Ziara ya Ruto nchini Marekani inatufunza kwanini Hayati Magufuli aliamua kuimarisha ATCL

Eti mandege mabovu,ndege mumeachiwa nzima mnfanyia uzinzi tu mpaka zinaharibika mnamsingizia yeye??
 
Kuna tweet Ruto kasema wamekodi kwa sababu gharama ya kwenda na KQ ilikua kubwa sana waka opt kukodi.

Jionee hapa chini.
View attachment 3004218
Labda hiyo ndio atumie kama hoja although pia inamuumiza kwa hoja zingine mbili.

Moja, Kenya Airways ni kampuni ya umma, na Rais ni msimamizi wa mali za umma, hivyo kuliona hilo la KQ kuwa na gharama kubwa zisizoweza kueleweka kwa wakenya wengi bila kulitatua ni kuchangia kuliua hilo shirika.

Mbili, kama angetumia KQ basi pesa za hizo gharama zingerudi kwa wakenya, na hiyo ni pride na faida kwa taifa la Kenya.

Mwisho wa siku, je kulikuwa na ulazima wa kuwa na safari ya kwenda USA kwa ufahari na ukubwa ule? Mbona amesafiri mara nyingi nje ya nchi na gharama za safari zile hazikuwa ni agenda kubwa sana kuliko hii ya sasa.
 

View: https://vm.tiktok.com/ZMr1wD4ME/
 
Eti mandege mabovu,ndege mumeachiwa nzima mnfanyia uzinzi tu mpaka zinaharibika mnamsingizia yeye??
Usiwe mbishi ndugu.
Ndege zilianza kuzingua tangu Magufuli akiwa hai. Kosa sio waendeshaji na wasimamizi wa hizo ndege, kosa ni kitendo cha yeye Magufuli kulazimisha tender za ununuzi wa mandege kiholela tena kwa cash kabla ya ATCL kuwa na business plan. Kununua ndege ni jambo moja lakini kuendelea kuimiliki na kuitumia ni jambo lingine tofauti kabisa.

Kukupa mwanga tu, tatizo la ATCL halikuwa na halijawahi kuwa ukosefu wa ndege, tatizo lilikuwa ni muundo wa uendeshaji wake na usimamizi wake. Na mpaka leo hii halikuwa kutatuliwa.
 
Aliimarisha au aliiua ATCL? Hakuwa na mipango wala plans yeye alikuwa anajikurupukia tu. Bunge ndo think tank ya nchi lakini yeye alilipiga teke akawa ndo anapuyanga peke yake as a resuult kuna hasara kubwa sana mpaka CAG alijaraibu kual edit ili kumfichia lakini ikashindikana
 
Kumbe shida ni mfumo wa uendeshaji??mmejiandaaje ktk kumlaumu jpm hata ktk TRC ambayo nayo imejenga reli mpya na ununuzi wa train ya umeme??
 
Ruto alikuwa sahihi kusafiri na Ndege ya kukodi

Kenya Ndege zao zinaua viongozi mawaziri,Mkuu wa majeshi zonaanguka hovyo na kuua

Hata ningekuwa Mimi singepanda
Rais wa Zambia (ambaye hakuweza kujiita hata Hustler kwenye kampeni zake) mara zote akisafiri kwenda London, New york, Geneva, Paris, Tokyo, Shangai, Johannesburg, Addis Ababa amekuwa akipanda ndege za kawaida tena akikaa business class.

Ruto ambaye anajinasibu kuwa ni hustler anashindwa nini kufanya angalau hata nusu ya hayo?
 
