Zidane au Xavi, nani alikuwa bora?

Zidane au Xavi, nani alikuwa bora?

NUMBERS DONT LIE

ZIDANE
GAMES:820
GOALS 103
ASSISTS 92
TROPHIES 11

XAVI HERNANDEZ
GAMES 767
GOALS 108
ASSISTS 204
TROPHIES 28

#IN THEIR PEAK XAVI WAS BETTER THAN ZIZOU....!!!


Naona mimi ndiye zaidi ya hawa jamaa kwani nimeona mechi zao zote na kuassist mechi nyingine pia. Nilikunywa vikombe vya bia (trophies) visivyohesabika na kupiga magoli (kukojoa) ya hajabu si chini ya elfu kadhaa.
 
Wacha bwana kipindi hicho kwa hisani ya TVZ. Ni fainali ambayo mambo ya LIBERO yalitokelezea kwa sana haswaa shughuli aliyokuwa akiifanya LOTHAR MATHEUS wa WEST GERMANY MASHINE! Argentina ikicheza tofauti kabisa na mwaka 1986 ikija na sytle ya kupaki basi ila wabrazil walilia sana walivyolizwa na kombinesheni ya CANIGIA na Maradona dakika za robo ya mwisho ingawa SAMBA ilipigwa zaidi ya asilimia 80. Mwisho ni uamuzi wa mpiga penalti mashuhuri ANDREAS BREHME wa W. Germany dhidi ya golikipa nguli mwenye macho ya mwewe ya kuokoa penalti wa Argentina GOYCOCHEA.

Msimfananishe hata kidogo hawa akina Messi na Ronaldo na Kizazi cha Pele au Maradona. Sana sana vita itakuwa nani zaidi kati ya PELE na MARADONA.

Kipindi hicho kilikuwa hakuna 'protection' kwa mastaa watu walikuwa WANAKULA MIWA HASWAA. Siku ukutane na URUGUAY hiiii hiii la UAKIKA kwanza unajua watabakia SABA uwanjani. Lakini Maradona alikuwa anakimbiza humo humo pamoja na KULIWA MIWA.



Maradona alikuwa mshenzi *****.anakokota kijiji kizima kama 2navyomuona mdogo wake king leo Messi. Argentina imebalikiwa aise. Wanamajembe yaloenda shule bwana. Achana nahao mbirimbi.
 
Xavi wasnt better than Zizou,ubora unaonekana hata ukihama timu moja kwenda timu nyingine.Xavi ameenda timu ipi nyingine akaproove bado ni bora?Diego folan kuna Man U alichemsha.Angalia Claude makelele hata alipohama Real kwenda Chelsea alifanya kazi yake ile ile.Zizou was the best!
Haaa...kwa Messi hajaenda nje ya Barcelona but ni habari nyingine kila mtu anajua...
Zidane is the best
 
Zizzou bila ubishi!

Hata 'impact-wise' naamini alikuwa nayo kubwa kuliko Xavi ingawa haimaniishi Xavi ni mbovu.
 
Zizou ni habari nyingine
Xavi ni kule tu kupiga pasi nyingi kulikotokana na mfumo na utamaduni wa Catalunya ila kipaji asilia Zizou ni fundi haswa.
Nina mafundi wangu asilia wengine ngoja niwaongeze hapa :
1.Gaucho - Brazil
2.Riquelme - Argentina
3.Redondo - Argentina
4.Gascoigne Paul Gazza - England
5.Hussein Aman Masha - Tz ( Ingawa hafahamiki huko duniani ila mimi nilimuelewa sana those days )
6.Edibily Jonas Lunyamila ( Nitaendelea kumuelewa mpaka kesho hata kama hafahamiki huko duniani)
 
unataka namba?

