Punguza chuki mkuu, usije ukapata presure au ugonjwa wa moyo bure!!!Labda diplomasia ya kuvaa ushungi.
haya maisha ni mapito tu.
Pia kumbuka kuwa binaadamu wote ni sawa tu mbele za Mungu hivyo hatuna sababu ya kuchukiana au kudharauliana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Punguza chuki mkuu, usije ukapata presure au ugonjwa wa moyo bure!!!Labda diplomasia ya kuvaa ushungi.
Matope hasa.ulitaka tuuze wapi gas mzee, manake hata tusipowauzia sisi wao wanaweza kuuziwa na wengine. unataka gasi tuifanyie nini mzee. yaani unapata mteja kununua gas afu unasema unaogopa kumuuzia asije kukupita kiuchumi? akili au matope.
Napenda kuandika kidogo tu kulingana na uwelewa wangu juu ya Ziara ya Mama nchi Kenya na mikataba mlio tiana sign.
1. Ujenzi wa bomba la gas kutoka Tanzania kwenda Mombasa kwa ajili ya matumizi ya viwanda nchini Kenya,hapa mama unefail pakubwa sana maana yake nikwamba bidhaa za Kenya zitakuwa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi na kuteka soko la Africa Mashariki kuliko Tanzania. Tutarudi miaka ya nyuma tena kila kitu Made in Kenya...
Mwambie huyo mjinga! Nani anaongoza Germany, Scotland, Newzealand ? Nani anaongoza WTO, IMF?Hayo maneno ya mkosaji !!fikra za miaka ya 50!!, wanawake wameongoza wazungu na kuleta maendeleo makubwa itakuwa kwa mwafrika, tena mtanzania?!!huyo mwanaume aliyeongoza miaka mitano , maendeleo gani ameyaleta?hao kina mseveni, mugabe, derby, biya, sasongweso zaidi ya miaka 30, madarakani walifanya nini?!acheni hizo muhukumuni mtu kwa uwezo wake na sio JINSI, yake.MAMA KANYAJA TWENDE,
Viwanda vya kubangua korosho tulikuwa navyo wakati wa Nyerere lakini kwa sera zetu za kijamaa na kukosa menejimenti vilikufa by early 1990s.Ndiyo maana nimesema tuna viongozi wasiokuwa na maono.
Umetoa mfano wa Korosho, sasa hebu jiulize, ingekuwaje kama tungekuwa na kiongozi mwenye maono na akili akahakikisha nchi inakuwa na viwanda vya kuchakata Korosho, na kisha Korosho hiyo tukaiuza kutokea Tanzania kwenda kwa walaji moja kwa moja?
Tukija kwenye issue ya Gesi, kwanini viwanda vyetu visipewe kipaumbele kwanza kabla ya kuiuza kwa majirani zetu?
Uchumi wa kati[emoji1787][emoji2][emoji1787]Magufuli na Kikwete nani aliua uchumi. Au ule uchumi wa madawa ya kulevya ndiyo mliona maendeleo. Mpende msipende hakuna raisi wa TZ ambaye aliupandiksha na kuukuza uchumi kama Magufuli. Mnaweza mkamchukia lakini alitutoa chini kabisa na kutufikisha uchumi wa kati. Hata Nyere hakuweza hilo. Leo hii ingekuwa bado awamu ya NNE hata mawaziri na viongozi wakuu wa serkali wangekuw wamekwisha kuwa MATEJA.
Hili suala la kuweka restriction za corona na kujipendekeza kwa watu sijajua mshauri ni nani, inatuletea picha ya udhaifu! Akimaliza hii ya Magufuli, itakuwa ngumu sana mimi kumpigia kura, niwe mkweli, nachukia udhaifu dhaifu kwenye uongozi! Tunarudi tena enzi za msoga sasa.
Unaposema kugawa gesi una maanisha nini? Kwani hao wakenya wanapewa bure?Unatazama kwanza hicho unachokiuza ni kwa gharama ipi. Sio tu kwasababu hakina mahitaji kwa sasa basi ukamua kukitoa sadaka na ukasahau baadae.
Gesi kwa sasa ni nishato nyeti sana kwetu sisi watanzania. Hatutakiwi kuigawa kama tunagawa njugu. Hebu fanya utabiri wa matumizi ya miaka ijayo ya nishati ya gesi kama chanzo cha nishati mbadala...
Aliyekufundisha uchumi kwamba unauza kitu nje ya nchi tu iwapo una "surplus" mwambie amekudanganya. Comparative advantage na monopolistic competition ndio msingi wa biashara ya kimataifa unaotumika sasa. Na ingekuwa hivyo usemavyo, basi dunia asingeweza kuishi mtu.
kufanyia nini wakati hajasogezewa karibu ?Jibu wewe uliifanyia nini? Au unafikiri yote tungetumia sisi bila kutafuta masoko?
warusi wenyewe wanashida ya nishati kama sisi?kwani gas anapewa bure...?
Urusi anauza gas karibu ulaya yote..
sioni kibaya labda kama tunampa bure...
Si ndio nikasema hakuna alienyimwa, wote wamepewa 💯Sasa unajua aliyetaka kumpa Dangote gesi ni nani na aliyemnyima ni nani?
Bomba lilishafikishwa mpaka Mita chache karibu na kiwandani. Rais wenu aliyefariki ndiye alikataa asipewe gesi bali pale pajengwe Substation uzalishwe umeme, yeye auziwe umeme na umeme mwingine utatumika kwenye viwanda vitakavyojengwa pale kwamaana palishatengwa kama Industrial park kwa Mtwara. Kwahiyo makosa ya mwingine asipewe Mama Samia, labda yeye atarekebisha, who knows!!
Aya nitajie kiwanda kingine kilichohitaji gesi kikanyimwa!!
Unaijua gharama ya kusogezewa karibu hiyo gesi?? Ukiambiwa uchangie angalau 50/50 utaweza??kufanyia nini wakati hajasogezewa karibu ?