Ziara ya waziri wa China East Africa yaipa Tanzania viwanda 200


Mkuu pamoja na mapungufu ya wenzetu ya hapa na pale lakini wakati mwingine sisi kama Taifa tunapashwa kuchukulia ushauri wa Wakenya Seriously - MK254 kwa mfano: amesema siku hizi hakuna cha mahusiano ya kindugu au nini sijui, wawekezaji wanacho tafuta ni kupata faida kubwa na hii hajalishi kama muwekezaji ni Mchina au Mzungu, cha muhimu ni wewe kuji-tune jinsi ya kudeal na muwekezaji ili hasikuzidi akili, kinacho hitajika ni kuweka mizingira ya win win situation at all times.
 
Safi sana ila kwenye mikataba suala la kodi na ajira muliangalie vizuri,isije ikawa waajiriwa wazawa n asilimia kumi wanaobakia wageni.

Kwenye kutafuta wawekezaji sisi ndio tunatakiwa kufaid na uwekezaji zaid mana tuna arthi,malighafi na cheap labour.

Viva nchi ya viwanda
 
mnaojua hesabu jumla Tanzania itakuwa na viwanda vingapi?
hapo mnanichanganya sasa, mkisema kiwanda, mnamaanisha kampuni au factory...... mi naelewa kiwanda ni factory ama plant....na sioni vile mnaeza jenga viwanda zaidi ya 1800 kwa mwaka mmoja na tanzania iwe haijulikani hapa africa kwa mambo ya industrialization/manufacturing..... unless huyo waziri alikua anahesabu hata wafanyikazi wa juakali na fundi wa mbao..... manake kama mnaeza jenga viwanda 1800 vya maana kwa mwaka mmoja, basi hivyo 200 vitakavyojengwa na wachina kwa miaka minne (2017-2020) si kitu
 

pia sisi tuko na changamoto tele huku kenya, number 1 ikiwa ni ufisadi.... lakini siku zote hata hao wafisadi wanaelewa, lazma kufanyike kitu, lazma pesa zitumike kwa project ilioahidiwa hata kama watazila nusu lakini ni lazima waifanye manake kama hawatakuza uchumi basi kesho kutakua hakuna lolote la kufaidika kwa uchumi...... ndo maana hata kama viongozi wetu na wabunge wengineo hapa kenya wanajulikana kupenda ufisadi... si rahisi kuwaona wakipinga uwekezaji au biashara...siku zote hua wako investor friendly .... wataeka kila kitu ambacho hatuna kwenye shoppinglist, wataweka campeni kali kuvutia wawekezaji alafu wanategemea hapo kwa hizo dili watapata kafaida , kwahivyo biashara lazma ziendelee kulingana na hao


kwahivyo lazima tuvutie wawekezaji wa vitu muhimu, policies za biashara ziboreshwe, ...yani at the end of the day things get done , we would have moved from point A to point B cause if we stop moving, everyone looses, as you might know, kenya i depends on its people for the economy (agriculture, service industry,manufacturing) , we have leant the hard way what happens when you stop moving
utakuta viongozi wanapiga kelele nyingi lakini ukiketi nao kuongea biashara/uwekezaji, wanageuka na kuwa sober
 
Mkuu, kama huu ungekuwa ushauri wenye mashiko, ningeuelewa. Lakini kama muda mwingi anautumia kumwaga vijembe kwamba Tanzania wajinga na hawajui walifanyalo siwezi kuelewa. Kama tusinge kuwa makini si tunge saini EPA? Kama tusinge kuwa makini, tungekuwa tumejiunga na single visa muda wote huo? Kama tusinge kuwa makini, leo hii Bologonja Border ingekuwa imefunguliwa?, Kama tunge fanya vyote hivyo nani ange baki analia? Tanzania tungebaki tunalia. Juzi tuu walitukata kiaina kwenye reli wakakimbiza mbali na Arusha, huku wakitukebehi kwamba tuna warudisha nyuma kwenye EAC? Tumekuwa na uhisiano na wachina kwa miaka mingi sana, na kama ulishawahi kusoma historia yetu na wachina ungeelewa nini kinazungumzwa.
 

