Zielewe kazi za Usalama wa Taifa (TISS) na mipaka yake

NATAKA nijunge usalama nafanyaje kaka
Wengine hawaitaki hio kazi wanasema ni ya kimbea mbea sana.
Working for Killers is a sure way of booking a place in Hell
 
Au kuna watu anataka awavimbie, awalipe visasi au wamuogope... Wacha upumbavu! Hao watu ni Choosen from god!

Haipatikani hiyo status kizembezembe!
Hakuna lolote na wala si chochote!
Hao tunaowatambua kuwa wanahusika na matendo mabaya ya kishetani nao wamechaguliwa na Mungu ili watende hayo matendo mabaya??

Kila mtu unayemuona hapa duniani tambua ya kwamba amechaguliwa na Mungu ili awepo hapa duniani, lakini siyo hao tu peke yao ambao wewe unadai kwamba wamechaguliwa na Mungu
 
Shukrani sana ,hakika umetufungua macho sana ,sina shaka maana Late Membe naye alikuwa mtu wa KITENGO hope ulipata madini mengi kutoka kwake.

Ni wazi SHUSHUSHU hawezi kujitangaza akiwa bar ,hao wanaojitangaza ni wehu tu wachukue mabar medi.

DAB alikuwa anaongoza GENGE la UHALIFU lakini walikuwa siyo "TEETH".
 
Uzi bora kwa mwaka 2024
 
Kwahiyo hata mtu aliyeko kazini na hajui chochote kuhusiana na ushushushu kivipi anakuwa recruited? Umeniacha hapo ila kwa chuo na mashuleni hiyo naelewa
Hakuna aliyezaliwa shushushu. Wanajifunza na wanapelekwa chuoni. Wengine walikuwa madereva sasa wamo huko idarani, wengine ni wakulima tu wengine wapiga kiwi viatu.
 
Umesema kwenye majukumu ya TISS ni kuripoti, juu ya matishio ya usalama ya ndani na nje!
Swali langu je TISS, hawawezi kuwajulisha serikali juu ya mikataba mibovu wanayoingia? Au Siyo majukumu yake?
Pili, Kama wanafanya kazi kwa maslahi ya Serikali na Siyo nchi ni hatari Sana.
 
MI ipo ndani ya wigo wa TISS
Mkuu Military intelligence ( MI) ni tofauti na TISS.

MI ni kitengo Cha upelelezi wa kijeshi ambacho kinatumika kupeleleza mambo ya kijeshi tu dhidi ya maadui wa kijeshi kuhusu yafuatayo:-
1. Uwezo wa adui kijeshi
2. Silaha za adui
3. Hali mazingira ya uwanja wa vita
4. Maeneo muhimu ya kimkakati ya kijeshi ya adui.
5. N.k

MI ni muhimu sana jeshini kwa kuwa ndiyo idara inayowawezesha makamanda wa vikosi kupanga vita na mashambulizi kwa adui kwa usahihi na taarifa sahihi.

Kwa masuala ya kiusalama ndani ya nchi TISS na MI hushirikiana kwa karibu ingawa ni matawi mawili tofauti ya kiusalama.

TISS ni kazi Yao ni kama ulivyoeleza.
 
Ungenielewa vizuri nilichoandika ungejua kwamba ulichosema hakina tofauti na nilichosema. TISS ni kubwa kuliko MI, kwa maana kwamba MI ipo ndani ya TISS. TISS sio MI, lakini MI ipo ndani ya himaya ya TISS. Na ndio maana TISS imepewa jukumu la kushirikiana na taasisi yeyote ndani ya nchi katika shughuli zake.

Narudia, MI ipo ndani ya himaya ya TISS. Vinginevyo dola yeyeto haiwezi kudumu zaidi ya masaa 48.
 
Nimeupenda Uzi na unaeleweka vzr ila Nina maswali madogo nataman kufahamu Je

1: Mleta Uzi ni miongoni mwa Teeth au unamaarifa tu kuhusu Teeth ?
Maana hapo chini naona Hadi namba za simu na email kiasi Cha kufanya mtoa comment fulan Kuomba kuunganishwa na kifurushi kama inawezskana 🙏

2: Kama jibu ni Yes yaani ni mwanachama je hii inaweza ikawa ni miongoni mwa njia za recruitment ya kupata walengwa ?🙏
 
Hahahahah sasa swali la kizushi linapataje jibu lisilo la kizushi? Niseme tu kwamba nadharia hiyo ndio kwanza nasikia kwako, sijui kwamba wamwera wengi wako huko.
Hao ni kweli wapo wengi sana, Toka enzi ya Nyerere, wengi wao ni wasemianari waliotaka kuwa makasisi wa kanisa Katoliki.

Binafsi naamini wamwera wapo wengi sana TISS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…