Ziara yangu ofisi za JamiiForums

Ziara yangu ofisi za JamiiForums

Sema hii bonge moja la picha..

G2.jpg


Kama kwenye hii picha Active upo, Jumapili mnapigwa na Spain. Shahidi Greatest Of All Time na Dr Restart
 

Wasalaam Wanajukwaa wenzangu.

Mapema tarehe 12 Julai, 2024 nimetembelea Ofisi za Jamii Forums kama mojawapo ya taasisi inayojihusisha na habari za kijamii. Lengo la ziara ni kuweza kufahamu shughuli za taasisi hii na kuona namna ya kushirikiana Ili kupanua wigo wa kuifikia jamii kidigitali.

Kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, tumejadiliana kuhusu umuhimu wa kushirikiana kwenye mada za kuifikia jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa jamii kwa ujumla na hususan, kupambana kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa watoto.

Kama mwanachama hai wa JF na aliyethibitishwa, niko tayari kuendelea kupokea mawazo na changamoto kutoka kwa wananchi kupitia mitandao ya kidigitali ambayo kimsingi inarahisisha sana mawasiliano na wananchi.

Hivyo, nawakaribisha nyote kunitumia mawazo mbalimbali na changamoto kwani, ushirikiano wa jamii ni muhimu kwa maendeleo.

Ahsante sana Mkurugenzi wa JamiiForums Maxence Melo (ninayesalimiana naye) na timu yako yote🤝

Mungu awabariki 🤝🇹🇿 na awabariki wanajukwaa wote🤝

Hunaubaya mama Yetu Allah akupee neema yake utukumbukee kina pdidy hukombelen ammen
 
Back
Top Bottom