Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan - Zanzibar, leo Septemba 2, 2022
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni amesema kuwa kupitia mfuko wa tozo, Wizara ya hiyo inajipanga kujenga vituo vya polisi na makazi ya askari 51780 nchi nzima.
Mpango wa awali wa wizara hiyo ilikuwa ni kukamilisha mchakato huu kwenye kipindi cha miaka 10 lakini kutokana na uwepo wa vyanzo vipya vya mapato (tozo ikiwemo), sasa wataukamilisha ndani ya miaka 3 ya mwanzo ya uongozi wa awamu wa sita.
Aidha, Mhe. Masauni amesema mapendekezo ya Rais aliyoyatoa moshi kuhusu kutatua changamoto ya matumizi mabaya ya fedha kwenye idara ya jeshi la polisi, wao kama wizara wameanza kuchukua hatua ikoiwemo kuhamisha fedha za mfuko wa "kufa na kuzikana" kwa kuzipeleka kwenye Shirika la bima ya Taifa ili walipwe kutoka huko.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kituo cha Polisi Mzimkazi, Jimbo la Makunduchi, Kusini Unguja ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni Rasmi.