Ziara ya Ruto nchini Marekani inatufunza kwanini Hayati Magufuli aliamua kuimarisha ATCL

Kwani lazima akodi?

Mbona Rais wa Zambia huwa anapanda kama Abiria πŸ˜ƒ
labda Zambia hawana ndege la rais. Pia ujue rais hasafiri peke yake huwa na delegation, kwa hivyo wakati aina ya usafiri inachaguliwa lazima wazingatie rais atasafiri na watu wangapi. Safari zingine zote marais wa kenya hutumia ndege la rais
 
Huna upeo
 
Magu alikua mshamba alikua anaogopa kupanda ndege nakingereza alikuaajui
 
Citizen tv.

Hv kwetu hata zamradi tv tu inaweza kuongoza mjadala mkali kam huo achilia mbali clouds na zinginezo? Je rais anaweza kujieleza?
 
You don’t believe that trash.

Labda kama unataka kuchokoza tena mjadala kuhusu dhana potofu ya β€œkufufua au kuimarisha shirika la ndege” kwa serikali kununua ndege kwa kutumia hela za walipa kodi. Tena bila feasibility analysis wala business plan. Kama vile tatizo la ATC lilikuwa ni kukosekana kwa ndege.

Halafu unazo taarifa za gharama zinazotumika hapa katika misafara ya Rais kwa kutumia hizo ndege za ATC? Unao ubavu wa kuuliza? Usiwacheke Kenya ambao mambo yao yanawekwa peupe na kila mtu ana uwezo wa kuchambua, kuhoji na kutoa wazo.
 
Ndugu yangu ni mbovu.
Kuanzia zile bombardia mpaka dream liner, ziko garage, zingine zipo hapo Dar na nyingine nje ya nchi.
Kama kweli ni mbovu yawezekana walikosa kuzifanyia matengenezo as per planned maintenance schedule.
Na hii inatokana kuendesha shirika kwa miemuko tu.
Kilichouwa mashirika ya Nyerere ndio hicho hicho kitaisambaratisha ATC .
 
Kile Kikundi Chenu Kinachotaka Kuikodisha ATC Kwa Akina Habib Kinaendelea Ama
 
Watu wanadai ATCL imefufuliwa na inazidi kuimarika!

Sijui kama wana hata uelewa wa abc za shirika kuthaminika kama β€œgoing concern”. Sijui kama hata wanajiuliza ATCL ya sasa ina TOFAUTI gani ya msingi na ATC ya nyuma?
 
Watu wanadai ATCL imefufuliwa na inazidi kuimarika!

Sijui kama wana hata uelewa wa abc za shirika kuthaminika kama β€œgoing concern”. Sijui kama hata wanajiuliza ATCL ya sasa ina TOFAUTI gani ya msingi na ATC ya nyuma?
Shirika la serikali kwa 100% halipimwi Earnings zake kama ufanyavyo kwenye biashara binafsi mfano Shabiby πŸΌπŸ˜‚
 
Shirika la serikali kwa 100% halipimwi Earnings zake kama ufanyavyo kwenye biashara binafsi mfano Shabiby πŸΌπŸ˜‚
Jibu la uswahili hili. Tofautisha Kati ya mashirika ya msingi na ya kibiashara. Halafu, kwako wewe, tofauti ya ATCL na Shabiby ni ipi?

Usafiri wa anga ni huduma ambayo inaweza kutolewa na sekta binafsi serikali ikabakia na jukumu la kuimarisha miundombinu na usimamizi (regulation) tu.

ATCL haliwezi kustahili ruzuku ya serikali kama suala la kudumu la kisera. Halina justification ya kuendeshwa kwa hasara na ruzuku. Itakuwa mzigo mkubwa usio wa lazima kwa walipa kodi. Mapato yake lazima yapimwe kama a going concern. Angalau i-break even basi.

Ikishindikana ni kubinafsishwa tu. Ndicho kinachofuata. Soma yanayoendelea katika SA na KQ.

Huduma za abiria kwenye treni, vivuko na usafiri jijini zinaweza kupewa ruzuku kama namna ya kupunguza makali ya maisha na kuongeza ufanisi wa mizunguko (mobility) kwenye maeneo yenye changamoto ya usafiri.
 
Tanzania ni Nchi ya Utalii wa kila aina so Ndege zetu za ATCL zaweza kuwa kama Promo tool tuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ni kama MO Dewji anavyotumia Jezi za Makolo FC kujitangaza 🀣🀣
 
Tanzania ni Nchi ya Utalii wa kila aina so Ndege zetu za ATCL zaweza kuwa kama Promo tool tuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ni kama MO Dewji anavyotumia Jezi za Makolo FC kujitangaza 🀣🀣
Zaburi 1:1-2

Heri wasiojifungamanisha na β€œmashujaa” watenda mizaha katika mambo yanayoliangamiza taifa.
 
Jamani muonee huruma wenye akili nchi hii, ni watanzania wenzetu pia. Nyuzi kama hizi zinaumiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…