utaleta ufumbuzi wa kutatua changamato ulizoona.
Awali ya yote tukumbuke mfumo wa uchumi tulioanza nao mara baada ya kupata uhuru na wenzetu walianzaje.
- Ujenzi wa bomba la mafuta kuwezesha Kenya kuzalisha bidhaa zaidi. Hapa tujiulize kwa nini wataweza kuzalisha na kuuza kwa bei nafuu. Kinachotakiwa kufanya ni kuweka bei ya ges chini kuliko Kenya hivyo wawekezaji wa nje wataamua kuwekeza Tanzania badala ya Kenya kutokana na unafuu huu.
Tena kuna uwezekano mkubwa kwa Kenya kununua gas kutoka Tanzania na kuiuza nchi za nje. Kwa sababu wao wana bandari bora kulinganisha na Mtwara na ni karibu na masoko. Sehemu kubwa ya gas yetu tulitegemea wawekezaji wauze gas hiyo nje kuliko hapa kwetu kwa vile matumizi yetu ya gas yako chini. Na ndio lengo kuu, isipokuwa kuna mahali tumezubaa na wenzetu wanatumia fursa. Na uwezekano wa kuuza gas yetu nje kupitia Kenya upo pia.
- Sera ya viwanda haiwezi kufa kama itasimamiwa kwa ukaribu. Kuna wawekezaji zaidi ya 500 kutoka Kenya. Inaonekana wamevutiwa kwa wingi kuwekeza kwetu. Usiogope, sera yetu ni kuvutia wawekezaji kutoka nje, lakini kwa vile ni Wakenya tunatishika, hatutishiki kwa Wachina, sawa Watanzania waliowekeza Kenya ni wachache, je Watanzania wangapi wamewekeza China?
- Kuhusu Kenya Airways ku dominate soko la Tanzania ni swala la mikakati tu. Waliweza ku dominate soko kwa vile hatukuwa na ndege. Air Tanzania nayo ifanye mikakati kutafuta masoko, mamlaka za viwanja vya ndege na washirika wake watoe huduma nzuri kwa wateja na kutafuta njia mpya. Tujifunze kutoka kwao, shirika lao pia linaendeshwa kwa hasara pamoja na kuwa wabia na KLM.
- Soko la utalii. Tumegundua kwamba tatizo letu ni kujitangaza. Kwa kipindi hiki tumejitangaza sana na tunaendelea kufanya hivyo, hata klabu kama Simba imeona umuhimu huo na kutakuwa na impact. Tuendelea kuimarisha viwanja vya ndege kuwezesha ndege kubwa kutua ili watalii wafike moja kwa moja Tanzania badala ya kushukia Kenya. Kwa mfano upanuzi wa viwanja vya ndege vya Songwe Mbeya na Iringa vitawezesha watalii kufika kwa urahisi katika mbuga za Ruaha, Kitulo, Katavi, Udzungwa nk. Watalii wengine hawapendi kwenda sehemu moja miaka yote, hivyo ni nafasi kubadili kutoka Kenya na Ukanda wa kaskazini na kuhamia Kusini
Nchi kama Dubai haikuanza na viwanda na sidhani kama kuna viwanda vingi, lakini mazingira rafiki yamepafanya kuwe kitovu cha biashara, hivyo kwa bidhaa za Kenya pia tunaweza kuwa kitovu cha biashara kwa bidhaa za Kenya kwenda nchi kama Afrika ya Kati na kusini. . Mbona bidhaa kutoka China zinanoingizwa na Watanzania pale Kariakoo zinanunuliwa na wafanyabiashara kutoka Kongo, Zambia, Burundi n.k? Hakuna kisichowezekana.
Kimsingi tuondoe hofu, tutumie fursa tulizonazo.