-zidane ni mchezaji bora wa miaka 50 iliopita wa ulaya (xavi pia ni wa ulaya)

UEFA Golden Jubilee Poll - Wikipedia

-ana baloon d or moja xavi ana kibuyu

-fifa player of the year mara 3 xavi ana kibuyu

-kila fainali man of the match yeye (kasoro 2006 ambayo alimpiga mtu kichwa), na sio man of the match tu bali anakuwa mchezaji bora wa michuano. nikukumbushe

1. 1998 huyu jamaa aliwafunga brazil goli mbili fainali akawa mchezaji bora wa michuano na man of the match fainali

2. mwaka 2000 mchezaji bora michuano EUro

3. 2002 anakosekana ufaransa wanatoka makundi world cup

4. 2006 anarudi world cup ufaransa wanafika fainali, kama sio ile red walikuwa wanabeba tena na mwanaume anabeba tena uchezaji bora.

kwenye club hivyo hivyo mpaka leo goli lake la 2002 la fainali ni moja ya magoli bora kupata tokea.

sasa jiulize mkuu ana magoli machache ila kwanini muhimu sana? siku madrid wakimfunga sijui getafe goli 9 wala zidane hatafunga matano, zidane anakuja kufunga ile mechi ngumu kabisa mechi ambayo mbinu zote zimeshindikana na kila mchezaji kakamatwa ndio zidane utamuona.

jamaa alikuwa hategemei mfumo wa timu, yeye ndio mfumo na ile chenga yake (ya michael laudrup) alikuwa akizichachafya midfield bora duniani, nenda youtube kaangalie france 1 brazil 0 world cup 2006 utajua zidane ni nani, midfield ya dunia kina dinho wapo form walikuwa wakiutafuta mpira.

xavi yeye alikuwa mtegemeaji mfumo, wafunge kina messi, siku barca kashinda 6 basi na yeye atupie mbili, siku mou au chelsea wakipaki basi na yeye haonekani, siku getafe wakikomaa na yeye haonekani, siku rubin kazan wakipiga buti na yeye haonekani etc.

hebu mkuu taja memorable moment za xavi anaamua mechi ya fainali au ana dictate mechi muhimu sana, kama vile zidane fainali zote kubwa yaani UEFA, EURO na World cup.


na pia usisahau point moja ya mwisho zidane anakuwa mchezaji bora wa dunia mara 3 wapinzani wake ni
1. Ronaldo de lima
2. Rivaldo
3. Ronaldinho
4. Figo
5. Beckham
6. Henry
7. Michael owen
8. oliver Khan
9. shevchenko
10. raul etc

kila timu ukigusa kuna watu balaa, yani ikija kuchagua nani bora hata hujui nani anashinda, tofauti na sasa ambapo wachezaji waliodumu kiwango kikubwa ni wawili tu.
Naomba mjadala ufungwe hapa. Umemaliza kila kitu hapa.
 
mwaka ule wa 98 kila mtu zidne wa ufaransa hadi kina mama wakapenda mpira duhh zizzou huyu

Miaka ile wabongo wengi tulikuwa ni washabiki wa Brazil, kwa sababu ni timu ilikuwa na record nzuri na ilikuwa na weusi kadhaa, bila kusahau kwamba timu ilikuwa na Ronaldo de Lima ambaye ndo alikuwa nuru kipindi hicho.

Ile game Zizzou anapiga magoli yale mawili lakini bado tunaamini yatarudi tu, mpaka Emmanuel Petit anafunga goli la tatu ndo tukakata tamaa, mi nilikuja kunyoosha mikono Euro 2000, mzee mzima akiwa na kampani ya Thiery, Wiltord, Trezeguet, Vieira, Pires, Thuram...

Nakumbuka Spain na Italy walivyoteseka chini ya Zizzou.
 
