Jibu la uswahili hili. Tofautisha Kati ya mashirika ya msingi na ya kibiashara. Halafu, kwako wewe, tofauti ya ATCL na Shabiby ni ipi?
Usafiri wa anga ni huduma ambayo inaweza kutolewa na sekta binafsi serikali ikabakia na jukumu la kuimarisha miundombinu na usimamizi (regulation) tu.
ATCL haliwezi kustahili ruzuku ya serikali kama suala la kudumu la kisera. Halina justification ya kuendeshwa kwa hasara na ruzuku. Itakuwa mzigo mkubwa usio wa lazima kwa walipa kodi. Mapato yake lazima yapimwe kama a going concern. Angalau i-break even basi.
Ikishindikana ni kubinafsishwa tu. Ndicho kinachofuata. Soma yanayoendelea katika SA na KQ.
Huduma za abiria kwenye treni, vivuko na usafiri jijini zinaweza kupewa ruzuku kama namna ya kupunguza makali ya maisha na kuongeza ufanisi wa mizunguko (mobility) kwenye maeneo yenye changamoto ya usafiri.