Ziara ya Ruto nchini Marekani inatufunza kwanini Hayati Magufuli aliamua kuimarisha ATCL

Ziara ya Ruto nchini Marekani inatufunza kwanini Hayati Magufuli aliamua kuimarisha ATCL

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Hadi sasa haieleweki Rais Ruto katika safari yake iliyobatizwa Jina la " Coming to America" alitumia kiasi gani kukodi ndege

Wataalam wa usafiri wa anga wanakisia Serikali imetumia Zaidi ya Ksh million 200 kukodi ndege hiyo Lakini Rais Ruto anasema Rafiki zake ndio walimkodisha ndege hiyo kwa gharama isiyozidi Ksh million 10

Mjadala ni mkali Citizen TV

Hapa ndipo nimemkumbuka yule Shujaa wa Afrika Dkt. Magufuli aliyetuachia urithi wa ndege za kutosha kuepuka mambo ya viongozi kukodi ndege kwa Marafiki

Mlale Unono 😃😃
 
Ulichokiandika hakina uhusiano, irrelevant.

Kinachopingwa na wakenya wengi ni namna safari ya Ruto kwenda USA ilivyofanyika kwa gharama kubwa zisizo za lazima.

Fahamu tu, Kenya airways wana ndege nyingi, kubwa na nzuri, ilitosha Ruto kutumia Kenya Airways kwenda USA na kusingekuwa na mjadala wowote.

Sioni suala hili halina uhusiano wowote na Magufuli kuifufua Air Tanzania kihuni huni vile kwa kununua mandege mabovu mabovu.
 
Kuna tweet Ruto kasema wamekodi kwa sababu gharama ya kwenda na KQ ilikua kubwa sana waka opt kukodi.

Jionee hapa chini.
Screenshot_20240530-201513.jpg
 
Mleta mada naona umechanganya mambo hapa. Na hii nadhani ni kutokana na kutoelewa kile ambacho kimezua mjadala huko Kenya.

Kinachohojiwa huko siyo kutokuwa na shirika la ndege imara, ila ni kitendo cha Ruto kukodi ndege kwa ajili ya ziara yake hiyo ya Marekani.

Kwamba Wakenya wanaamini kuwa hakukuwa na ulazima wa kukodi ndege hasa kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha pesa.

Ndiyo maana Ruto anajitetea kuwa, hakutumia pesa za umma kukodi ndege hiyo, bali alichangiwa na aliowaita ni rafiki zake.

Lakini, siyo suala la uimara au ulegevu wa shirika la ndege la Kenya, kwani KQ ni moja ya mashirika ya ndege imara Afrika Mashariki na Kati.

Lina safari hadi za kwenda huko USA na Uingereza, wakati ATCL haiendi hata Afrika Kusini.

Ova
 
Mpaka sasa hivi ninavyoandika hapa zaidi ya ndege nne za ATCL zilizonunuliwa na Magufuli zimepaki chini, mbovu, haziruki popote zaidi ya miezi sita na hazijulikani zitafufuka lini.
Je ni mbovu au labda season ya biashara imekuwa low?

Kuhusu boing nadhan inajulikana dunia nzima kwamba zilisimamishwa kutokana na hitilafu fulani fulani
 
Mwisho kabisa Ruto ametumia hoja dhaifu sana ya kusema eti ni marafiki zake wametoa pesa za hiyo ziara. Ruto amesahau haya;

1. Maafisa wa serikali hawapaswi kufadhiliwa chochote moja kwa moja kutoka kwa mtu, taasisi au kikundi fulani. Ufadhili wote wa namna hiyo, ni sawa na rushwa, utakatishaji wa fedha.

2. Ufadhili huo ulipaswa kutangazwa kabla na kuidhinishwa na vyombo husika vya serikali nk.

3. Kwa kuwa mpaka sasa Marekani (wenyeji wa hiyo ziara) na shirika la ndege (wasafirishaji) wamekanusha kutoa ufadhili huo, hiyo ina maana kama ni kweli huo ufadhili ulitolewa na watu basi walitoa pesa, sasa imekuwaje Serikali ikaidhinisha matumizi makubwa hivyo ya pesa kwa ajili ya ziara wakati wangeweza kufanya tofauti.
 
Ulichokiandika hakina uhusiano, irrelevant.
Kinachopingwa na wakenya wengi ni namna safari ya Ruto kwenda USA ilivyofanyika kwa gharama kubwa zisizo za lazima.

Fahamu tu, Kenya airways wana ndege nyingi, kubwa na nzuri, ilitosha Ruto kutumia Kenya Airways kwenda USA na kusingekuwa na mjadala wowote.

Sioni suala hili halina uhusiano wowote na Magufuli kuifufua Air Tanzania kihuni huni vile kwa kununua mandege mabovu mabovu.
Tukikupa urais unao uwezo hata wa kununua mpya moja??

Tumpe heshima zake angalau alijaribu.
 
Hadi sasa haieleweki Rais Rutto katika safari yake iliyobatizwa Jina la " Coming to America" alitumia kiasi gani kukodi ndege

Wataalam wa usafiri wa anga wanakisia serikali imetumia Zaidi ya Ksh million 200 kukodi ndege hiyo Lakini Rais Rutto anasema Rafiki zake ndio walimkodisha ndege hiyo kwa gharama isiyozidi Ksh million 10

Mjadala ni mkali Citizen TV

Hapa ndipo nimemkumbuka yule Shujaa wa Africa Dr Magufuli aliyetuachia urithi wa ndege za kutosha kuepuka mambo ya viongozi kukodi ndege kwa Marafiki

Mlale Unono 😃😃
Si bora hata huko kenya kiasi cha pesa alichotumia. Rais Ruto kinajadiliwa. Kwenye media
Ungeweza kufanya hivo awamu ya 5?
 
Back
Top Bottom