Waliotengeneza huu mfumo au hichi kitengo cha usalama wa taifa enzi hizo, walisahau kitu kimoja cha muhimu sana. Kama huu mfumo au hichi kitengo kimefanikiwa kwa viwango na namna kubwa ya kipee kama hii, yaani miaka 60 ya usalama kamili kitaifa. Nina imani kitu walichokisahau waanzilishi kipindi hicho, kingefanikiwa kwa viwango vikubwa vivohivyo. Huu mfumo au hichi kitengo ni ushuhuda tosha kwamba mifumo ni vitu imara na muhimu sana kwa taifa lolote lile.
Waanzilishi walisahau kuanzisha mfumo/kitengo "binafsi" cha kuratibu, kupanga na kusimamia maendeleo ya taifa zima kiujumla kwenye kila sekta, kuendana na mabadiliko ya kidunia na mataifa makubwa. Sababu usalama wa taifa hauna maana kubwa sana kama nchi haina maendeleo. Tuko salama, sawa. Lakini wananchi wanalia na wanakufa njaa.
Maendeleo kumaanisha: Matumizi ya kodi kimipango, usimamizi wa mikataba ya kimataifa, matumizi ya rasilimali nchi, uboreshaji na matumizi ya tehama kimipango, uboreshaji wa mfumo wa elimu... Nk.
Nina uhakika huo mfumo/kitengo hakipo. Na kama kipo basi kimezorota au sio cha kariba niliyoisema na ninayomaanisha. Na maendeleo ya kitaifa badala ya kusimamiwa, kuamuliwa na kupangwa na maamuzi ya mtu mmoja ambaye hamjui anafikiria nini kutokana na uwezo wake kiakili. Maendeleo ya taifa yangekuwa yanasimamiwa na kupangwa na huu mfumo/kitengo. Chini ya watu makini maalumu wenye akili, elimu na maarifa juu ya kila kitu kinachopaswa kutekelezwa ili kuendeleza na kwa faida ya Taifa.
Binadamu hubadirika kila siku, mifumo hubaki milele na huboreshwa ili kuboresha taifa zaidi.
Ndani ya miaka 60 iliyokatika nina uhakika tungekuwa superpower Africa.