Ziara ya Ruto nchini Marekani inatufunza kwanini Hayati Magufuli aliamua kuimarisha ATCL

Ziara ya Ruto nchini Marekani inatufunza kwanini Hayati Magufuli aliamua kuimarisha ATCL

Mleta Mada umedhihirisha Fikra za Kikomunisti zinazoimaliza Tanzania KQ iko kibiashara sio Shirika hili la ATLC ambalo kazi yake ni kubeba Viongozi Uchwara.
 
Mleta mada naona umechanganya mambo hapa. Na hii nadhani ni kutokana na kutoelewa kile ambacho kimezua mjadala huko Kenya.

Kinachohojiwa huko siyo kutokuwa na shirika la ndege imara, ila ni kitendo cha Ruto kukodi ndege kwa ajili ya ziara yake hiyo ya Marekani.

Kwamba Wakenya wanaamini kuwa hakukuwa na ulazima wa kukodi ndege hasa kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha pesa.

Ndiyo maana Ruto anajitetea kuwa, hakutumia pesa za umma kukodi ndege hiyo, bali alichangiwa na aliowaita ni rafiki zake.

Lakini, siyo suala la uimara au ulegevu wa shirika la ndege la Kenya, kwani KQ ni moja ya mashirika ya ndege imara Afrika Mashariki na Kati.

Lina safari hadi za kwenda huko USA na Uingereza, wakati ATCL haiendi hata Afrika Kusini.

Ova
Amesema kwa nini hakusafiri na KQ
 
Shirika letu ni hasara tuu,wala msijivunie ATCL .Uzuri report za CAG zinaonyesha mambo yalivyo
 
Tunamlaumu Magufuli kwenye ATCL kwa haya;
1. Aliilazimisha ATCL kununua ndege kubwa na nyingi wakati walikuwa hawazihitaji kwa wakati huo.
Ndege kubwa na nyingi zinahitajika kwa wakati gani??
2. Aliingilia tender ya ununuzi wa ndege za ATCL hivyo gharama ya ununuzi ikawa kubwa maana wauzaji hawakushindanishwa.
Gharama ilikuwa kubwa ukilinganisha na bei ipi ambayo ina ushindani??
3. Alinunua ndege mbovu na mtumba kwa bei ya ndege mpya.

4. Alinunua ndege nyingi, kwa haraka, kwa cash na hiyo imezaa hasara mara dufu.
5. Aliingiza ATCL katika mtego wa kutumia gharama kubwa kuzihudumia hizo ndege alizozinunua wakati ATCL haikuwa na uwezo huo.
ATCL inauwezo wa kufanya nini??
 
Mambo ya ATCL na TRC ni yale yale, kote huko Magufuli alikosea, na usitegemee chochote kikubwa, kizuri au cha kudumu kutoka TRC kwenye SGR na treni za umeme. Ni miradi ya upigaji mtupu, haina faida yoyote kwa nchi au mlalahoi.
Kuanzia malengo, tender mpaka ujenzi wa SGR vyote havijakaa sawa, hivyo tutavuna mabua tu.
Mkuu ifike hatua watanzania muache uzembe ktk kufikiri.hizi siasa kila sehemu ndizo zimetufikisha hapa tulipo.

Bila shaka ni mmoja wa watu wanaokosoa ujenzi wa bwawa la umeme,hii sio bahati mbaya ni laana imekomaa vichwani,au laah mnafanya kazi za watu.

Yaani miradi mnayoshindwa kuiendesha alaumiwe aliyeianzisha!!!
 
Mkorinto,

Kuna mtu anaitwa pascal mayalla alikuwa akisifu sana kuhusu ATCL
Uzi wake huu hapa.

Baadae akaja kuomba radhi kwa kusema kwamba hakuwa sahihi katika uzi wa barafu

Post in thread 'Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka'
Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

Kuna wakati watu wanasema si kwamba kupinga kinachofanywa na serikali ila kuna watu wana uwezo wa kutazama mbali.

Yapo wapi yale mapambio? Shirika limeendelea kupoteza kwa miaka mitano mfululizo tena kipindi magufuli yupo.

Penye ukweli pasemwe. Mzee wetu magufuli kuna vitu hakuwa sawa. Aidha ni ego aliyokuwa nayo au alitaka ufahari kwa namna fulani.
 
Mkuu elimu ya uraia inapanuka, barafu ya ujinga inayeyuka, wananchi wanafungua zaidi kimawazo na kimtazamo!
Lakini siyo kwa sababu vyombo vya habari vimekuwa huru zaidi ya wakati wa Magufuli. Sasa hivi tena ndiyo vimebanwa zaidi, hata kama siyo kwa njia za vitisho. Hiyo ndiyo hoja yangu.
Kama watu wanapanua wigo wao wa kujuwa mambo, siyo kwa sababu vyombo hivi vimewasaidia kufanya hivyo. Watakuwa wanatumia njia mbadala.
 