Wacha bwana kipindi hicho kwa hisani ya TVZ. Ni fainali ambayo mambo ya LIBERO yalitokelezea kwa sana haswaa shughuli aliyokuwa akiifanya LOTHAR MATHEUS wa WEST GERMANY MASHINE! Argentina ikicheza tofauti kabisa na mwaka 1986 ikija na sytle ya kupaki basi ila wabrazil walilia sana walivyolizwa na kombinesheni ya CANIGIA na Maradona dakika za robo ya mwisho ingawa SAMBA ilipigwa zaidi ya asilimia 80. Mwisho ni uamuzi wa mpiga penalti mashuhuri ANDREAS BREHME wa W. Germany dhidi ya golikipa nguli mwenye macho ya mwewe ya kuokoa penalti wa Argentina GOYCOCHEA.

Msimfananishe hata kidogo hawa akina Messi na Ronaldo na Kizazi cha Pele au Maradona. Sana sana vita itakuwa nani zaidi kati ya PELE na MARADONA.

Kipindi hicho kilikuwa hakuna 'protection' kwa mastaa watu walikuwa WANAKULA MIWA HASWAA. Siku ukutane na URUGUAY hiiii hiii la UAKIKA kwanza unajua watabakia SABA uwanjani. Lakini Maradona alikuwa anakimbiza humo humo pamoja na KULIWA MIWA.
Now am talking to someone who watched soccer at its Best.Baada ya hao watu ndio kina Zizou watoto wa jana wanazungumzia soccer leo,mchezaji akiguswa anajidondosha eti wanalindwa.Usenge mtupu.
 
Kwahyo point yako ya kumsupport zidane ni kuhama timu au sio ..... rekebisha hapo kwanza au utuambie kwamba zidane ni bora kwasabab kahama(tuthibitishe ujinga wako) ndio tuendelee ... NI HOJA YA KIJINGA HYO NA IMENIKWAZA SANA YAN .
Umeanza kuangalia mpira lini?kuna ligi ni laini na ligi ni ngumu kijana.Ili uwe bora lazima uonekane kwenye ligi tofauti uwe na watu tofauti kwenye combination,uonyeshe kuibeba timu.Ujimga wako wakusoma mwanaspoti,bingwa na kuenda vibanda umiza usiulete humu.
 
5.Hussein Aman Masha - Tz ( Ingawa hafahamiki huko duniani ila mimi nilimuelewa sana those days )
6.Edibily Jonas Lunyamila ( Nitaendelea kumuelewa mpaka kesho hata kama hafahamiki huko duniani)

Mkuu kweli wewe ni mpenzi wa soccer, mimi ni mshabiki wa Simba damu ila kwa Lunya Lunya sina ubishi, alikuwa akishika tu mpira nazima radio, baada ya dakika kama mbili ndo nawasha kusikiliza kama hakijanuka, maana ile "Lunyamila, anapiga chenga ya kwanza, ya pili, anakuja Kasongo Athumani kumkaba anakula chenga, etc etc" ilikuwa inanipa presha.

Hussein Aman Masha hajawahi kutuangusha wana Simba wala Taifa Stars, kama kiungo au mkoba, penat hakosi hata uweke makipa wanne golini.
 
Baada ya Pelle na Maradona!Kipaji halisi ni Ronaldo De Luis Nazario Lima (The Phenomenon)ndicho kipaji halisi kilichowahi kutokea katika uso wa dunia katika karne za karibuni labda kidogo Ronaldo De Asis Moreira a.k.a( Ronaldnho )alijaribu kukikarbia kipaji cha Lima...kina Zidane na hao kna xav plus current Messi & Chrstiano Ronaldo zlkua mvua za msimu kutegemea wameamkaje au wamecheza na nan..nmemaliza ....haya ata Ibrahimovic aliwahi kukiri
 
kwa kizazi chetu cha 80`s hatutokaa tumuone mchezaji mwingine ka ZIZOU,acheni kumlinganisha ZIDANE na vitu vya kijinga,hasa kama umewahi kumwona anvyochezea ngozi ya ng`ombe ila kama umesimuliwa tu hauwezi kutuelewa hapa tunachomaanisha...
 
Back
Top Bottom