Mkuu ndiyo maana nimetanguliza neno la "PAMOJA NA MAPUNGUFU YAO" lakini once in a while Wakenya uzungumza/shauri vitu vyenye mshiko - tuchukue ushauri wenye maana kwetu tupuuzie maoni yao mengine ambayo hayana tija kwetu. .
 
Mkuu ndiyo maana nimetanguliza neno la "PAMOJA NA MAPUNGUFU YAO" lakini once in a while Wakenya uzungumza/shauri vitu vyenye mshiko - tuchukue ushauri wenye maana kwetu tupuuzie maoni yao mengine ambayo hayana tija kwetu. .
Hivi huyu MK254 umesikia leo jana?. Kwanza yuko wapi, aje hapa atuambie ushauri wake unakwendaje na maneno aliyo tuponda nayo huko nyuma? Mk254, anapo ponda Tanzania na kusema ni aibu kwa Afrika, li-nchi kubwa na bado masikini leo hii ndio tukae tuone anatushauri. Labda wewe kama unataka kumsikiliza, mimi namjuwa, anakujaga Tanzania anakula bata, akiondoka anaondoka na gunia zima la kashfa za kuwapa Watanzania.
 
Post kama hizi ambazo kizalendo kabisa tulipaswa ndio tuchangie kwa kupongeza eti ndio huoni watu. Halafu zile post za kijinga na za kipuuzi ndio unakuta mijitu inatoka jasho kwa kutokwa na mitusi.

Vijana wengi wa ufipa ni shilawadu
 
Zito Kabwe na ndugu zake wa chadema wakisikia hii habari wanaweza kufa kihoro kwa chuki, na kwa kuongezea pia mvua zimeanza kunyesha hivyo hakuna baa la njaa!
zitto kabwe hayupo chadema bwana
 
This is another fuc..n African move,
Tutaendelea kuliwa mpaka mungu arudi, viwanda 200 na ufala mwingine, whem r we going to wake up? When r we going invest in China,? how long we r going to stay cowards., and bastards.
I thought our government is focusing to develop our local things experts and technicians, tuanzie chini, tuwe focused, tuwe strategized, tuwawezeshe na tuwape nafasi wabunifu wetu, hata ikichukua 50yrs we might have our own technology but it have to start from the bottom,
I really hate, and I hate this methodology, Chinese are enjoying our Natural resources ***** we are remaining poor. Ufala huu.

We can manufacture a lot of things locally if we need to..
 

Mkuu hilo lisikupe shida, kama umesona vizuri masuala ya saikolojia comments za MK254 aziwezi kukupa shida, lakini wakati mwingine anatoa maoni/ushauri wenye mantiki kwa kutumia abbrasive language.

Deep down hana Tatizo na Tanzania ndiyo maana anaitembelea mara kwa mara, yeye anasema anakuja huku kikazi, wakati fulani aliamini kwamba Tanzania hakuna watu wanaweza kufanya kazi zake na wana ujuzi na exposure kuliko ya kwake, siku hizi ameshika adabu kidogo baada ya kupigwa maswali yenye mitego welevu wakagundua janja yake, otherwise hana tatizo na mtu ni kihasi cha kumuelewa na kwenda naye sambamba.
 
Mmm, haya mahaba kwa MK254 siyo ya spoti spoti, bila shaka wakenya wamepata mtetezi. Au na wewe mkenya ulie vaa koti la mtanzania? Tujuze yakhe
 
Acha kurukia habari bila kuzielewa wewe jamaa, alisema viwanda 200 afrika nzima na TZ ikiwemo.
 