Shujaa wako we shoga, lile lihutu lilikuwa baguzi, baguzi, liuaji, aligawa nchi. Mfuate akhera bwege we. Ndege imekodishwa amechangia mamako? Vimaskinu havinaga ht haya.
Nesi wa Kiyao wasalimie Wadada wenzako Hapo Tunduru 🐼
 
Kumbe shida ni mfumo wa uendeshaji??mmejiandaaje ktk kumlaumu jpm hata ktk TRC ambayo nayo imejenga reli mpya na ununuzi wa train ya umeme??
Tunamlaumu Magufuli kwenye ATCL kwa haya;
1. Aliilazimisha ATCL kununua ndege kubwa na nyingi wakati walikuwa hawazihitaji kwa wakati huo.

2. Aliingilia tender ya ununuzi wa ndege za ATCL hivyo gharama ya ununuzi ikawa kubwa maana wauzaji hawakushindanishwa.

3. Alinunua ndege mbovu na mtumba kwa bei ya ndege mpya.

4. Alinunua ndege nyingi, kwa haraka, kwa cash na hiyo imezaa hasara mara dufu.

5. Aliingiza ATCL katika mtego wa kutumia gharama kubwa kuzihudumia hizo ndege alizozinunua wakati ATCL haikuwa na uwezo huo.
 
Kumbe shida ni mfumo wa uendeshaji??mmejiandaaje ktk kumlaumu jpm hata ktk TRC ambayo nayo imejenga reli mpya na ununuzi wa train ya umeme??
Mambo ya ATCL na TRC ni yale yale, kote huko Magufuli alikosea, na usitegemee chochote kikubwa, kizuri au cha kudumu kutoka TRC kwenye SGR na treni za umeme. Ni miradi ya upigaji mtupu, haina faida yoyote kwa nchi au mlalahoi.
Kuanzia malengo, tender mpaka ujenzi wa SGR vyote havijakaa sawa, hivyo tutavuna mabua tu.
 
mtakwenda mtarudi, aliyoyafanya Magufuli hamtayafuta ng'o.
 
Inawezekana alinunua nyingi,hata juzi juzi tulipokea nyingine na inawezekana Bado zingine nyingi nyingi
 
Hizo ndege zimekufa baada ya kurithishwa madaraka na hichi kibibi.maana hakajui kuwaongoza watu wake.kila mradi ulioanzishwa na Magufuli Kwa Sasa zinakufa sababu ya kurithi li mutu la ajabu ajabu.
Katika hili nitamtetea Samia Suluhu kwa 100%. Hana kosa lolote, tutamlaumu bure.
Matatizo ya ATCL yalikuwepo kabla ya Magufuli lakini Magufuli ndio alikuja kuyachochea zaidi kwa kuleta mandege mengi makubwa na mabovu huku akitegemea ATCL iliyokufa iyaendeshe na kuleta faida kubwa. Na kusimama, kukamatwa na kususua kwa ndege za ATCL kumekuwepo tangu Magufuli akiwa hai madarakani.
 
Kwa kuendeleza, na je kama Rais, hajui kwamba huo ni mtego kwani jamaa wanaweza kumwendea kwa jambo lao fulani na hivyo akawa hana budi kuwalipa fadhila waliyomtendea?
 
Kenya Airways na ATCL ipi kubwa?
Uwepo wa shirika la ndege la taifa na Rais kukodisha ndege kusafiria ni vitu viwili tofauti.
Hoja hapa yaweza kuwa matumizi mabaya ya fedha za uma.
 
Pascal,

Msome barafu hapa chini. Huyu jamaa nilikuwa nampenda sana alikuwa anafanya critcal observation. Sijui tunapata wapi mtu kama yeye!

 
Mkuu Zanzibar,

Nimekuwa nikikufatilia wewe ni mtu mwenye madini sana.

Tatizo la ATCL limekuwepo tangu mzee magufuli akiwa hai. Shirika limepata hasara kwa miaka mitano mfululizo licha ya serikali kutoa ruzuku lakini bado shirika limeendela kupata hasara.

Hapa ndio nikamkumbuka barafu kwenye uzi wake β€œhizi kachumbari za ndege” akifafanua kwa kina.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…