Mheshimiwa waziri
Dkt. Gwajima D kabla ya yote ningependa kwanza kutumia nafasi hii kukupongeza kwa kazi kubwa unayofanya yenye tija na manufaa kwa taifa lako na wananchi wenzako mmoja wapo nikiwa mimi.
Mheshimiwa mimi binafsi nimekuwa nikiona juhudi kubwa unazofanya ktk kupambana na vitendo vya kikatili katika jamii, pamoja na mauaji ya mara kwa mara yanayofanywa dhidi ya watoto wetu na ndugu zetu. Ki ukweli hayo mambo huwa yanaumiza na kusikitisha sana. Lakini niseme kuwa mara nyingi vitendo hivyo huwa vinachangiwa zaidi na sheria zetu ambazo adhabu zake nyingi haziendani na kosa husika, au kama zinaendana basi utekelezaji unakuwa sio mzuri.
Nafikiri ili kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la mauaji ya kiholela hasa kwa watoto wetu inatakiwa sheria za hukumu ya mauaji zibadilishwe. Mtu anaepatikana na hatia ya kuua basi hukumu yake itekelezwe hapo hapo bila kusubiri mpaka saini ya raisi.
Hili swala la mtu aliepatikana na hatia ya mauaji kusubiri hadi saini ya raisi ndo ahukumiwe, ndio limesababisha wauaji wengi kuendelea kula bata na kuliongezea taifa hasara ya kuwahudumia wauaji ambao wengi wao huwa hawakumbani na adhabu yao ya kunyongwa, bali hukaa gerezani mpaka siku Mungu mwenyewe atapoamua kuichukua roho yake. Hivyo kusababisha watu wengi wenye mioyo ya kikatili kuendelea kufanya mauji kwa kuamini kwamba hata atapokamatwa na kuhumiwa kunyongwa, uwezekano wa yeye kukutana na adhabu hiyo ni mdogo sana. Sana sana atakaa tu jela na kukosa ule uhuru wa kuwa uraiani, kuonana na ndugu zake, kuwatembelea jamaa zake nk.
Tukianza kuhesabu toka hukumu ya kunyongwa ilipotungwa hadi leo weshahukumiwa wangapi, sidhani kama tutapata hata watu 50. Mfano sidhani kama baba wa taifa hayati mwl Nyerere aliwahi kusaini watu wangapi wanyongwe, marehem mzee wetu mzee Mwinyi, hayati mzee wetu mzee Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa mhe raisi Samia? Ni wauaji wangapi ambao wameshahukumiwa na maraisi hao sita toka awamu ya kwanza mpaka hii ya sita?
Uzoefu unaonesha kuwa kila raisi anapoingia madarakani hukwepa sana jukumu hilo la kusaini kunyongwa kwa wauaji, hivyo kusababisha wahalifu wasiiogope hukumu hiyo ya mauaji maana haitekelezwi ipasavyo. Haiwezekani mtu akipatikana na hatia ya kuiba, kubaka, kupigana, kuuza madawa ya kulevya nk ahukumiwe hapo hapo mahakamani na kuchukuliwa na askari magereza ili akaanze kutumikia hukumu yake, halafu muuaji yeye akishahukumiwa asubiri mpaka raisi aamue utekelezaji wa hukumu yake na wakati huo huo raisi mwenyewe hakuwepo wakati wa kutolewa hukumu.
Nafikiri ni vizuri mtu anapopatikana na hatia ya mauaji na kuhumiwa na hakimu basi hukumu hiyo ianze utekelezaji kwa mhalifu kupewa muda fulan mfano week au mwezi kwa ajili ya kukata rufaa, kuagana na ndugu zake nk, baada ya hapo mhalifu ahukumiwe kwa kunyongwa bila hata kusubiri saini ya raisi. Maamuzi ya mahakama na ushahidi uliotumika kumkuta mtuhumiwa na hatia vitumike kuhalalisha hukumu hiyo kwa muda tu wa week au mwezi mmoja baada ya muuaji huyo kukutwa na hatia.
Naomba ulifanyie tathmini hili swala na ukiona linafaa na kuweza kusaidia katika kukomesha mauji ya watoto wetu, na watanzania wenzetu basi ulipeleke bungeni ili kubadilisha sheria ya hukumu ya kifo iliyopo sasa.
Bila hivyo kama nchi tutaendelea kupambana na tatizo ambalo itakuwa ngumu kulimaliza.