Ni kweli

Magufuli aliwachukua vibaraka wote wa CCM waliopandikizwa Chadema akawarejesha Nyumbani kwa mtindo wa kuunga Juhudi

Chadema imekuwa Huru sababu ya Magufuli lakini sasa tunarudi enzi za awamu ya 4 ambako wanaccm walijaza mapandikizi Chadema mfano Lema, Zitto na Wenje walikuwa mapandikizi ya Membe

Mdee, Bulaya, Freeman mapandikizi ya Laigwanani

Ndio sasa unasikia Lisu analalamikia rushwa Kutoka kwa jirani 😂😂
 
Kucheka kwa mambo 'siriusi' kama haya, siyo kicheko hasa, bali ni kilio tu cha ndani kwa ndani!
 
Mkorinto,

Kuna mtu anaitwa pascal mayalla alikuwa akisifu sana kuhusu ATCL
Uzi wake huu hapa.

Baadae akaja kuomba radhi kwa kusema kwamba hakuwa sahihi katika uzi wa barafu

Post in thread 'Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka'
Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

Kuna wakati watu wanasema si kwamba kupinga kinachofanywa na serikali ila kuna watu wana uwezo wa kutazama mbali.

Yapo wapi yale mapambio? Shirika limeendelea kupoteza kwa miaka mitano mfululizo tena kipindi magufuli yupo.

Penye ukweli pasemwe. Mzee wetu magufuli kuna vitu hakuwa sawa. Aidha ni ego aliyokuwa nayo au alitaka ufahari kwa namna fulani.
Unaweza mchukulia mayala kama msaka uteuzi au bendera fata upepo???huko kote anafiti.

Lakini wewe unatakiwa uwe na uhakika unahitaji nini usiwe kama yeye.
 
Ndugu yangu ni mbovu.
Kuanzia zile bombardia mpaka dream liner, ziko garage, zingine zipo hapo Dar na nyingine nje ya nchi.
Juzi hapa kati nimeiona Airbus moja kati ya zile nne hapo airport kwenye hangar moja hivi, injini zote zimeondolewa limebaki fupa tu. Najiuliza, hivi sisi watanzania kuna kitu tunaweza kufanya kwa ufanisi?
 
Kushughulika na CCM kunahitaji Movement siyo hivi vyama vya Ruzuku!
Samahani/Hapana.

CCM wamefika kwenye hatua ya kujimaliza wao wenyewe sasa. Hakutahitajika uwepo wa "Movement" tena.
"Self-destruction" inawatafuna ndani kwa ndani sasa.
 
Samahani/Hapana.

CCM wamefika kwenye hatua ya kujimaliza wao wenyewe sasa. Hakutahitajika uwepo wa "Movement" tena.
"Self-destruction" inawatafuna ndani kwa ndani sasa.
CCM haiwezi kujimaliza yenyewe kwa sababu pamoja na makundi yaliyoko bado wanaujua Utamu wa madaraka

Kwahiyo wataendelea kupeana nafasi Ili Mradi wabaki Madarakani
 
KQ inayopiga route ya America ina safari kila siku, we huoni ni hasara kwa ndege ya KQ kukodishwa siku nne. Hizo siku nne hiyo KQ inayopiga piga route za NBO-JFK Itaunda pesa mingi kuliko zile ingepata ingekodishwa na mtu binafsi.
 
Kwani lazima akodi?

Mbona Rais wa Zambia huwa anapanda kama Abiria 😃
 
Hadi sasa haieleweki Rais Ruto katika safari yake iliyobatizwa Jina la " Coming to America" alitumia kiasi gani kukodi ndege

Wataalam wa usafiri wa anga wanakisia Serikali imetumia Zaidi ya Ksh million 200 kukodi ndege hiyo Lakini Rais Ruto anasema Rafiki zake ndio walimkodisha ndege hiyo kwa gharama isiyozidi Ksh million 10

Mjadala ni mkali Citizen TV

Hapa ndipo nimemkumbuka yule Shujaa wa Afrika Dkt. Magufuli aliyetuachia urithi wa ndege za kutosha kuepuka mambo ya viongozi kukodi ndege kwa Marafiki

Mlale Unono 😃😃
Kwani Kenya hawana shirika lao la Ndege?
 
CCM haiwezi kujimaliza yenyewe kwa sababu pamoja na makundi yaliyoko bado wanaujua Utamu wa madaraka

Kwahiyo wataendelea kupeana nafasi Ili Mradi wabaki Madarakani
Pengine sikujieleza vizuri hapo.
Ninaposema "wanajimaliza", sina maana ya hayo makulaji yao wayaache; bali nina maana kwamba hayo makulaji yatakuwa matamu sana kiasi cha kuwamaliza wao.
Wamejisahau, hakuna anayestuka tena.
 
Back
Top Bottom