Hoja zako zote ziko wrong.
Kuhusu gesi.
Hadi sasa hakuna uhaba wa gasi kwa matumizi ya Tanzania. Bomba la kusafirisha gesi toka Mtwara hadi sasa linafanya kazi chini kabisa ya uwezo wake haifikii hata asilimua 50. Hakuna kiwanda cha ndani kinachohitaji gesi ya Mtwara na kinashindwa kupata. Kuuza gesi Kenya kutasaidia bomba la gesi liweze kuwa utilised walau juu ya asilimia 50. Duniani kote walio na gesi nyingi wanaiuza nje ili kupata fedha tena kutokana na gesi kugunduliwa kwa wingi hivi karibuni bei imeanza kushuka rejea eneo la mediteranian. Kosa linaloigharimu Tanzania isinufaike sana na gesi yake ni mikataba mibovu ya uchimbaji na ujenzi wa bomba la Mtwara Dar iliyoingiwa na serikali ya awamu ya nne. Ndio maana umeme wa gesi umekuwa ghali. Hivyo kuiuza Kenya kutaleta unafuu kwa sababu ya economy of scale.
Uwekezaji wa Kenya
Kenya kana zilivyo nchi zote za dunia wana haki pia ya kuwekeza Tanzania kwa kufuata sheria zetu xa uwekezaji. Kwa nini ulalamike Kenya wakiwekeza lakini hulalamiki US au China wakiwekeza nchini? Hata hoja ya kulalamika kuwa Kenya wamewekeza miradi 500 nchini sisi tumewekeza miradi 30 haina mashiko kwani katika uwekezaji sio lazima mlingane , kinachotakiwa ni sisi kama nchi tuwe na sheria nzuri zinazolinda maslahi ya watu wetu wakati uwekezaji unafanyika. Kuna maeneo tunaweza kuzuia kabisa, mfano kumnyang'anya ardhi ya kilimo mkulima mdogo kisha ardhi hiyo hiyo unampa mkulima mkubwa toka nje alime.
Viwanda
Hoja kwamba viwanda vya Kenya vitaua viwanda vyetu haina mantiki. Katika uchumi sio lazima uzalishe kila kitu hata kama huna comparative advantage. Unachotakiwa kufanya ni kuzalisha vitu ambavyo una comparative advantage na kuwauzia wenzako kisha wewe unanunua vile ambavyo huna comparative advantage. Kama gesi imetoka kwetu ikasafirishwa umbali mrefu kwenda Kenya maana yake kuna gharama kubwa ya kuisafirisha kwa mtumiaji wa Kenya kuliko mtumiaji wa Tanzania hivyo kama bado pamoja na ughali wa gesi bado bidhaa toka Kenya ambayo imesafirishwa kuja Tanzania itauzwa kwa bei nafuu kuliko bidhaa kama hiyo iliyozalishwa Tanzania maana yake ni kuwa kiwanda cha Tanzania ni inefficient producer. Sasa wewe uko tayari kununua bidhaa ya ndani tena isiyo bora kwa gharama kubwa kuliko bidhaa rahisi lakini bora toka nje? pia kumbuka bidhaa toka Kenya ikiuzwa nchini serikali inakusanya kodi ya VAT na kodi ya mapato na wananchi wanapata satisfaction kwa kula bidhaa bora. Viwanda vya ndani Tanzania vinaathiriwa na gharama kubwa za uzalishaji zinazotokana kwanza na ughali wa nishati ya umeme au gesi unaitokana na mikataba ya kufisadi iliyofanyika huko nyuma na sio sababu ya kuelewana na Kenya.
Usafiri wa anga
Kuruhusu Kenya airways kuja nchini maana yake pia ATCL inaruhusiwa kwenda Kenya hivyo pande zite mbili zitanufaika. Hata kana ATCL haiwezi kushindana na Kenya airways, bado Tanzania itapata faida za moja kwa moja na zile zisizo za moja kwa moja. Ndege za kenya zikitua katika viwanja vyetu zitalipa kodi mbali mbali, kuweka mafuta, kununua vyakula vya kwenye ndege, makampuni yetu ya kuhandle mizigo yatapata kazi ya kushusha na kupakia, abiria wanaokuja wanatumia pesa kwa huduma wawapo nchini. Urahisi wa connection kuja nchini tokea hub ya Jomo Kenyatta airport utafanya tupate wageni wengi wakiwemo watalii kwa sababu ni rahisi uwanja wao kupokea wasafiri wanaokuja kwetu kutokana na mashirika mengi ya ndege kufua huko. Kiuchumi manufaa ni mengi mno kwa Tanzania tena pengine kuliko hata kenya yenyewe. Kama ATCL ikishindwa kuperform mchawi wetu sio Kenya ni sisi wenyewe mipango yetu mibovu.
Mazao ya wakulima
Wakulima wetu watapata sako la uhakika hivyo kuchochea bei anayolipwa mkulima kuongezeka kutokana na ushindani. Kumbuka hivi karibuni walipozuia mahindi yasiingie kenya bei ya mahindi kwa mkulima ilishuka sana.
NB: Tuache chuki dhidi ya Kenya bali tujifunze na kuiga toka kwao moyo wa kufanya kazi kwa bidii, uzalendo kwa nchi na kuwa aggressive katika kuchangamkia fursa.