Mmm, haya mahaba kwa MK254 siyo ya spoti spoti, bila shaka wakenya wamepata mtetezi. Au na wewe mkenya ulie vaa koti la mtanzania? Tujuze yakhe
Unajua ndugu baadhi ya watu humu wanashangaza sana. Ukianza kwenda nao point to point unawakuta hola. Lakini wanaongea hao!!!
 
Unajua ndugu baadhi ya watu humu wanashangaza sana. Ukianza kwenda nao point to point unawakuta hola. Lakini wanaongea hao!!!
Mimi nilikuambiga kitambo kuna mabomu yaliyotegwa ardhini, from time to time, yanajilipua yenyewe huna haja ya metal detectors.
 
Mmm, haya mahaba kwa MK254 siyo ya spoti spoti, bila shaka wakenya wamepata mtetezi. Au na wewe mkenya ulie vaa koti la mtanzania? Tujuze yakhe

Mbona unanishangaza, yaani kujieleza kwangu kwote unajielewa!!!

Nimesema baadhi ya Wakenya wana mapungufu yao hasa kwenye masuala ya PR, lakini si wote - mkuu usisahau kwamba Taifa lao ndilo limewekeza sana Tanzania na kuajili Watanzania wengi kuliko Mataifa mengine - kumbuka vile vile kwamba linapo kuja suala la ushindani wa kibiashara kinacho tumika pale ni law of the jungle - hakuna cha urafiki, ushikaji au u-komredi kila kitu it's everyman for himself and God for us all - don't you forget that.

Tatizo letu kubwa Watanzania hatujazoea modus operandi za namna hiyo, lazima tujifunze kuwa aggresive na si kutegemea/letewa kila kitu on a silverplate.

Haya ndiyo mambo MK254 anatukumbushaga kila siku ingawa lugha yake wakati mwingine inaonyesha kama anatudharau vile - sisi tuchukue yenye mshiko tuachane na yale yasiyo na tija kwetu - hicho ndicho nilikuwa namaanisha.
 


hapo umeongea kama wazee saba!
hua nafikiria hivyo kabisa! hua nashikwa na kawazimu hivi nikijiuliza kwanini hua hatuanggalii bigger picture.... kama tungeanza miaka ya 70, sahii ingekua tumepiga hatua... tukianza sahii ikifika kama 2035, tutakua tuko na chetu.........

hata haina haja tuanzie mbali, kuna vile vitu mi hua naita, small wins, tuanza na hivyo angalau, vile vifaa na vitu ambavyo tukitengeneeza, ni guarantee kwamba tunahitaji na tutavitumia... vitu kama viatu vya wanajeshi, au bullet proof vest, citlary,vitu vya jikoni, cable na sockets na glop za stima, hata street lights, spare part za gari ambazo ni nyingi nchini mwetu- Toyota, ......nak...... bidhaa kama hizi na nyenginezo ni bidhaa ambazo zinanunuliwa kila siku na zinahitajika, tujenge makampuni ya kutengeneza bidhaa kama hizo alafu tuongeze ushuru kwa bidhaa za nje ziwe hazinunuliki ...

tunafaa tuwekeze pesa nyingi sana kwa mambo ya utafiti.... duniani, ni bara la africa ndo liko nyuma zaidi kwa uwekezaji wa itafiti, alafu kila siku tunashangaa kwanini hatuundi chochote cha maana
 
Unajua ndugu baadhi ya watu humu wanashangaza sana. Ukianza kwenda nao point to point unawakuta hola. Lakini wanaongea hao!!!

Hilo ndilo tatizo kubwa la watu wenye analytical mind ambayo ni borderline, amuoni beyond your noses - siasa tuu masaa yote, mtu mwenye akili tinamu awezi ku-ignore uwekezaji wa Kenya nchini ambao ume-create imployment kwa Watanzania wenzetu - siyo kila siku tunazungumzia ubaya wa Wakenya tuu, tuwapongeze pale wanapofanya vizuri na sisi tujifunze kutoka kwao, Dk.Magufuli alikwenda Kenya for good reason sasa sijui kwa nini sisi hilo hatulioni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…